Murtaza Mangungu: Kiongozi pekee anayeweza kuipa ubingwa wa Africa timu ya Simba

Murtaza Mangungu: Kiongozi pekee anayeweza kuipa ubingwa wa Africa timu ya Simba

Mcheza Piano

JF-Expert Member
Joined
Mar 2, 2024
Posts
562
Reaction score
1,339
Achana na porojo za vikundi vinavyo hongwa na watu wenye nia mbaya ili kumhujumu ndugu Murtaza Mangungu (genius wa msimbazi), leo nataka kukumegea siri makini sana.

Ni hivi, ndugu Murtaza Mangungu ni kiongozi makini anayesimamia katiba na sheria ndiyomaana mpaka sasa hajajiingiza kwenye sarakasi za hovyo zinazo endelea pale msimbazi.

Amesema wazi kuwa hawezi kujiuzulu bila kujua kosa lake maana yupo pale kwa matakwa ya katiba ya Simba sio kwa matakwa ya ma popoma kama GENTAMYCINE .

Pili amesema kuwa yuko tayari kutoa fedha zake mfukoni na kupitisha bakuli kwa mashabiki, wapenzi na wanachama wa Simba ili kufanya usajili makini kwaajili ya msimu ujao.

Kwa maneno mengine, Murtaza hataki kulamba viatu vya mwekezaji kisa tu mwekezaji ana fedha. Murtaza anajua kuwa mwekezaji anapata faida na kama hayuko tayari kutumia sehemu ya faida yake kufanya usajili basi asepe watakuja wawekezaji wengine.

Hakika Murtaza ndiyo tumaini letu pekee na yeye ndiye anayeshikilia maslahi ya timu yetu na amesimama imara kuzuia uporaji wa hii timu unaotaka kufanywa na wahuni.

Ikumbukwe kuwa huyu anayetaka kuipora timu yetu, anatuhumiwa kupora mashamba ya serikali kwa kujifanya kuwa mwekezaji anayetaka kuendeleza mashamba hayo baada ya kupewa ametumia hati zake kuchukua mikopo ambayo ameitumia kwa maslahi yake binafsi na serikali imempa muda kutoa maelezo yaliyo nyooka kabla hajashushiwa rungu zito.

Murtaza analifahamu vyema hili sakata na anataka kutusaidia wanasimba kuzuia ujangili kama huu kufanyika pale simba.

Hongera sana Murtaza, kwasasa utatukanwa na kudhihakiwa na mashabiki maandazi, ila mwakani hao hao watakuja hapa kukumwagia sifa. Tafadhali kaza buti, shikilia hapo hapo.
 
Nadhani atawafaa yanga sisi hatumtaki
GP5GyvAXUAA4d4-.jpeg
 
Mkuu hiyo ID yako mbona inafanya uzi uwe wa mashaka mashaka na yale usemayo?
 
Nadhani atawafaa yanga sisi hatumtakiView attachment 3017944
Hamumtaki kivipi, na wakati mlimchagua wenyewe kuwa mwenyekiti wenu?

Au unataka kusema lile pilau alilowalisha siku ile ya uchaguzi, pamoja na ule ujio wa Manzoki kutoka China viliwachanganya na kujikuta mnampiga kura mgombea ambaye hakuwa chaguo lenu?
 
Hamumtaki kivipi, na wakati mlimchagua wenyewe kuwa mwenyekiti wenu?

Au unataka kusema lile pilau alilowalisha siku ile ya uchaguzi, pamoja na ule ujio wa Manzoki kutoka China viliwachanganya na kujikuta mnampiga kura mgombea ambaye hakuwa chaguo
Uyo alipita kwa goal la mkono
 
Hamumtaki kivipi, na wakati mlimchagua wenyewe kuwa mwenyekiti wenu?

Au unataka kusema lile pilau alilowalisha siku ile ya uchaguzi, pamoja na ule ujio wa Manzoki kutoka China viliwachanganya na kujikuta mnampiga kura mgombea ambaye hakuwa chaguo lenu?
Mangungu anatosha
 
Back
Top Bottom