Muongozo wa kununua vifaa vinavyotumia processor za intel

Muongozo wa kununua vifaa vinavyotumia processor za intel

Jinsi socket inavyokuwa latest ndio Jinsi ilivyo nzuri hata kama socket ya 765 ni nzuri itakusaidia nini kama cpu zake ni slow sana? Hivyo vipini ni design tu, usiviweke sana kichwani na kukuinfluence kwenye mawazo yako wakati unachagua pc.

Jaribu pcpartpicker ukichagua motherboard itakupa aina cpu and vice versa, pia Wikipedia wanakuwa na hizi list
Mfano hii
Ukiclick motherboard husika ina kupeleka moja kwa moja site ya Intel unaona na support.

Xeon ni professional cpu japo zinatumika same architecture na Cpu za kawaida, motherboard zake ni tofauti, huwa kimakusudi Intel wanazitofautisha na motherboard za majumbani kawaida, kuna baadhi ya mods watu wanafanya lakini kurun xeon kwenye mobo za kawaida, na motherboard za xeon zinakuwa na Bei ndefu sana.

Uzuri wa motherboard si hizo socket Bali ni features nyengine, fatilia H series, B na Z series zaidi kuliko socket, socket ipo hivyo Sababu ya maamuzi tu na design ambazo zipo nje ya uelewa wetu watumiaji wa kawaida.

Kama nilivyosema juu motherboard nzuri si socket Bali ni series yake, motherboard ya elfu 60 na motherboard ya milioni 1 zote zinaweza kuwa na socket moja, ukipata motherboard Z series high-end ndio inakuwa nzuri zaidi utapata features za kisasa kama
-uwezo wa ku overclock,
-support ya frequency kubwa
-slot nyingi za ram
-slot nyingi za storage
-optical audio
-wifi 6
-gigabit ether net etc

Mfano Angalia hii
Amazon product ASIN B087LHPYT6
Hivyo socket ni lazima iwepo ile ile Haijalishi ni motherboard ipi ila features zinabadilika baina ya H, B na Z motherboard.
Shukrani sana mkuu!🙏🙏🙏

1.Hivi mkuu motherboard mpya kutoka dukani inakuwa haina chochote?Namaanisha kuwa huwa inakuja bila CPU,GPU,RAM,HDD/SDD?

2.Hivi mkuu hii series ya motherboards ya 100,200,300,400 na 500 zinapatikana bongo?Na kama zinapatikana hapa bongo bei zake zipoje hasa kuanzia series ya 300?Kwa hapo bongo used bei zake zipoje na mpya bei zake zipoje?Nje used bei zake zipoje na mpya bei zake zipoje?(Mkuu hapa naulizia hizi za matumizi tu ya kawaida siyo akina Z.Nazungumzia akina H)
 
Shukrani sana mkuu!🙏🙏🙏

1.Hivi mkuu motherboard mpya kutoka dukani inakuwa haina chochote?Namaanisha kuwa huwa inakuja bila CPU,GPU,RAM,HDD/SDD?
Ndio haina chochote
2.Hivi mkuu hii series ya motherboards ya 100,200,300,400 na 500 zinapatikana bongo?Na kama zinapatikana hapa bongo bei zake zipoje hasa kuanzia series ya 300?Kwa hapo bongo used bei zake zipoje na mpya bei zake zipoje?Nje used bei zake zipoje na mpya bei zake zipoje?(Mkuu hapa naulizia hizi za matumizi tu ya kawaida siyo akina Z.Nazungumzia akina H)
Na kibongo bongo zipo ila bei ghali kupita maelezo capricorn mjini wanazo.

Ambazo hupati kana kirahisi used ni hizi za kina dell na HP sema hizi zinakuwa modified utumie power supply zao tu.

nchi kama USA ama Malyasia na UAE (Dubai) ni rahisi kupata Motherboard kwa bei ya Rahisi unaweza agizishia.
 
Shukrani sana kaka.Hivi nikiwa na motherboard ambayo ni low end kama vile H310 LGA 1151 kisha nikaiweka CPU ambayo ni overclockable kama vile core i7-8700K, je hii CPU itakubali kufanya kazi?(CPU iliyowekwa haijafanyiwa overclocked)
 
Ndio inafanya, hutaweza tu ku overclock.
 
Celeron gen ya 8 ni dual core bado, hivyo i5 gen ya 4 inakuwa nzuri zaidi.

Sema kama ni desktop na una plan ya kuja kui upgrade baadae celeron gen ya 8 ina make sense zaidi maana utakuja kuweka i3/i5/i7 gen ya 8 mbele ya safari.
Mkuu samahani sijaelewa hapa!Unamaanisha kuwa inawezekana kuupgrade celeron gen ya nane kwenda core i7 generation ya 8 kama vile kwenda core i7-8550U?Inawezekana vipi wakati motherboard ya celeron ni ya zamani na hata haipo kwenye ile series ya intel ya 100,200,300?
 
Unaweza upgrade za desktop sio laptop.

Na celeron na Pentium zipo aina mbili gen za karibuni, pentium silver na Gold. Hizi pentium gold zinashare na i3/i5/i7 kwenye motherboard.
 
Unaweza upgrade za desktop sio laptop.

Na celeron na Pentium zipo aina mbili gen za karibuni, pentium silver na Gold. Hizi pentium gold zinashare na i3/i5/i7 kwenye motherboard.
Mkuu napata sana shida jinsi ya kujua generation ya CPU ambayo ni celeron au pentium.Ni mbinu ipi huwa inatumika kujua generation?
 
Mkuu napata sana shida jinsi ya kujua generation ya CPU ambayo ni celeron au pentium.Ni mbinu ipi huwa inatumika kujua generation?
Kwenye celeron na Pentium ni vurugu vurugu tu namba zake, wakilala wakiamak wanazipa majina mapya.

Vyema U Google, kama unataka gen ya 8 Google cpu upgrade i3 8100 itakuja results ya website ya Cpu upgrade utaona zote including celeron na pentium
 
Shukrani sana mkuu ila technically CPU zote ambazo zinaweza kuwa upgraded kwenda 8th generation ikiwa ni pamoja na hao akina celeron na pentium na wengine wengi maana yake wote hao wanashare socket ya LGA 1151 na wapo kwenye motherboard ya series ya 300?
 
Shukrani sana mkuu ila technically CPU zote ambazo zinaweza kuwa upgraded kwenda 8th generation ikiwa ni pamoja na hao akina celeron na pentium na wengine wengi maana yake wote hao wanashare socket ya 1151 na wapo kwenye motherboard ya series ya 300?
Ndio mkuu,
 
Kila laptop ina ssd ya Sata, hivyo unatoka hdd unaweka ssd.

Ila laptop baadhi zina separate port ya ssd unaweka hdd na ssd pamoja, hizi zinakuwa na m.2 ssd port.
Kaka nataka niupgrade laptop yangu kutoka core i5-6200U kwenda core i7-6500U.Je,hili linawezekana?
 
Desktop ni muhimu sana mkuu kama umeshajitosheleza. Sababu itakuwa mama wa vifaa vyako vyote kama TV, simu, Tablet, gaming console etc. Sio idea mbaya.
Mkuu nia yangu ni kujifunza,naomba unipe elimu angalao kidogo tu kuhusiana na ni kwa vipi desktop inaweza kuwa Mama wa vifaa vifuatavyo ulivyotaja:

1.TV
2.Tablet
3.Simu
4.Gaming console
5.etc

Sifa na utukufu zikufikie popote ulipo Chief.
 
Hayo ni matumizi Sasa, matumizi ni mengi.

Vyote hivyo vikiharibika ama kama unataka kuflash ama kumod software zake etc utaanza na computer kuseti mambo kabla hujaenda kwenye kifaa husika kumalizia.

Ukiwa na desktop nzuri na Router nzuri desktop yako inaweza tumika na vifaa vyote hivyo kucheza games, kuhifadhi mafile mbalimbali, kuangalizia movies etc.

Mfano Una smart TV unaweza Seti tu plex server ikawa direct ina chukua movie kwenye desktop na kuplay kwenye TV, ama Una steam link ina chukua games kwenye desktop na kuplay kwenye TV.

Mambo ni mengi sana.
 
Chief-Mkwawa naomba kuuliza kitu hizi namba huwa zinamaanisha nini
Intel HD Graphics 3000, 4000 au 5000 na ipi hapo ni bora zaidi?
 
Back
Top Bottom