Muosha Magari apatisha ajali gari lenye thamani zaidi ya Milioni 100. Akutwa anaruka sarakasi

Muosha Magari apatisha ajali gari lenye thamani zaidi ya Milioni 100. Akutwa anaruka sarakasi

Habari wakuu, tunakumbushana kuweni makini na waosha magari mnapowaachia funguo wakati wa kuosha dinga zenu, Jamaa kapeleka gari aina ya Ford Ranger carwash huku Dom kaacha funguo na kuondoka, mwoshaji kamaliza akachukua ford ranger ya Mteja kwenda kutamba nalo, kilichotokea kala mzinga ndinga haitamaniki yeye kapata uchizi wa ghafla.

View attachment 1877570View attachment 1877572
View attachment 1877571
Huyu jamaa mwenye kibukta ndo mwoshaji, hiyo video ndo inaonyesha kichaa cha ghafla alichopata, sipati picha mmiliki ana hali gani hiki ndo ukute alikuwa na third party tu.

View attachment 1878612

Ww unadhani hata kama ina bima kubwa kampuni ya bima italipa??? unless muosha magari awe na leseni na pia asiwe mlevi na Ripoti ya police iandikwe vizuri
 
Mkuu kwa uelewa wangu kuhusu hiyo gari ni kwamba aliyepeleka kuosha naye sio yake, aliyeiodondosha naye ni mwingine, yaani kuna shida balaa.
Mkuu sjakuelewa hapo aliyeidondosha si kijana wa car wash ambae kwenye picture anaonekana kifua wazi ?
 
Una idea yoyote labda kuhusu masuala ya bima?

Nikusema buses zote za mikoani,daladala kwenye miji mbalimbali hapa home gari zote zinazoendeshwa mijini huwa zinaendeshwa na wamiliki?sasa kumbe kuna haja gani kukata bima hali yakuwa haitoi msaada chombo kikipata tatizo kikiwa nje ya mikono yako?...hey mimi nakushauri kitu hujui kukaa kimya siyo dhambi.
Mkuu mambo ya bima sio rahisi hivyo kama unavyofikiria tena iwe ile bima kubwa ndio balaa kabisa , gari ikipata ajari hata kama unaendesha mwenyewe kama leseni yako ni chini ya miaka mitatu tangu uipate, kuna asilimia wanakata kwenye fidia, sasa kama kwa huyo ambaye huenda hata leseni hana ni mtihani mkubwa mno kwa mwenye gari
 
Una idea yoyote labda kuhusu masuala ya bima?

Nikusema buses zote za mikoani,daladala kwenye miji mbalimbali hapa home gari zote zinazoendeshwa mijini huwa zinaendeshwa na wamiliki?sasa kumbe kuna haja gani kukata bima hali yakuwa haitoi msaada chombo kikipata tatizo kikiwa nje ya mikono yako?...hey mimi nakushauri kitu hujui kukaa kimya siyo dhambi.
Hivi ujaona tofauti tu hapo(private use) hiyo ni gari kwa matumizi binafsi na hayo mabasi na daladala ni kwa matumizi ya biashara (commercial use). Ktk Bima kunakuwaga na risk assessment.. it's obvious magari ya biashara risk ni kubwa zaidi na uzingatiwaji kwamba yanaendeshwa na madereva tofauti pasi na mmiliki halali so ata rate za ukokotoaji ni tofauti na private, kwa muktadha huo sioni room ya kulipwa hyo mmiliki wa gari
 
Ukisikia mitihan dunian ndo kama hii Sasa Sasa muosha magari atatoa wap hela ya ford ranger million 120 jamaa inabidi asamehe tu maana hata akimfunga haisaidii bado.

NB:
Hata mimi ningejifanya kichaaaa[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
🥲 🥲 🥲
 
hio comprehensive insurance wabongo wachache wanayo wngi wanatumia tu hizi third party za laki 1, huwa zinahusisha tu watu au mali za watu utaowasababishia madhara mfano kugonga mtu au wanyama au gari,

Ila ikitokea ana comprehensive income, bado sughuli ni pevu maana kuna mibadala mitatu tofauti na watu wanavyodhani .

1. kufanyiwa marekebisho, watapeleka gari likanyoshwe kwenye gereji wanazozijua wao, kwa hii ford wanaweza kuipeleka kenya ikarudi ipo fresh.

2. kununuliwa gari kama iliyopata ajali, hapa wanaweza kukununulia gari huko be forward, tena kwa mile age na uchakavu unaoendana na gari kabla halijapata ajali.

3. kupewa cash uwende kununua gari mwenyewe, hapa huwainatokea kama wamekosa fundi wa kurekebisha au wamekosa gari za mtumba huko be forward 😂

Hapo watakomaa kuipeleka gereji ikanyooshwe tu, hawana pesa za mchezo kukununulia nyingine ama kukupa cash, Bongo Nyoso!!
Hapo inabidi ucheze nao akili hao bima na pia utembeze mlungula kwa mtu kisha mnacheza mchezo wakupatie Cash ndio furaha iliyopo hapo kwa mwenye gari
 
Kama wamiliki gari ya zaidi ya shilingi 100milioni kwanini usinunue ka- jetwash kako mwenyewe na vifaa vya kuoshea bei rahisi kabisa.

Waosha Jumamosi au Jumapili nyumbani kwako?

Gari la milioni 100 huwezi tu kumpatia mwosha magari wa mitaani aoshe na umpe funguo juu, huo ni ujinga.

Lazima ufahamu anatumia maji yepi, sabuni ya aina gani? na hata fagio ni zipi atumia kufagia ndani ya gari.

Ila haingiii akilini kwenda kulikabidhi gari kama hilo kwa mtu baki ambae huna uhakika na taarifa zake.
wengi hawana huo muda wa kufanya ivyo,Ukifanya ivyo na riziki za vijana unazipunguza
 
Umemjibu vyema yeye mzee wake ndo kamwambia hivyoo. Alimwambia hivyoo maana anajua mtoto wake Hamna kitu anajua zaidi ya kuangalia tamthilia za kifipino na kuvaa suruale zilizo chanika chanika.
Chuma cha mjerumani ninyi watu ni wakorofi sana aisee majibu yenu huwa nacheka na sasa hivi inabidi niwe nasoma JF nikiwa mazingira huru ya kucheka...
 
Wabongo bhana wapo watu hizo ford ranger kuzipata ni kama sisi kununua ist ajali tu mnazungumzia kazurumu mbona ist zinapata ajali hamzungumzii kuzurumu wapo wahuni maisha yamenyooka wanarafuta matumizi tuu endeleeni kuona kila aliefanikiwa kazurumu...
 
hio comprehensive insurance wabongo wachache wanayo wngi wanatumia tu hizi third party za laki 1, huwa zinahusisha tu watu au mali za watu utaowasababishia madhara mfano kugonga mtu au wanyama au gari,

Ila ikitokea ana comprehensive income, bado sughuli ni pevu maana kuna mibadala mitatu tofauti na watu wanavyodhani .

1. kufanyiwa marekebisho, watapeleka gari likanyoshwe kwenye gereji wanazozijua wao, kwa hii ford wanaweza kuipeleka kenya ikarudi ipo fresh.

2. kununuliwa gari kama iliyopata ajali, hapa wanaweza kukununulia gari huko be forward, tena kwa mile age na uchakavu unaoendana na gari kabla halijapata ajali.

3. kupewa cash uwende kununua gari mwenyewe, hapa huwainatokea kama wamekosa fundi wa kurekebisha au wamekosa gari za mtumba huko be forward 😂

Hapo watakomaa kuipeleka gereji ikanyooshwe tu, hawana pesa za mchezo kukununulia nyingine ama kukupa cash, Bongo Nyoso!!
Umetia chumvi. Bima haijawahi kumnunulia mtu gari, baada ya assessment kufanyika na technical opinion kutolewa kuwa gari ipo beyond economical repair na au thamani ya matengenezo ni zaidi ya 75% ya thamani gari bima wanakulipa fedha inayolingana na thamani ya gari kabla ya ajali.

Kama gari inaweza kutengenezwa, si lazima kampuni ya bima kukuchagulia garage. Mteja anaweza kuchagua garage anayoona inafaa.

Vijana msiwe mnapenda habari za vijiweni.
 
Back
Top Bottom