Musoma: Ahama nyumba kutokana na visa vya wanyama kama nyoka, Simba, Chui na moto wa ajabu

Musoma: Ahama nyumba kutokana na visa vya wanyama kama nyoka, Simba, Chui na moto wa ajabu

Song of Solomon

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2021
Posts
2,752
Reaction score
5,609
FAMILIA moja ya Mwalimu Mstaafu katika mtaa wa Morembe kata ya Bweri, Musoma mjini imelazimika kuhama katika nyumba iliyokuwa ikiishi kutokana na visa mfululizo vya wanyama wakali kama nyoka, Simba, Chui na hata moto wa ajabu unaoteketeza vitu vya ndani.

Mwalimu Mary Warioba alistaafu utumishi mwaka jana akiwa akifundisha katika Shule ya Msingi Ryamrimi nakuamua kujenga nyumba yakustiri familia yake aliyoishi yeye, mtoto wake na mjuu tangu mwaka jana.

Hata hivyo, nyumba hiyo imegeuka shubiri kuanzia Oktoba pale mauzauza yalivyoanza kuitesa familia hiyo. Bi Mary anadai kuwa visa vilianza baada ya kuonekana watoto kuanza kulalamika kuwa kulikuwa na Joka ndani hata hivyo yeye hakuweza kuliona.

“Tukaanza kuona Simba, Chui ndani ya fensi (uzio) baadaye kinyesi cha binadamu kikawa kinapakazwa kwenye kuta, magodoro, vyombo hata tukipika chakula tukitaka kula tunakuta kinyesi cha binadamu,” amesema Mary.

Ameongeza kuwa ilipofika Novemba 3 Mwaka huu ulianza kuzuka Moto ambao uliteketeza akiba ya vyakula vilivyohifadhiwa kwenye stoo pamoja na magodoro.

“Ule moto ulikuwa unazuka wakati wowote na kuteketeza kitu chochote,” amedai.

Baada ya kushuhudia hali halisi na kusimuliwa juu ya matukio Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, ACP Longinus Tibishubwamu, ameshauri familia ihame kwa muda wakati taratibu za kutafuta ufumbuzi wa hali hiyo zikiendelea.

Imeandaliwa na Editha Majura, Musoma.

#habarileoUpdates #dailynewsdigitalupdates
 
Mstaafu ni mwongo huyo! Ametumia pensheni yote kujenga nyumba ya kuishi na hela itakuwa imekata, anachokifanya ni kutafuta sababu auze hiyo nyumba apate pesa bila kustukiwa na family
 
Back
Top Bottom