Muongozo wa kununua vifaa vinavyotumia processor za intel

ahsante sana, na hizo processor zina generations yani mfano,kwa ufinyu wa budget mi pc yango ni core i3, sasa wakati nafanya uchaguzi nikaambiwa nichague fourth generation, naomba utujuze na generations za hizo processors tofauti ni nini?
 
ukichagua processor bila generation ni rahisi kuuziwa bidhaa mbaya, kifupi ni kwamba i3 generation ya 6 ina nguvu kuliko i7 generation ya kwanza pitia hapa kujua generation
Muongozo wa kununua vifaa vinavyotumia processor za intel

generation ya 4 kwa processor zinazoishiwa na M ndio bora zaidi kwa sasa tukizungumzia perfomance unayopata na bei utakayouziwa kwenye laptop.

ila kama unataka overall processor nzuri kuanzia ulaji mdogo wa umeme, gpu nzuri, perfomance kubwa bila kujali bei basi generation ya 6 ndio bora zaidi.

mwishoni wa mwaka huu generation ya 7 itaingia sokoni ambayo ni nzuri zaidi
 
Naomba unifahamishe kuhusu uwezo wa hii processer ya laptop yangu ni
Intel(R) Core (TM) i5 CPU M 520 @2.40GHz 2.40 GHz
Natanguliza shukrani.
 
Naomba unifahamishe kuhusu uwezo wa hii processer ya laptop yangu ni
Intel(R) Core (TM) i5 CPU M 520 @2.40GHz 2.40 GHz
Natanguliza shukrani.
hio ni generation ya kwanza mkuu, sababu inatoka familia ya M ina nguvu kiasi chake, mambo yote ya kawaida itayafanya vizuri ila itapata shida kwenye mambo yanayohitaji zaidi gpu kama vile gaming, japo si games zote utashindwa kucheza
 
Shukrani tena mkuu
 
Kaka shukrani sana kwa huu msaada,mi nna shida moja ,hivi unawezaje kujua size ya GPU kwenye pc(Laptop/desktop) endapo ikiwa imewashwa,kwa window au kama haina window .
NATANGULIZA SHUKRANI
 
Kaka shukrani sana kwa huu msaada,mi nna shida moja ,hivi unawezaje kujua size ya GPU kwenye pc(Laptop/desktop) endapo ikiwa imewashwa,kwa window au kama haina window .
NATANGULIZA SHUKRANI
ikiwa imewashwa nenda sehemu ya search andika neno dxdiag kitakuja hiko kiprogram, click itakuonesha cpu, gpu, audio, input etc

kama haijawashwa ni kuangalia either sticker pale mbele au kuangalia kwenye kitako model number na kuigoogle.

ila tu kuwa makini gpu haiangaliwi kwa vram, ikiwa na ram kubwa haimaanishi kwamba ndio nzuri kama watu wengi walivyozoea
 
Uzi huu utanisaidia kununua laptop mwezi wa 11, mie ni mtumiaji wa kawaida sihitaji laptop ya kiurahisi ila ninataka laptop nzuri hivyo si vibaya kunishauri ili siku ikifika nifanye maamuzi (mfano natenga budget ya laki 7 mpaka milioni, hapa sipati kweli kitu kizuri?)
 
minimum budget yako kwa hio laki 7 hadi 8 unapata core i3 six generation i3 6100u. ukienda hadi milioni 1 unaweza kupata i5 6200u.

ila siku yoyote ile 7th generation inatoka ambayo itakuwa nzuri zaidi pengine mpaka hio mwezi wa 11 ikawa laptop zake zipo mitaani napo kutakuwa na cpu za i3 7100u na i5 7200u kwenye budget yako.

kwa brand budget yako nakushauri tafuta business class brand kama lenovo thinkpad au dell latitude etc

pia kama unapenda uzuri unaweza kutafuta brand zenye muonekano mzuri kama hp envy au spectre, dell xps na asus zenbook
 
Noted mkuu ikifika siku nitapitia uzi wote pia na window shopping ya wiki nzima alafu nakuwa naomba ushauri kwa specifications nitazaziana kabla ya kufanya manunuzi
 
Noted mkuu ikifika siku nitapitia uzi wote pia na window shopping ya wiki nzima alafu nakuwa naomba ushauri kwa specifications nitazaziana kabla ya kufanya manunuzi
mkuu siku zote ukipatia processor automatic specs nyengine nazo zinakuwa vizuri. mfano ingia amazon andika i3 6100u laptop then zitakuja laptop zote zenye hio processor utaona zina ram kuanzia 4gb, hdd ni 500gb kupanda webcam etc

vitu muhimu vyengine vya kuangalia ni ssd, laptop zenye ssd zinakuwa na speed zaidi kuliko zenye hdd, sema bei ya ssd 128gb ni sawa na hdd 1tb. hivyo utaangalia kama huna mambo mengi ya kuhifadhi ssd ni bora zaidi kama una mambo mengi nunua ya hdd baadae ukipata hela nyengine utaitoa hio hdd na kueka ssd.

chengine ni display, laptop nyingi zinakuja na HD ya kawaida yaani 1366x768 ila ukipata display ya full HD ni bora zaidi 1920x1080 na ni vyema ikawa ni Ips panel ili uone vizuri hata kama utakuwa huiangalii laptop direct
 
nashukuru sana Mungu akuzidishie .. na mimi ni mmoja wapo waliokuwa wanaangalia RAM kubwa nakuitrust PCπŸ˜€πŸ˜€
 
Naomba kujuzwa kuhusu uwezo wa hii processor Intel(R) Core (TM) i5 - 2540M CPU @ 2.60 GHz na kwa upande wa games ipoje. Asanteni
 
Hii thread ni nzuri mno,can somebody teach me how to download it?[emoji1]
Mkuu kui-download kivii mkuu?njia nyingine nzuri kama kitu kimekuvutia una reply kama ulivyofanya inakuwa ipo kwenye kumbukumbu yako kwenye profile au unacopy link na kui-paste popote kisha unasave kwenye document zako ambazo ni za muhimu, ukihitaji una-click link tu
 
nashukuru sana Mungu akuzidishie .. na mimi ni mmoja wapo waliokuwa wanaangalia RAM kubwa nakuitrust PCπŸ˜€πŸ˜€
laptop chache sana duniani haziruhusu kuongeza ram, naweza kwenda kkoo nikanunua laptop used ya 150,000 nikanunua hdd ya 1tb kwa 100,000 na ram 4gb kwa 30,000 jumla gharama ni 280,000 hapo sababu we unaangalia ram na storage ukiingia kichwa kichwa utauziwa laki 6 hadi 8. cpu na gpu ni muhimu sana sababu ni ngumu kuongezeka.
 
Naomba kujuzwa kuhusu uwezo wa hii processor Intel(R) Core (TM) i5 - 2540M CPU @ 2.60 GHz na kwa upande wa games ipoje. Asanteni
hizi cpu za laptop zinazoishiwa na M ni nzuri sana hio cpu ina uwezo wa kucheza games nyingi za kisasa, kitu kitakachokukwaza ni kwamba gpu yake yaani intel hd 3000 sio nzuri sana, games kama za Fifa, Pes, magari, zitacheza bila matatizo ila games kubwa kubwa kama witcher 3, gta v, fallout 4, arma 3 etc zitakusumbua. ila nafikiri ukieka resolution ndogo kabisa kama 360x640 au 480x800 unaweza cheza hadi games kubwa.
 
Asante sana Mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…