Muongozo wa kununua vifaa vinavyotumia processor za intel

Mkuu Chief Mkwawa, kuna Msela angu mmoja ana laptop aina ya Asus (spec sijazijua) ila ina tatizo kwenye casa inacheza cheza hovyo tatizo litakuwa nini hapo?
 
mkuu siku zote ukipatia processor automatic specs nyengine nazo zinakuwa vizuri. mfano ingia amazon andika i3 6100u laptop then zitakuja laptop zote zenye hio processor utaona zina ram kuanzia 4gb, hdd ni 500gb kupanda webcam etc

vitu muhimu vyengine vya kuangalia ni ssd, laptop zenye ssd zinakuwa na speed zaidi kuliko zenye hdd, sema bei ya ssd 128gb ni sawa na hdd 1tb. hivyo utaangalia kama huna mambo mengi ya kuhifadhi ssd ni bora zaidi kama una mambo mengi nunua ya hdd baadae ukipata hela nyengine utaitoa hio hdd na kueka ssd.

chengine ni display, laptop nyingi zinakuja na HD ya kawaida yaani 1366x768 ila ukipata display ya full HD ni bora zaidi 1920x1080 na ni vyema ikawa ni Ips panel ili uone vizuri hata kama utakuwa huiangalii laptop direct
Mkuu, hii display unaiangalia vipi kwenye laptop?
 
mkuu hizo bei ni nzuri kupita kiasi mpaka napata wasi wasi anaweza kuwa tapeli.

kwa heavy task hio i5 7300HQ au i7 yake yaani 7700HQ na nvidia 1050ti inakufaa. ila hakikisha hio i7 ni kama hio nilioitaja na sio ile inayoishia na u kama 7600u.

hizo zinazoishiwa na HQ zina core nyingi i5 ni core 4 na thread 4 wakati i7 ni core 4 na thread 8. ila kama unafanya multithreaded works nyingi kama video editing itakufaa zaidi hio i7.
Chief-Mkwawa mchango wako wa utaalam ni msaada mkubwa pengine kuliko unavyofahamu! Bravo
 
chief mkwawa,ninalaptop ya dell core i5 ram 4 na processor 2.7 lkn inazingua mwanga nimeongeza mpaka mwishoo lakin autoshii,afuu ikiwa imewaka fenii inauguruma,tatiz niii ninii?
 
Mkuu Chief Mkwawa, kuna Msela angu mmoja ana laptop aina ya Asus (spec sijazijua) ila ina tatizo kwenye casa inacheza cheza hovyo tatizo litakuwa nini hapo?
akiwa anatumia au hata akiwa hatumii?

laptop za kisasa touchpad zake ni multitouch, zimetengenezwa ili uweze ku apply gestures za windows 10, hivyo zina sense mguso zaidi ya mmoja, inapotokea kuna kitu kimegusa touchpad kama vile kiungo chako cha mwili au uchafu, then na kidole chako pia kinagusa hapo kunakuwa na miguso miwili na utaona cursor ina ruka ruka au inaji right click etc.

sometime linakuwa ni Tatizo tu la touchpad, inaweza kuwa imeharibika.

njia rahisi ni kununua mouse ya nje, au aibadilishe hio touchpad.
 
chief mkwawa,ninalaptop ya dell core i5 ram 4 na processor 2.7 lkn inazingua mwanga nimeongeza mpaka mwishoo lakin autoshii,afuu ikiwa imewaka fenii inauguruma,tatiz niii ninii?
umeeka drivers za graphics? na hio i5 yako ni ipi? nenda my computer halafu right click then properties utaona jina la hio i5.

na feni linaunguruma pc ikipata joto, likiwa linaunguruma nenda task manager ili ujue nini kinaungurumisha, kwenda task manager right click chini kwenye task bar kisha chagua task manager.

sshot-31.png
 
Mkuu, hii display unaiangalia vipi kwenye laptop?
kwenye computer yako bonyeza search kisha andika hili neno

dxdiag

then kitatokea hicho ki dxdiag ki click then kitafunguka, click display utapata information hizo za resolution na aina ya display.
 
akiwa anatumia au hata akiwa hatumii?

laptop za kisasa touchpad zake ni multitouch, zimetengenezwa ili uweze ku apply gestures za windows 10, hivyo zina sense mguso zaidi ya mmoja, inapotokea kuna kitu kimegusa touchpad kama vile kiungo chako cha mwili au uchafu, then na kidole chako pia kinagusa hapo kunakuwa na miguso miwili na utaona cursor ina ruka ruka au inaji right click etc.

sometime linakuwa ni Tatizo tu la touchpad, inaweza kuwa imeharibika.

njia rahisi ni kununua mouse ya nje, au aibadilishe hio touchpad.
Hii casa inacheza cheza wakati wa kui point kwenye file haiwi stable kabisa yaani unaweza ukawa una_direct kwenye file flani lkn unakuta mara imeruka kwenda juu zaidi au Kwingineko na hata ikitulia kwenye file husika ukigusa tu TouchPad basi inahama tena na kuruka Kwingine.... Ila Thanks kwa hio suggestion yako ngoja nichek nazo!

Sent from my TECNO-J8 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu mi nataka kunua laptop kwa ajili ya gaming naomba mwongozo ni generation ya ngapi ya intel core i5 inakuwa na dedicated graphic memory kubwa
 
dedicated haina cha generation ipo generation zote, ila i5 nzuri kwa games ni zile zinazoishiwa na HQ ambazo zipo gen ya 6 na 7.

gen ya 6 ni i5 6300HQ
gen ya 7 ni i5 7300HQ

na gpu ni nvidia xx50 kupanda inafaa, mfano 750m, 760m 950m, 1050ti etc 1060, 1070, 1080 etc

pia usiangalie ukubwa wa memory kwenye graphics kama kigezo cha uzuri pekee. kuna gpu zina memory 8gb na zinapitwa na gpu za 1gb.

hizo i5 na dedicated gpu jipange kuanzia 1.5m kupanda ndio utazipata
 
umeeka drivers za graphics? na hio i5 yako ni ipi? nenda my computer halafu right click then properties utaona jina la hio i5.

na feni linaunguruma pc ikipata joto, likiwa linaunguruma nenda task manager ili ujue nini kinaungurumisha, kwenda task manager right click chini kwenye task bar kisha chagua task manager.

sshot-31.png
sijakuelewaa chief,niniii maana ya graphic na kishafika kwenye task manager nifanyee ninii chief
 
drivers za graphics ndio zinazo controll mwanga, na graphics (gpu) ni kifaa ndani ya laptop yako ambacho kinacontroll visual, kama vile kuplay video, kucheza games, etc.

ukifika kwenye task manager itakuonyesha ni kwa kiasi gani processor, ram na harddisk inatumika, hapo ikiwa inaunguruma.
 
nimechekii wameonesha CPU 0%,memory 42% disk0%
 
drivers za graphics ndio zinazo controll mwanga, na graphics (gpu) ni kifaa ndani ya laptop yako ambacho kinacontroll visual, kama vile kuplay video, kucheza games, etc.

ukifika kwenye task manager itakuonyesha ni kwa kiasi gani processor, ram na harddisk inatumika, hapo ikiwa inaunguruma.
sasa chief tatizoo LA mwanga tunalisolve vpp?? msaada piaa na fenii kuunguruma
 
Back
Top Bottom