Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu kama nitakuwa sahihi hiyo gari sio ya mtu. Ni gari Ofisi X ya umma.Haya ndio madhara ya kupata mali kwa njia ambazo zina mazonge
Habari wakuu, tunakumbushana kuweni makini na waosha magari mnapowaachia funguo wakati wa kuosha dinga zenu, Jamaa kapeleka gari aina ya Ford Ranger carwash huku Dom kaacha funguo na kuondoka, mwoshaji kamaliza akachukua ford ranger ya Mteja kwenda kutamba nalo, kilichotokea kala mzinga ndinga haitamaniki yeye kapata uchizi wa ghafla.
View attachment 1877570View attachment 1877572
View attachment 1877571
Huyu jamaa mwenye kibukta ndo mwoshaji, hiyo video ndo inaonyesha kichaa cha ghafla alichopata, sipati picha mmiliki ana hali gani hiki ndo ukute alikuwa na third party tu.
View attachment 1878612
Mkuu kwa uelewa wangu kuhusu hiyo gari ni kwamba aliyepeleka kuosha naye sio yake, aliyeiodondosha naye ni mwingine, yaani kuna shida balaa.Mzee et wewe ungefanya nini hapo KWA haraka haraka
Mkuu sjakuelewa hapo aliyeidondosha si kijana wa car wash ambae kwenye picture anaonekana kifua wazi ?Mkuu kwa uelewa wangu kuhusu hiyo gari ni kwamba aliyepeleka kuosha naye sio yake, aliyeiodondosha naye ni mwingine, yaani kuna shida balaa.
Mkuu mambo ya bima sio rahisi hivyo kama unavyofikiria tena iwe ile bima kubwa ndio balaa kabisa , gari ikipata ajari hata kama unaendesha mwenyewe kama leseni yako ni chini ya miaka mitatu tangu uipate, kuna asilimia wanakata kwenye fidia, sasa kama kwa huyo ambaye huenda hata leseni hana ni mtihani mkubwa mno kwa mwenye gariUna idea yoyote labda kuhusu masuala ya bima?
Nikusema buses zote za mikoani,daladala kwenye miji mbalimbali hapa home gari zote zinazoendeshwa mijini huwa zinaendeshwa na wamiliki?sasa kumbe kuna haja gani kukata bima hali yakuwa haitoi msaada chombo kikipata tatizo kikiwa nje ya mikono yako?...hey mimi nakushauri kitu hujui kukaa kimya siyo dhambi.
Hivi ujaona tofauti tu hapo(private use) hiyo ni gari kwa matumizi binafsi na hayo mabasi na daladala ni kwa matumizi ya biashara (commercial use). Ktk Bima kunakuwaga na risk assessment.. it's obvious magari ya biashara risk ni kubwa zaidi na uzingatiwaji kwamba yanaendeshwa na madereva tofauti pasi na mmiliki halali so ata rate za ukokotoaji ni tofauti na private, kwa muktadha huo sioni room ya kulipwa hyo mmiliki wa gariUna idea yoyote labda kuhusu masuala ya bima?
Nikusema buses zote za mikoani,daladala kwenye miji mbalimbali hapa home gari zote zinazoendeshwa mijini huwa zinaendeshwa na wamiliki?sasa kumbe kuna haja gani kukata bima hali yakuwa haitoi msaada chombo kikipata tatizo kikiwa nje ya mikono yako?...hey mimi nakushauri kitu hujui kukaa kimya siyo dhambi.
🥲 🥲 🥲Ukisikia mitihan dunian ndo kama hii Sasa Sasa muosha magari atatoa wap hela ya ford ranger million 120 jamaa inabidi asamehe tu maana hata akimfunga haisaidii bado.
NB:
Hata mimi ningejifanya kichaaaa[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Nami niliwaza kuuliza swali kama hiliKama Habari isingekuwa maarufu mmiliki angekuja akakamata usukani na kujidai yeye ndo kapata ajali. Bima ikaanza kama ni kubwa
Hapo inabidi ucheze nao akili hao bima na pia utembeze mlungula kwa mtu kisha mnacheza mchezo wakupatie Cash ndio furaha iliyopo hapo kwa mwenye garihio comprehensive insurance wabongo wachache wanayo wngi wanatumia tu hizi third party za laki 1, huwa zinahusisha tu watu au mali za watu utaowasababishia madhara mfano kugonga mtu au wanyama au gari,
Ila ikitokea ana comprehensive income, bado sughuli ni pevu maana kuna mibadala mitatu tofauti na watu wanavyodhani .
1. kufanyiwa marekebisho, watapeleka gari likanyoshwe kwenye gereji wanazozijua wao, kwa hii ford wanaweza kuipeleka kenya ikarudi ipo fresh.
2. kununuliwa gari kama iliyopata ajali, hapa wanaweza kukununulia gari huko be forward, tena kwa mile age na uchakavu unaoendana na gari kabla halijapata ajali.
3. kupewa cash uwende kununua gari mwenyewe, hapa huwainatokea kama wamekosa fundi wa kurekebisha au wamekosa gari za mtumba huko be forward 😂
Hapo watakomaa kuipeleka gereji ikanyooshwe tu, hawana pesa za mchezo kukununulia nyingine ama kukupa cash, Bongo Nyoso!!
Hatarious[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Aaah we!! Hapo hata ukoo wangu wote ujichangishe hiyo hela haipatikani. Hivyo bora niende mirembe kiroho safi.
Mwamba ufalme wa mungu utausikia redioni sio mbinguniComprehensive insurance wakati dereva hana leseni,kama Mimi ndio mwenye gari tunaingia mkataba wa kumtatua marinda kwa muda usiojulikana mpaka adebedwe kama akina James Delicious
wengi hawana huo muda wa kufanya ivyo,Ukifanya ivyo na riziki za vijana unazipunguzaKama wamiliki gari ya zaidi ya shilingi 100milioni kwanini usinunue ka- jetwash kako mwenyewe na vifaa vya kuoshea bei rahisi kabisa.
Waosha Jumamosi au Jumapili nyumbani kwako?
Gari la milioni 100 huwezi tu kumpatia mwosha magari wa mitaani aoshe na umpe funguo juu, huo ni ujinga.
Lazima ufahamu anatumia maji yepi, sabuni ya aina gani? na hata fagio ni zipi atumia kufagia ndani ya gari.
Ila haingiii akilini kwenda kulikabidhi gari kama hilo kwa mtu baki ambae huna uhakika na taarifa zake.
Chuma cha mjerumani ninyi watu ni wakorofi sana aisee majibu yenu huwa nacheka na sasa hivi inabidi niwe nasoma JF nikiwa mazingira huru ya kucheka...Umemjibu vyema yeye mzee wake ndo kamwambia hivyoo. Alimwambia hivyoo maana anajua mtoto wake Hamna kitu anajua zaidi ya kuangalia tamthilia za kifipino na kuvaa suruale zilizo chanika chanika.
Unaujua uvivu wa kuosha gar mwenuewe ndugu yanguHoja nzuri hii. Mwenye sikio na asikie
Umetia chumvi. Bima haijawahi kumnunulia mtu gari, baada ya assessment kufanyika na technical opinion kutolewa kuwa gari ipo beyond economical repair na au thamani ya matengenezo ni zaidi ya 75% ya thamani gari bima wanakulipa fedha inayolingana na thamani ya gari kabla ya ajali.hio comprehensive insurance wabongo wachache wanayo wngi wanatumia tu hizi third party za laki 1, huwa zinahusisha tu watu au mali za watu utaowasababishia madhara mfano kugonga mtu au wanyama au gari,
Ila ikitokea ana comprehensive income, bado sughuli ni pevu maana kuna mibadala mitatu tofauti na watu wanavyodhani .
1. kufanyiwa marekebisho, watapeleka gari likanyoshwe kwenye gereji wanazozijua wao, kwa hii ford wanaweza kuipeleka kenya ikarudi ipo fresh.
2. kununuliwa gari kama iliyopata ajali, hapa wanaweza kukununulia gari huko be forward, tena kwa mile age na uchakavu unaoendana na gari kabla halijapata ajali.
3. kupewa cash uwende kununua gari mwenyewe, hapa huwainatokea kama wamekosa fundi wa kurekebisha au wamekosa gari za mtumba huko be forward 😂
Hapo watakomaa kuipeleka gereji ikanyooshwe tu, hawana pesa za mchezo kukununulia nyingine ama kukupa cash, Bongo Nyoso!!
Hii nayo sio mbaya kama anataka kuwepa kupumuliwa kisogonisio akauze figo mkuu pale Regency hospital kwa madoni aje alipe deni