Mussa Mangu ashinda rufaa ya kupinga kunyongwa kwa mauaji ya Erasto Msuya

Mussa Mangu ashinda rufaa ya kupinga kunyongwa kwa mauaji ya Erasto Msuya

Kweli huyo jamaa kimazingira hakuwa na hatia ni vile tu jeshi letu la polisi lipo nyuma sana kwenye investigations.....
Hiyo inanikumbusha wale jamaa walimuua yule mzungu mpinga ujangili Wayne Lotter (R.I.P). Kuna yule mdada aliunganishwa kwenye kesi eti kisa tu alikuwa anawapikia chakula. Wote walihukumiwa kunyongwa.
 
Kama alimuendesha mtuhumiwa Hadi kwenye mauaji na yeye hakuripoti polis baada ya tukio ujue na yeye ni sehemu ya tukio
Inawezekana yeye ni muajiriwa tu wa huyo boss. Boss kafanya mauaji akiripoti Boss akafungwa na yeye ajira yake itakuwaje!? MaBoss wengine ni Mafia unamripoti taarifa zinarudi kwake kupitia Askari Chawa, itakuwaje hapo!?
 
Habari wana jukwaa natumaini mpo salama!

Mfungwa Mussa Mangu aliyekua anatumikia adhabu ya kunyongwa hadi kufa kwa kuhusika katika mauaji ya Bilionea Erasto Msuya ameachiwa huru jana baada ya kukata rufaa yeye na wenzake wanne.

Mahakama ya rufaa imeamua Mussa Mangu kuachiliwa huru mara moja baada ya kuonekana hana hatia wakisiliza hukumu hiyo kupitia "video conference" wakiwa Ukonga Gerezani walikohifadhiwa

View attachment 2586007
Alikuwa anasubri kunyongwa alikuwa Bado hajaanza kutumikia adhanu ya kunyongwa.
 
Je baada ya kosa kutendeka na kujua,je alitoa taarifa kwa Jeshi la Police au nae alificha Siri!!??
Inategemea, je shtaka lake lilikuwa lipi? Kama shtaka lake lilikuwa kuhusika na mauaji hizo sababu zitakosa msingi, lakini kama kosa lake ni kushuhudia mauaji na kukaa kimya hapo sawa.
 
Inategemea, je shtaka lake lilikuwa lipi? Kama shtaka lake lilikuwa kuhusika na mauaji hizo sababu zitakosa msingi, lakini kama kosa lake ni kushuhudia mauaji na kukaa kimya hapo sawa.
Kushuhudia na kukaa kimya hakumfanyi yeye apewe adhabu ya kifo kama aliyeua.
 
Je baada ya kosa kutendeka na kujua,je alitoa taarifa kwa Jeshi la Police au nae alificha Siri!!??
aliweza akawa alitishiwa sana,kumbuka anafamilia .na kibaya boss alihusika.unadhani angefanyaje !!?
 
Simple mkuu, hajawa linked na crime scene, tatizo tunaishi kwenye nchi ambayo bado inatumia mbinu za kipelelezi za miaka ya 20s,yaani kipigo, kulazimisha ushahidi, kukamata ovyo bila ya kujiridhia beyond doubts kuwa suspect ni mhusika, ni ndoto yangu kujenga DNA lab, iwe chini ya TP, nita train foresinc investigatives na finger prints za watanzania wote zitahifadhiwa ndani ya lab hii, watch the space
Una mawazo yaliyoendelea kijana.

Lakini mbona DNA lab ipo pale kwa Mkemia Mkuu wa Serikali?
 
Hiyo inanikumbusha wale jamaa walimuua yule mzungu mpinga ujangili Wayne Lotter (R.I.P). Kuna yule mdada aliunganishwa kwenye kesi eti kisa tu alikuwa anawapikia chakula. Wote walihukumiwa kunyongwa.

Yule alificha silaha makaburini. Ndicho kilichomwangusha.
 
Back
Top Bottom