Wananchi wa Dar kaeni Mkao wa kula,vyuma vipya piruuu vya Mwendokasi mda wowote citashushwa tayari kuanza kutumika.ππ
My Take: Rais Samia Huwa anawajibu Wapinga Maendeleo Kwa Kazi Zinazoonekana.
======
Scania Tanzania wameandika hivi kwenye kurasa zao za mitandao ya kijamii:
Habari wadau!
Huu ndio muonekano mpya wa basi la BRT kutoka Scania na Marcopolo! Hivi karibuni litaongezwa kwenye kikosi cha DART. Safari yako ya kila siku sasa inapata sura mpya, basi hili siyo tu la kuvutia, bali ni la kisasa kabisa!
Tazama video hii uone muundo wa nje wa basi hili, linaloleta mabadiliko kwenye usafiri wa umma Dar es Salaam. Endelea kufuatilia kwa maelezo zaidi! π
Umesema yatafika hivi karibuni hizo lugha watanzania tumechoka.Yafike kwanza
Haya tueleze wewe unaposema yatafika karibuni .Hiyo karibuni maana yaje nini? Ni lini hiyo exact date? Lugha hizo za karibuni ni za kikaghai hizo.Taja lini? Eti hivi karibuni hiyo si sawa tu na yale maneno ya tuko mbioni kuleta haileweki mbio fupi ,ndefu na zitaisha lini.Hiyo.karibuni yako maana yake nini?
Kuna step umeiruka. Wapo kwenye mchakato na baadae wataufanyia upembuzi wa awali na matokeo yakiwa mazuri wataingia kwenye upembuzi yakinifu kabla ya kuingia kwenye procurement processes ambazo huchukua muda. Endeleeni kuwa watulivu.