Muongozo wa kununua vifaa vinavyotumia processor za intel

Mkuu hivi hii processor yangu iko sawa kweli? naweza kuiongeza? naweza kucheza game?View attachment 1820384
Processor ipo vizuri Mkuu na huwezi kuiongeza.

Hii machine ina gpu dedicated ama ni hii hii inayokuja na cpu? Kama ni hii utacheza games nyingi ila za kisasa utacheza kwa quality ndogo na baadhi hazitarun kabisa.
 
Wakuu wapi naweza pata motherboard ya hp 15 Da kama inavyooneka kwenye picha maana nimempatia fundi anadai kashindwa ipata
 
Ni laptop hii? Kama fundi ameshindwa ni kuagizishia tu nje.
Ndio ni laptop ilipigwa short na cable ya ethernet as if ilikuwa cable ya umeme,wasiwasi wangu ni kupata exactly na iliyoungua. Je nikipata motherboard ya i7 na iliyokuwepo ni i5 je itakubali kufanya kazi?na kama ni ndio hakuna madhara katika performance?
 
Ndio inafanya, na hakuna madhara performance itaongezeka kama inakuja na cpu built in. Sema iwe model moja tu.
 
Naomba kufahamu kuna aliyejaribu kutumia computer monitor kama TV!? Nikimaanisha kuconnect decorder mfano Azam na monitor kwa kutumia HDMI cable?
Inadisplei Full HD vizuri?
Je kuna extra device inahitajika!?
 
Kama monitor ina hdmi huhitaji extra device, incase monitor haina speaker (nyingi hazina) utahitaji speaker za nje kwa ajili ya sauti.

Na azam ama King'amuzi chochote kibongo bongo havina full HD.
 
Kama monitor ina hdmi huhitaji extra device, incase monitor haina speaker (nyingi hazina) utahitaji speaker za nje kwa ajili ya sauti.

Na azam ama King'amuzi chochote kibongo bongo havina full HD.
Mkuu habari,

Naitaji gpu ambayo ntacheza game zote kwa high setting hii ninayo tumia naweza kucheza game zote ila hizi latest nashuka mpk lowest setting

Pia naitaji isiwe high profile nimeona iz 1050ti vp zinaweza kuwa nauwezo huo

Pia ni kipi kingne niapgrade kwenye pc yangu ili nipate setting nzuri kwakila game
 
Pia nasikia 1650ti nayo ni kari zaidi
Ndio 1650 kwa sasa ndio low profile nzuri zaidi, Sema subiria kidogo 3000 series zina roll out.

Halafu bei za gpu ni ndefu sana kwa sasa hasa hizi zinazo kula umeme kidogo watu wa crypto wamepandisha bei. Utaambiwa milioni na upuuzi.
 
Dah! Me nilijiua high profile ndio ziko juu sana
 
Hizo zinazotumia umeme wa nje zina nguvu zaidi rtx 3090 ina nguvu kama Mara 4 hivi ya 1650.
Mkuu nimejaribu kuangalia pia benchmark ya rx 550 4gb lakini mbona hata 4gb yake haina parfomance kubwa kiivyo yahn kama ni frame rate inanizid 10 au 15 so hapa inavyo onekana ni kwamba kila gpu ina parfomance yake
 
Mkuu usiangalie performance ya Gpu kupitia ram. Kabla haijatoka Gtx 1650 rx 550 na gtx 750Ti ndio zilikua Gpu nzuri kwenye low profile na desktop zetu hizi za Ki masikini.

Lakini ukicompare Gpu zote rx 550 still ni lowend.

Tumia benchmarks mbalimbali kuangalia performance online na sio ram.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…