Muongozo wa kununua vifaa vinavyotumia processor za intel

Muongozo wa kununua vifaa vinavyotumia processor za intel

Naomba msaada kila niki install window 10 pc yangu ina stack sasa sijui shida nn maana nilitumia power iso kutengeneza bootable flash lakn ikastack then nikatumia Rufus lakin wapi [emoji24][emoji24] Chief-Mkwawa
 
Naomba msaada kila niki install window 10 pc yangu ina stack sasa sijui shida nn maana nilitumia power iso kutengeneza bootable flash lakn ikastack then nikatumia Rufus lakin wapi [emoji24][emoji24] Chief-Mkwawa
Unatumia flash mkuu? Ikistack kuna error yoyote unapata?
 
Unatumia flash mkuu? Ikistack kuna error yoyote unapata?
Nimetumia Flash mkuu, alafu nikiwa naitumia inakuwa natumia inaganda kabisa yaan ina freeze hata kale ka cursor haka move kabisa sijajua shida iko wapi maana hiyo window 10 nilii download zamani nikaiweka kwenye external.
 
Wakubwa hii machine kwa price ya discount 450000/= ni sawa?
IMG-20230813-WA0011.jpg
IMG_20230813_123829.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakubwa hii machine kwa price ya discount 450000/= ni sawa? View attachment 2716171View attachment 2716172

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuwa makini kuna harufu ya utapeli hapa. Machine nzuri specs zake lakini unaona kabisa vitu vimeandikwa mara mbili mbili, mfano Display haiwezi kuwa Full HD halafu ikawa 2160p halafu 4k display, pia i5 yenye 8 cpu na dedicated vram 8GB haiwezi kaa kwenye slim design etc.

Mwisho wa siku huwezi pata Laptop zenye hizo specs kwa laki 4, mwambie akufanyie delivery ama akwambie duka lake lilipo usikubali kutuma hela online.
 
Kuwa makini kuna harufu ya utapeli hapa. Machine nzuri specs zake lakini unaona kabisa vitu vimeandikwa mara mbili mbili, mfano Display haiwezi kuwa Full HD halafu ikawa 2160p halafu 4k display, pia i5 yenye 8 cpu na dedicated vram 8GB haiwezi kaa kwenye slim design etc.

Mwisho wa siku huwezi pata Laptop zenye hizo specs kwa laki 4, mwambie akufanyie delivery ama akwambie duka lake lilipo usikubali kutuma hela online.
Mkuu ile pc yangu ya core i3 1005g1 nimeiongezea RAM na ninajipanga niiongezee SSD ya 256, sijui inauzajwe Sata ssd mkuu.
 
Mkuu ile pc yangu ya core i3 1005g1 nimeiongezea RAM na ninajipanga niiongezee SSD ya 256, sijui inauzajwe Sata ssd mkuu.
Ssd tafuta 512GB ama 1TB mkuu, zimeshuka sana siku hizi, zote mbili ni chini ya laki 1 ukitafuta vizuri.
 
Bei ya RAM nayo ile ddr 4 ni shingapi? Maana kunajamaa alinipiga kabisa.
8GB naona jiji wanauza 90,000 sijui madukani, sasa hivi ddr5 zimetoka ddr4 zinashuka.

Aliexpress around 50,000 kwa ddr4 nzuri za 3200mhz za 8gb
 
8GB naona jiji wanauza 90,000 sijui madukani, sasa hivi ddr5 zimetoka ddr4 zinashuka.

Aliexpress around 50,000 kwa ddr4 nzuri za 3200mhz za 8gb
Asante mkuu pc yangu saiv inanisumbua na hii kitu sijui kwann kabla hata sijaweka hiyo Ram naona inaniletea shida dah! [emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]
images%20(5).jpg
 
Asante mkuu pc yangu saiv inanisumbua na hii kitu sijui kwann kabla hata sijaweka hiyo Ram naona inaniletea shida dah! [emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]View attachment 2717491
Hio ni bsod mkuu, huwa haina sababu maalum, mwanzo wakati unainunua haikua hivi? Hivi karibuni huja update windows? Sometime kuweka vitu up to date inasaidia pia.
 
Hio ni bsod mkuu, huwa haina sababu maalum, mwanzo wakati unainunua haikua hivi? Hivi karibuni huja update windows? Sometime kuweka vitu up to date inasaidia pia.
Sawa mkuu maana kunasiku niliipiga Window na kui update lakn iliniletea hv, Nikapiga tena na saiv inakuwa pia inaleta hv hata kama niki update mkuu
 
Computer nyingi tunazonunua huwa zinatumia processor za intel au amd, lakini ni intel ambaye ametawala sana kushinda amd kwenye computer zetu. Leo nimeamua niandike uzi huu kuhusu hizi processor za intel na namna ya kuzichagua ili kuwasaidia watu wanapotaka kununua laptop/desktop mpya wafanye maamuzi sahihi.

Processor ni nini?

Labda utakuwa unajiuliza kwa nini ukitaka kununua laptop mpya unatakiwa uangalie processor? Nini cha muhimu kuhusu hii processor?

-Kwa lugha rahisi processor ni kifaa ndani ya computer yako kinachobeba maagizo ya program za computer. Maagizo hayo yanaweza kuwa ya kimahesabu, kimantiki, maagizo yanayoingia kwenye computer na yanayotoka.

-jinsi processor inavyokuwa na speed kubwa ndio jinsi maagizo yatakavyofanywa haraka na ndio jinsi program za computer zitakavyofanya kazi upesi.
processor_01.jpg


Familia ya processor za intel

Intel wana processor za aina nyingi na ni ngumu kuzitaja kwa pamoja, ila wameturahisishia kwa kuzipanga processor zao kwenye familia. Na hii ndio familia yao.

1. Atom processor- processor hizi hutumika kwenye vimini laptop na tablet ni ndogo kiumbo ndio maana hata vifaa vyake ni vidogo, processor hizi hazina nguvu sana na vifaa vyake hukaa sana na chaji.

2. Celeron processor- Haina tofauti sana na atom ila hii ina afadhali kidogo. Inatumika kwenye vifaa vikubwa kuliko atom kama vile laptop kubwa na desktop

3. Pentium- hii ina speed kuliko celeron na atom pia inatumika kwenye vifaa vikubwa.

4. Core 2 duo- hii ni maarufu kwa perfomance yake ya multitasking, inauwezo wakufanya mambo mengi kwa wakati mmoja ila nyingi ni za kizamani.

5. Core i3- hii ni processor latest za intel ni dual core lakini core zake zina perfomance kubwa na pia inakuwa na thread 2 kwenye kila core, ni nzuri kwa wanaotaka perfomance kubwa kwa bei rahisi.

6. Core i5- ya laptop ni dualcore na ya desktop ni quadcore isiyokuwa na thread, software nyingi kubwa duniani zimekuwa optimized kutumia core kama za i5, ni nzuri sana kwa watu wanaotumia software zinazodemand perfomance lakini hawafanyi multitasking.

7.Core i7- hii inakuwa na quadcore processor na thread 8 kwenye desktop na pia inaweza kuwa dualcore kwenye laptop. Hii ndio processor nzuri zaidi kwa watu wa kawaida na inafanya multitasking hata kama software zinademand sana.

8. Xeon- hii ndio processor yenye speed zaidi kwenye processor za intel lakini imekuwa designed kufanya kazi kwenye computer kubwa kama vile server. Unapohost website processor kama hii ndio inayoprocess webpages.


Generation ya processor(muhimu)

Ni muhimu sana kujua processor inatokea generation ipi kuna processor zenye i7 ya 2010 ambazo zipo slow vibaya mno, na pia kuna uwezekano i3 kuipita i7 kwenye perfomance kama zinatoka generation tofauti. Hivyo eneo hili inabidi uwe makini kuepuka kuuziwa mbuzi kwenye gunia. Hivyo unaponunua laptop/desktop ni lazima ujue ipo generation gani la sivyo upo hatarini na hivi ndio namna ya kujua.

- Processor yenye namba inayoanziwa na elfu nne ni fourth generation(4xxx)
Mfano Intel i3-4130.

- Processor yenye namba inayoanziwa na elfu tatu ni third generation (3xxx)
Mfano i3-3130.

- Processor inayoanziwa na elfu mbili ni second generation(2xxx)
Mfano i3-2140

Sishauri kabisa kununua processor ya first generation, mtu unatakiwa atleast ununue ya second generation na pia bei inatakiwa iwe ndogo kwa hii second compare na third/fourth.

Processor ndogo kama atom na celeron zina generation zake ambazo ni
-clover trail
-bay trail

Processor za zamani za atom zilikuwa mbaya sana na zipo slow ila baytrail ikaja kuzipa nguvu na kuzifanya ziwe na perfomance kubwa, hivyo kama unataka kifaa cha atom/celeron make sure processor yake iwe inatoka generation ya baytrail.


Herufi za mbele ya processor(muhimu)

Kama umechunguza mbele ya processor kunakuwa na herufi mbali mbali hizi pia ni muhimu sana kuzijua kwani usipozizingatia unaweza kujuta.

Mfano processor inaweza kuitwa i5-4000m au i5-4000u au i5-4000y je nini kinatofautisha hizi processor?

1. Herufi kwenye processor za desktop.

Bila herufi – hii inakuwa na speed halisi ya processor mfano i7-4770

K- herufi hii inamaanisha processor ipo unlocked na unaweza kui over clock na kuongeza speeed. Processor yenye 3.5ghz unaweza kui overclock ikafika 4ghz. Jina lake linakuwa mfumo huu i7-4770K. ni nzuri sana kwa wanaocheza magame na kufanya rendering.

R- herufi hii inamaanisha processor hii ni ndogo sana na inaweza kutumika kwenye videsktop vyenye umbo dogo hali ya kuwa ina graphic kubwa kama iris pro. Jina lake linakuwa mfumo huu i7-4770R hii ni nzuri kwa wale wenye ofisi ambazo ni safi hawataki mawaya mengi na desktop kubwa kukaa kwenye meza. angalia picha hapo chini uone desktop ndogo.

brix1_s.gif


S- herufi hii inamaanisha hiyo proceesor wame optimize perfomance mara nyingi wanai underclock kuzuia processor kupata joto sana. Mfano i7-4770 ina 3.4ghz lakini i7-4770S ina 3.1ghz tu, ina maana hapa wamepunguza 300mhz kutoka stock kuja S.

T- herufi hii inamaanisha processor inatumia power ndogo, kwa wale wenzangu wanaotumia luku kama unataka desktop isiokula umeme basi hii ndio yenyewe ila perfomance nayo itapungua kidogo. Mfano wa jina ni i7-4770T

2. Herufi mbele ya processor za laptop(mobile)

Tumeshaona herufi mbele ya desktop, sasa hivi tuangalie herufi mbele ya processor za laptop ambazo pia zinaweza kutumika kwenye home theatre pc (htpc) au wengine wanaita mini desktop.

M- herufi hii inamaanisha hio processor ni mobile, ndio herufi common kwenye processor za laptop mfano i5-4000M

U- herufi hii inamaanisha processor ya laptop inatumia power ndogo hizi processor zinatumika sana kwenye vilaptop vyembamba (ultrabook). Kwa sababu zinakaa na chaji kutokana na kutumia power ndogo, perfomance yake nayo pia ni ndogo. Mfano i5 4250U

Y- hii ni ultra low power yaani inakula umeme mdogo kushinda hata U lakini vile vile perfomance inazidi kushuka nayo mfano i7-4610Y

HQ- herufi hii inamaanisha high perfomance, zinauzwa bei ghali sana na power yake inashindana na desktop. Usije ukajaribu kuieka kwenye mapaja laptop ya design hii maana zinashika moto upesi sana kutokana na quality ya processor. Ni nzuri kwa wale wanaopenda kucheza game, kutumia software kubwa wakiwa kitandani. Mfano ni i7-4700HQ

MQ- herufi hii inamaanisha hio procesor ni quad core. Kama umesoma vizuri juu i5 na i7 za desktop ni quadcore lakini za laptop ni dualcore, hivi processor hii inamaanisha unaweza tumia quadcore kwenye laptop yako kama unataka mfano i7-4900MQ

MX- herufi hii inamaanisha ni xtreme edition, processor hii unaweza kui over clock kama vile K series ya desktop na ina perfomance kubwa sanaaa, ila kuwa makini na mapaja tu.
Mfano i7-4940MX

Huu ndio muongozo wa kununua processor za intel, kama kuna sehemu hujapaelewa unaweza kuuliza nitaelezea zaidi.
Nina ku bookmark Mwalimu wa maana sana wewe, nininyi ndiyo tunawataka humu siyo wale wa kula tunda kimasihara
 
Back
Top Bottom