Muosha Magari apatisha ajali gari lenye thamani zaidi ya Milioni 100. Akutwa anaruka sarakasi

Muosha Magari apatisha ajali gari lenye thamani zaidi ya Milioni 100. Akutwa anaruka sarakasi

ndio matokeo ya kuosha gari vichochoroni...
lazima ukutane na wahuni
Mkuu, zikifika zimefika tu, hata angeosha wapi. Kuna yule dereva wa RC mara alipark gari home kwake the next thing mwanae akapita nalo
Mimi mzee wangu ameshapigwa sana vitu ndani ya gari kuanzia garage mpaka kwa waosha magari mpaka akaacha kuosha car wash

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ngoja niwape story yangu, Mimi niliazima tayota ist kwa rafiki yangu ili niwahi safari nioliokuwa naiendea, baada kupewa Gari Safi kabisa bado mpya Ina week mbili nikanyoosha goti vizuri safari yangu nikaenda maana ilikuwa mkoa Hadi mkoa mwingine.

Wakati narudi kutoka safari yangu nikiwa njiani nipo kwa road la vumbi na speed ya 70 hivi ghafla Ng'ombe mbele yangu anakatiza Barabara nilitupia mgu kwa brake Gari ikakubali lakini ikaenda pembeni kidogo, bwana we sijui ibilisi gani kanijaa nikajikuta nimetupia mguu kwenye Moto tena la haula Gari iliruka na kuzunguka Kama Mara 4 hivi ikatulia ndugu yangu natoka pale Sina hili Wala lile nikaangalia huku na kule hakuna mtu kucheki Gari ya mtu imeisha yaani.

Nilichomoka mbio hizo alafu sijui naenda wapi na Sina mpangilio wowote kichwani nakuja kusimama najishangaa kwanza Sasa naenda wapi alafu nimeacha kila kitu kwenye gari na documents muhimu ambazo hatakiwi mtu kuziona looh nikarudi Tena speed nikafika nikakunja doc zangu kwanza nikavua vyatu nikaanza kutembea peku nilikuwa nimefunga tai aisee


Itaendeleaa.............[emoji22][emoji22][emoji22][emoji22][emoji22]
[emoji28][emoji28][emoji28]
 
Sasa mkuu bima ndogo itamlipaje. Jifunze kuhusu third party liability.
Kingine, ukiwa na bima kubwa (comprehensive) unalipwa hata kama aliyeendesha babu yako. Huyo Mtu wa bima ama ni kilaza au aliamua kusema hivyo ili msimsumbue
Ndugu usiwe mbishi bima inategemea vitu vingi. Sio universal Kama unavyotka wewe. Bima ni mkataba.. je mkataba unasemajee?? All in all hkna excuse kma leseni hkna ninavyujua. Tuendelee kuelimishana
 
Wengi naona wanasema wanasema gari haina bima ila inayo tena bima kubwa kupitia system mpya ya tiramis unaiona fresh imekatwa kampuni ya UAP.
Changamoto kubwa nayo iona ni dogo kutokuwa na leseni hii itamkosesha mwenye gari malipo.

View attachment 1878916
Nilikuwa nashangaa wanaosema gari haina bima. Kuna link ya zamani ukiingia utaona gari haina bima Ila hii ndio huwa ipo accurate.

Ishu iliyobaki ni kama dogo alikuwa na leseni.
 
Ukisikia mitihan dunian ndo kama hii Sasa Sasa muosha magari atatoa wap hela ya ford ranger million 120 jamaa inabidi asamehe tu maana hata akimfunga haisaidii bado.

NB:
Hata mimi ningejifanya kichaaaa[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Bora afungwe ili akitoka awe na heshima na Mali za watu,
Tena kama kuna mashamba yao ya urithi pia yauzwe ,hili walipie nusu hasara

Sent from my Infinix X623 using JamiiForums mobile app
 
muhimu bima hata awe huyo boss utamkuta anaruka sarakasi kama huyo dogo
sidhani kama bima watalipa ...huu ni uzembe wa mwenye gari,

mchongo wa chini ya meza ni kucheza na polisi - wafanyakazi wa bima (hasa manager) kisha kupika taarifa --- hapa mgao yabidi uwe pasu kwa pasu
 
Sio anajifanyisha kweli? 🤔

Hapo ni kumchukulia hatua mengine kama anayo yatajulikana Hospitali.
 
Halafu huku kwetu madongo kuinama mbona hao waoshaji kama siku unataka akusafishie ndani huwa wanasemaga uache wazi gari kisha funguo usepe nazo halafu wao wanalock gari kwa kile kidude cha kulock na ku unlock milango au hii ipo kwetu sisi tunaomiliki vibajaji. Teh.

Hivyo anakosha akimaliza gari anaifunga na hii inafanyika kwa yule muoshaji aliyezoeleka miaka nenda rudi kama hayupo basi aliyepo ataosha nje inatosha.
 
Back
Top Bottom