Music producers wakali kwenye bongo fleva kwa sasa

Music producers wakali kwenye bongo fleva kwa sasa

Hope umeangalia Dar zaidi pia mikoani kuna maproducer wakali tuu Arusha yuko DX wa noise maker production,wapi Duke,Kanyeria,Pancho latino,Dunga,akili the brain..
 
mngetusaidia na nyimbo zilizowaongoza kutuambia hao wakali..clubs nyingi huwa nazisikia zile za raymond, natafuta kiki na kwetu...ila ile mitungi, mikasi huwa naonaga imetulia sana. Hata hivyo utamu wa pipi ni mate yako mwenyewe.
 
Been waiting for this kinda topic for quite some time. Music industry as a whole imekuwa nchini ila music production imeonekana kutopiga hatua kabisa namaanisha kabisa. Audio quality zetu ni mbovu haziendani na audio quality za miaka ya Leo duniani.

Producers na wasanii wawekeze kwenye music production kama wafanyavyo kwenye video. Music industry kama bongo movies; producer huyo huyo, sound engineer huyo huyo, mastering inafanywa na huyo huyo, beat imetengenezwa na huyo huyo. Kuna watu wanao uwezo wa kufanya vyote kwa ufanisi ila isiwe kila wakati ili kulinda quality ya production.

Matumizi ya drums kwenye kila wimbo sasa inaboa. Dayamondi nae kila wimbo anatumia tarumbeta hadi inakera. Inabidi tubadilike kuleta ladha tofauti.

Leo kuna hi-fi sound ila kwenye muziki wetu ni kama msamiati mpya. Ukisikiliza nyimbo za bongo kwenye headphones au loud speaker husikii tofauti yeyote sana sana quality ndiyo inakuwa mbaya Zaidi. Hii inatokana na audio zetu kuwa na ombwe in the background (for lack of a better term). Tuongeze matumizi ya synth pia.

Kuna mvuto wa pekee kwenye intro na outro kwenye music na zamani tulikuwa vyema kwneye hili ila miaka ya Leo naona imepotea wakati Bado ni kitu cha muhimu kwenye music. Producers wakubwa kama kanye West anatumia sana hii trick na ndiyo sababu ya kuwa among best producers kwa muda sasa. Ni kawaida muziki wetu siku hizi kuanza na kuisha ghafla tu as thou producer alikua na haraka smh.

Muziki wa taratibu unakosa harmony kitu ambacho ni muhimu sana kwa aina hiyo ya music. Kudos to Ali Kiba kwa wimbo wake wa Aje naona alizingatia hilo na wimbo umetoka bomba kweli japo sijui nani alisuka ile production

Pamoja na yote hayo naamini tukiamua tunaweza kama ambavyo wasanii waliamua kuwekeza kwenye video na kuweza. Wimbo kama Gere produced by Nah reel by far ni moja kati ya production nzuri za hivi karibuni. Producers wetu wasichoke kujifunza na kuwekeza kwenye vyombo na sound engineering. Wasikilize productions za producers wakubwa na wenye mafanikio kama Kanye West/Mike Dean na kufonzya maarifa zaidi pale wanapopwaya.
 
You have a point, ila hoja yako ina base kwenye mastering ambayo pia inahusisha sound engineering... Kwa bongo sababu ya gharama ni kama hamna ila binaweza kufanyika.
Hivi hauwezi kujiwekeza kwenye mastering mtu ukawa unatoa vitu vizuri sana? mastering gharama yake ipo sehemu gani...?
 
jamani nyimbo ya joh makini na chidnma audio imetengenezwa na producer gani ? vipi kuhusu Wivu ya Jux?
 
jamani nyimbo ya joh makini na chidnma audio imetengenezwa na producer gani ? vipi kuhusu Wivu ya Jux?
Perfect Combo, producer ni RKay ni jamaa mmoja kutoka Kenya, yupo kwenye Industry kwa muda mrefu sasa, na anafanya vizuri pia
 
dah, mwaka kesho kutwa ntaingia hapo kweny list wakuu
 
ngoma kali zote mjini kwa sasa zinatoka kwa abbydady
 
Back
Top Bottom