Muosha Magari apatisha ajali gari lenye thamani zaidi ya Milioni 100. Akutwa anaruka sarakasi


Ww unadhani hata kama ina bima kubwa kampuni ya bima italipa??? unless muosha magari awe na leseni na pia asiwe mlevi na Ripoti ya police iandikwe vizuri
 
Mkuu kwa uelewa wangu kuhusu hiyo gari ni kwamba aliyepeleka kuosha naye sio yake, aliyeiodondosha naye ni mwingine, yaani kuna shida balaa.
Mkuu sjakuelewa hapo aliyeidondosha si kijana wa car wash ambae kwenye picture anaonekana kifua wazi ?
 
Mkuu mambo ya bima sio rahisi hivyo kama unavyofikiria tena iwe ile bima kubwa ndio balaa kabisa , gari ikipata ajari hata kama unaendesha mwenyewe kama leseni yako ni chini ya miaka mitatu tangu uipate, kuna asilimia wanakata kwenye fidia, sasa kama kwa huyo ambaye huenda hata leseni hana ni mtihani mkubwa mno kwa mwenye gari
 
Hivi ujaona tofauti tu hapo(private use) hiyo ni gari kwa matumizi binafsi na hayo mabasi na daladala ni kwa matumizi ya biashara (commercial use). Ktk Bima kunakuwaga na risk assessment.. it's obvious magari ya biashara risk ni kubwa zaidi na uzingatiwaji kwamba yanaendeshwa na madereva tofauti pasi na mmiliki halali so ata rate za ukokotoaji ni tofauti na private, kwa muktadha huo sioni room ya kulipwa hyo mmiliki wa gari
 
Ukisikia mitihan dunian ndo kama hii Sasa Sasa muosha magari atatoa wap hela ya ford ranger million 120 jamaa inabidi asamehe tu maana hata akimfunga haisaidii bado.

NB:
Hata mimi ningejifanya kichaaaa[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
🥲 🥲 🥲
 
Hapo inabidi ucheze nao akili hao bima na pia utembeze mlungula kwa mtu kisha mnacheza mchezo wakupatie Cash ndio furaha iliyopo hapo kwa mwenye gari
 
wengi hawana huo muda wa kufanya ivyo,Ukifanya ivyo na riziki za vijana unazipunguza
 
Umemjibu vyema yeye mzee wake ndo kamwambia hivyoo. Alimwambia hivyoo maana anajua mtoto wake Hamna kitu anajua zaidi ya kuangalia tamthilia za kifipino na kuvaa suruale zilizo chanika chanika.
Chuma cha mjerumani ninyi watu ni wakorofi sana aisee majibu yenu huwa nacheka na sasa hivi inabidi niwe nasoma JF nikiwa mazingira huru ya kucheka...
 
Wabongo bhana wapo watu hizo ford ranger kuzipata ni kama sisi kununua ist ajali tu mnazungumzia kazurumu mbona ist zinapata ajali hamzungumzii kuzurumu wapo wahuni maisha yamenyooka wanarafuta matumizi tuu endeleeni kuona kila aliefanikiwa kazurumu...
 
Umetia chumvi. Bima haijawahi kumnunulia mtu gari, baada ya assessment kufanyika na technical opinion kutolewa kuwa gari ipo beyond economical repair na au thamani ya matengenezo ni zaidi ya 75% ya thamani gari bima wanakulipa fedha inayolingana na thamani ya gari kabla ya ajali.

Kama gari inaweza kutengenezwa, si lazima kampuni ya bima kukuchagulia garage. Mteja anaweza kuchagua garage anayoona inafaa.

Vijana msiwe mnapenda habari za vijiweni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…