Samcezar
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 13,095
- 22,731
Upate connection zao vizuri. Wengi wao huwa wanawapa kazi madereva wao ya kuuza na mwisho wa siku madereva wanawatonywa madalali au wenyewe wanakuwa madalali. Hii kitu huwa inaboa sana.....Kuna mdau fulani anahusika sana na magari aliniambia kama unataka gari ya kununua hapa bongo bora ununue kwa wahindi au waarabu wa kkoo. Wale jamaa wanatunza sana magari yao halafu pia hayapati dhoruba sana kama haya mengine. Utakuta gari inazunguka hapohapo kkoo au posta na upanga.
Na pia hao jamaa wanauza gari nzuri sana kwa bei chee kwasababu wanataka kuleta nyingine mpya zaidi.
Mimi madalali huwa siwapendi hata kidogo.