Hakuna Kodi nyepesi kulipika. Umeongea kwa hisia Kari kiasi kidogo unishawishi.
Kuna watu hawatumi ,pesa wao nikupokea TU nao wanalalamikia tozo. Hii sio sawa.
Hata huko Bank 🏧 Nako Tozo ilifika.
Japo ninteja wa bank lakini kipato change ni chakawaida.
Na Bank hakuna njia ya mkato. Huku kwenye mitandao walio wengi walisha buni mbinu ya kukimbia Tozo. Ambapo mbinu hizo zililenga KUSAIDIA hayo makundi unayo taja .
Nikituma kwa mwanafunzi na pewa lipa namba. Nikituma kwa mgonjwa hivyohivyo. Je wewe hii hukuijua?
Kwani waliopita waliendesha je nchi au serikali bila tozo?Duniani hakuna hiki kituko unachoandika hapa. Haina tofauti na Kodi ya kichwa. Ni upuuzi m.tupu
Tuwaulize waliomweka Nia yao ilikuwa ni Nini? Kama ni kisimamia mapato na kumshauri Rais bila kubughudhi raia watajua wenyewe.
Kama ni michango mchangiaji akubali sio alazimishwe. Akitaka kufanya kitu halafu kwa malipo ya mtandao nyinyi mnakata, hata Kama anatoa msaada. Huu tunasema ni ushetani kabisa. Ni Kama mtu anatembea barabarani anatokea mtu mbele yake anamzuia asiendelee
Naomba unielewe hii tozo inawasaidia je wasio na kipato, (masikini) wagonjwa, Yatima, walemavu, watoto na wazee. Kwa sababu Asilimia kubwa haya makundi yanatumia malipo ya mtandao kupokea msaada
Umesema hii tozo inawasaidia haya makundi tusaidie kufafanua zaidi.
Tujiulize mimi na wewe serikali ilishawahi kuwanunulia wasio na kipato, Wazee, Yatima, watoto au wagojwa chakula au msaada wowote wapate kuishi? Wanaomba msaada sio, na nyinyi mnamkata. Tuache kutiana ujinga wa Zungu na mungulu.
Je Kuna huduma huyu mtoto anapata akiwa shuleni?
Je Kuna huduma mgonwa anapata akiwa hospital au anapojiuguza akiwa mahali popote hapa Tanzania?
Zahanati yenyewe ukienda kupata kile kadi umwone daktari ni pesa.
Huyu Yatima serikali inamjali vipi atimize ndoto zake serikali ikiwa Kama mlezi. Hawa watu hawana Hali ya kutunzwa kwa mkono wa serikali kweli?
Wazee wamelitumikia Taifa hajui suti ni mdudu gani Leo kachoka anategemea watoto tena Kama anao wenye uwezo na wajukuu na ndugu. Leo hii anapewa hell ya sukari Madilu anakata. Inatia hasira Sana.
Tuombe huyu Jamaa ajiuzulu tu ili tunusuru maisha ya wengine.