Muongozo wa kununua vifaa vinavyotumia processor za intel

Muongozo wa kununua vifaa vinavyotumia processor za intel

Yah! Ina slots mbili za hard drive, ila na waswas na speed kama ntamix na hiyo 128/256 SSD kama ulivosema!
speed ya ssd haihusiani na ukubwa, unaweza kuwa na ssd ya 128gb na ikawa na speed sana.

na ili ufurahie speed ya ssd inabidi operating system iwe ndani ya hio ssd, na program zako pia ziwe ndani ya ssd.

vitu kama nyimbo, movie, picha, documents etc hivi ndio vinakaa kwenye Hdd.
 
mkuu ivi unaweza badilisha procesor ikiwa ndogo uiupgrade iwe kubwa...?
ndio inawezekana ila kwa generation moja,

kama laptop ni ya zamani basi na cpu yake ya ku upgrade ni ya kizamani vile vile.

mfano computer ya core 2 duo una upgrade na core 2 duo mwenzie au core 2 quad huwezi ukaeka i7 au i5 ya kisasa
 
ndio inawezekana ila kwa generation moja,

kama laptop ni ya zamani basi na cpu yake ya ku upgrade ni ya kizamani vile vile.

mfano computer ya core 2 duo una upgrade na core 2 duo mwenzie au core 2 quad huwezi ukaeka i7 au i5 ya kisasa
ASNTE MKUU NAOMBA NIONGEZEE IVI KWA DELL LATITUDE D 430...NAWEZA NIKAIFANYA IKAWA NA SPEED KUBWA?
 
2gb...lakini speed ni ndogo sana muda mwingine nikiplay video zenye uwezo mkubwa zinascrach....
video mara nyingi ni issue ya gpu, unatumia player gani? download media player classic (mpc) ndio inaplay video nyingi kwenye pc zenye uwezo mdogo.
 
huko Duniani 2TB yenye speed nzuri kama samsung evo inauzwa dola 600 hadi 700, sitashangaa bongo ikiwa milioni 2 au zaidi.

labda kama pc yako inakubali kuingia HDD mbili ununue ssd ya 128gb au 256gb kwa ajili ya OS na program zako muhimu, huwa hakuna faida vitu kama miziki, picha na video vikiwa katika ssd.

muone Krait anajua duka wanalouza
kuna duka lingine lipo mtaa wa jamhuri au Bara bara ya samora(sina uhakika) 128GB wanauza 250k!! sipati picha 2TB itakuwa sh. Ngapi!! Naona afadhari ya mtaa wa uhuru wanayouza 180k-150k kwa 128GB, Chief-Mkwawa kuna duka niliulizia posta wakanambia zipo SSD za CHIP za kawaida hawana sasa hapa nikashindwa kuelewa, maana ebay niloziona zinazofanana na HDD, je? Hizi za Chip zinaweza kubali kwenye Dell Latitude E6400?
 
kuna duka lingine lipo mtaa wa jamhuri au Bara bara ya samora(sina uhakika) 128GB wanauza 250k!! sipati picha 2TB itakuwa sh. Ngapi!!
Nlikuwa nakusubiri mkuu, linaitwaje hilo duka tafadhali?
 
kuna duka lingine lipo mtaa wa jamhuri au Bara bara ya samora(sina uhakika) 128GB wanauza 250k!! sipati picha 2TB itakuwa sh. Ngapi!! Naona afadhari ya mtaa wa uhuru wanayouza 180k-150k kwa 128GB, Chief-Mkwawa kuna duka niliulizia posta wakanambia zipo SSD za CHIP za kawaida hawana sasa hapa nikashindwa kuelewa, maana ebay niloziona zinazofanana na HDD, je? Hizi za Chip zinaweza kubali kwenye Dell Latitude E6400?
ssd ni speed, huwa mara nyingi utofauti wa bei ni kutokana na speed ila 250k still ni kubwa hata kwa yenye speed.

chip ya kawaida amemaanisha sata? ungeenda na laptop akakuekee mwenyewe.
 
ooohh! Ni mtaa wa uhuru kama unaelekea Posta nikipita nitaangalia jina, maana sikulikalili
 
Computer nyingi tunazonunua huwa zinatumia processor za intel au amd, lakini ni intel ambaye ametawala sana kushinda amd kwenye computer zetu. Leo nimeamua niandike uzi huu kuhusu hizi processor za intel na namna ya kuzichagua ili kuwasaidia watu wanapotaka kununua laptop/desktop mpya wafanye maamuzi sahihi.

Processor ni nini?

Labda utakuwa unajiuliza kwa nini ukitaka kununua laptop mpya unatakiwa uangalie processor? Nini cha muhimu kuhusu hii processor?

-Kwa lugha rahisi processor ni kifaa ndani ya computer yako kinachobeba maagizo ya program za computer. Maagizo hayo yanaweza kuwa ya kimahesabu, kimantiki, maagizo yanayoingia kwenye computer na yanayotoka.

-jinsi processor inavyokuwa na speed kubwa ndio jinsi maagizo yatakavyofanywa haraka na ndio jinsi program za computer zitakavyofanya kazi upesi.
processor_01.jpg


Familia ya processor za intel

Intel wana processor za aina nyingi na ni ngumu kuzitaja kwa pamoja, ila wameturahisishia kwa kuzipanga processor zao kwenye familia. Na hii ndio familia yao.

1. Atom processor- processor hizi hutumika kwenye vimini laptop na tablet ni ndogo kiumbo ndio maana hata vifaa vyake ni vidogo, processor hizi hazina nguvu sana na vifaa vyake hukaa sana na chaji.

2. Celeron processor- Haina tofauti sana na atom ila hii ina afadhali kidogo. Inatumika kwenye vifaa vikubwa kuliko atom kama vile laptop kubwa na desktop

3. Pentium- hii ina speed kuliko celeron na atom pia inatumika kwenye vifaa vikubwa.

4. Core 2 duo- hii ni maarufu kwa perfomance yake ya multitasking, inauwezo wakufanya mambo mengi kwa wakati mmoja ila nyingi ni za kizamani.

5. Core i3- hii ni processor latest za intel ni dual core lakini core zake zina perfomance kubwa na pia inakuwa na thread 2 kwenye kila core, ni nzuri kwa wanaotaka perfomance kubwa kwa bei rahisi.

6. Core i5- ya laptop ni dualcore na ya desktop ni quadcore isiyokuwa na thread, software nyingi kubwa duniani zimekuwa optimized kutumia core kama za i5, ni nzuri sana kwa watu wanaotumia software zinazodemand perfomance lakini hawafanyi multitasking.

7.Core i7- hii inakuwa na quadcore processor na thread 8 kwenye desktop na pia inaweza kuwa dualcore kwenye laptop. Hii ndio processor nzuri zaidi kwa watu wa kawaida na inafanya multitasking hata kama software zinademand sana.

8. Xeon- hii ndio processor yenye speed zaidi kwenye processor za intel lakini imekuwa designed kufanya kazi kwenye computer kubwa kama vile server. Unapohost website processor kama hii ndio inayoprocess webpages.


Generation ya processor(muhimu)

Ni muhimu sana kujua processor inatokea generation ipi kuna processor zenye i7 ya 2010 ambazo zipo slow vibaya mno, na pia kuna uwezekano i3 kuipita i7 kwenye perfomance kama zinatoka generation tofauti. Hivyo eneo hili inabidi uwe makini kuepuka kuuziwa mbuzi kwenye gunia. Hivyo unaponunua laptop/desktop ni lazima ujue ipo generation gani la sivyo upo hatarini na hivi ndio namna ya kujua.

- Processor yenye namba inayoanziwa na elfu nne ni fourth generation(4xxx)
Mfano Intel i3-4130.

- Processor yenye namba inayoanziwa na elfu tatu ni third generation (3xxx)
Mfano i3-3130.

- Processor inayoanziwa na elfu mbili ni second generation(2xxx)
Mfano i3-2140

Sishauri kabisa kununua processor ya first generation, mtu unatakiwa atleast ununue ya second generation na pia bei inatakiwa iwe ndogo kwa hii second compare na third/fourth.

Processor ndogo kama atom na celeron zina generation zake ambazo ni
-clover trail
-bay trail

Processor za zamani za atom zilikuwa mbaya sana na zipo slow ila baytrail ikaja kuzipa nguvu na kuzifanya ziwe na perfomance kubwa, hivyo kama unataka kifaa cha atom/celeron make sure processor yake iwe inatoka generation ya baytrail.


Herufi za mbele ya processor(muhimu)

Kama umechunguza mbele ya processor kunakuwa na herufi mbali mbali hizi pia ni muhimu sana kuzijua kwani usipozizingatia unaweza kujuta.

Mfano processor inaweza kuitwa i5-4000m au i5-4000u au i5-4000y je nini kinatofautisha hizi processor?

1. Herufi kwenye processor za desktop.

Bila herufi &[HASHTAG]#8211[/HASHTAG]; hii inakuwa na speed halisi ya processor mfano i7-4770

K- herufi hii inamaanisha processor ipo unlocked na unaweza kui over clock na kuongeza speeed. Processor yenye 3.5ghz unaweza kui overclock ikafika 4ghz. Jina lake linakuwa mfumo huu i7-4770K. ni nzuri sana kwa wanaocheza magame na kufanya rendering.

R- herufi hii inamaanisha processor hii ni ndogo sana na inaweza kutumika kwenye videsktop vyenye umbo dogo hali ya kuwa ina graphic kubwa kama iris pro. Jina lake linakuwa mfumo huu i7-4770R hii ni nzuri kwa wale wenye ofisi ambazo ni safi hawataki mawaya mengi na desktop kubwa kukaa kwenye meza. angalia picha hapo chini uone desktop ndogo.

brix1_s.gif


S- herufi hii inamaanisha hiyo proceesor wame optimize perfomance mara nyingi wanai underclock kuzuia processor kupata joto sana. Mfano i7-4770 ina 3.4ghz lakini i7-4770S ina 3.1ghz tu, ina maana hapa wamepunguza 300mhz kutoka stock kuja S.

T- herufi hii inamaanisha processor inatumia power ndogo, kwa wale wenzangu wanaotumia luku kama unataka desktop isiokula umeme basi hii ndio yenyewe ila perfomance nayo itapungua kidogo. Mfano wa jina ni i7-4770T

2. Herufi mbele ya processor za laptop(mobile)

Tumeshaona herufi mbele ya desktop, sasa hivi tuangalie herufi mbele ya processor za laptop ambazo pia zinaweza kutumika kwenye home theatre pc (htpc) au wengine wanaita mini desktop.

M- herufi hii inamaanisha hio processor ni mobile, ndio herufi common kwenye processor za laptop mfano i5-4000M

U- herufi hii inamaanisha processor ya laptop inatumia power ndogo hizi processor zinatumika sana kwenye vilaptop vyembamba (ultrabook). Kwa sababu zinakaa na chaji kutokana na kutumia power ndogo, perfomance yake nayo pia ni ndogo. Mfano i5 4250U

Y- hii ni ultra low power yaani inakula umeme mdogo kushinda hata U lakini vile vile perfomance inazidi kushuka nayo mfano i7-4610Y

HQ- herufi hii inamaanisha high perfomance, zinauzwa bei ghali sana na power yake inashindana na desktop. Usije ukajaribu kuieka kwenye mapaja laptop ya design hii maana zinashika moto upesi sana kutokana na quality ya processor. Ni nzuri kwa wale wanaopenda kucheza game, kutumia software kubwa wakiwa kitandani. Mfano ni i7-4700HQ

MQ- herufi hii inamaanisha hio procesor ni quad core. Kama umesoma vizuri juu i5 na i7 za desktop ni quadcore lakini za laptop ni dualcore, hivi processor hii inamaanisha unaweza tumia quadcore kwenye laptop yako kama unataka mfano i7-4900MQ

MX- herufi hii inamaanisha ni xtreme edition, processor hii unaweza kui over clock kama vile K series ya desktop na ina perfomance kubwa sanaaa, ila kuwa makini na mapaja tu.
Mfano i7-4940MX

Huu ndio muongozo wa kununua processor za intel, kama kuna sehemu hujapaelewa unaweza kuuliza nitaelezea zaidi.
Boot device not found!!! Kwenye pc naomba msaada hapo mkuu kama una utaalamu kuhusu hilo
 
Mkuu Chief Mkwawa naomba muongozo wako;
1.je ninaweza kubadilisha CPU kutoka i5-6200U kwenda i7?

2.naomba muongozo jinsi ya kufanya partition Hard Disc, ni machine mpya sasa nataka kutenganisha storage ya systeam files ijitegemee kivyake. ukubwa wa HDD ni 1000GB.
 
Mkuu Chief Mkwawa naomba muongozo wako;
1.je ninaweza kubadilisha CPU kutoka i5-6200U kwenda i7?

2.naomba muongozo jinsi ya kufanya partition Hard Disc, ni machine mpya sasa nataka kutenganisha storage ya systeam files ijitegemee kivyake. ukubwa wa HDD ni 1000GB.

1. unaweza ndio ila i7 za u nazo ni dual core na hyperthread hazina maana, utofauti wa perfomance kati ya i5 6200u na i7 6500u ni mdogo sana kama 10% tu.

2. kufanya partition ni rahisi tu, tumia tool inayokuja na windows ya disk management, soma zaidi hapa

How to Partition Windows 10 Free – EaseUS
 
Mkuu CHIEF MKWAWA kuna hii desktop ya Hp Compaq yenye specifications hizi:
Intel(R) Pentium(R) 4 CPU 3.06 GHz 3.06 GHz, 496 MB of RAM..
Nataka ku_upgrade RAM, je RAM yenye ukubwa gani itafaa na inapatikana vipi na kwa shilingi ngapi..!? Je hiyo processer ipo vizuri..!?
 
Back
Top Bottom