Mussa Mangu ashinda rufaa ya kupinga kunyongwa kwa mauaji ya Erasto Msuya

Kweli huyo jamaa kimazingira hakuwa na hatia ni vile tu jeshi letu la polisi lipo nyuma sana kwenye investigations.....
Hiyo inanikumbusha wale jamaa walimuua yule mzungu mpinga ujangili Wayne Lotter (R.I.P). Kuna yule mdada aliunganishwa kwenye kesi eti kisa tu alikuwa anawapikia chakula. Wote walihukumiwa kunyongwa.
 
Kama alimuendesha mtuhumiwa Hadi kwenye mauaji na yeye hakuripoti polis baada ya tukio ujue na yeye ni sehemu ya tukio
Inawezekana yeye ni muajiriwa tu wa huyo boss. Boss kafanya mauaji akiripoti Boss akafungwa na yeye ajira yake itakuwaje!? MaBoss wengine ni Mafia unamripoti taarifa zinarudi kwake kupitia Askari Chawa, itakuwaje hapo!?
 
Alikuwa anasubri kunyongwa alikuwa Bado hajaanza kutumikia adhanu ya kunyongwa.
 
Mleta madam tuliza kwanza akili kwa sababu unayo,Kisha ulete habari kamili.
 
Je baada ya kosa kutendeka na kujua,je alitoa taarifa kwa Jeshi la Police au nae alificha Siri!!??
Inategemea, je shtaka lake lilikuwa lipi? Kama shtaka lake lilikuwa kuhusika na mauaji hizo sababu zitakosa msingi, lakini kama kosa lake ni kushuhudia mauaji na kukaa kimya hapo sawa.
 
Inategemea, je shtaka lake lilikuwa lipi? Kama shtaka lake lilikuwa kuhusika na mauaji hizo sababu zitakosa msingi, lakini kama kosa lake ni kushuhudia mauaji na kukaa kimya hapo sawa.
Kushuhudia na kukaa kimya hakumfanyi yeye apewe adhabu ya kifo kama aliyeua.
 
Je baada ya kosa kutendeka na kujua,je alitoa taarifa kwa Jeshi la Police au nae alificha Siri!!??
aliweza akawa alitishiwa sana,kumbuka anafamilia .na kibaya boss alihusika.unadhani angefanyaje !!?
 
Una mawazo yaliyoendelea kijana.

Lakini mbona DNA lab ipo pale kwa Mkemia Mkuu wa Serikali?
 
Hiyo inanikumbusha wale jamaa walimuua yule mzungu mpinga ujangili Wayne Lotter (R.I.P). Kuna yule mdada aliunganishwa kwenye kesi eti kisa tu alikuwa anawapikia chakula. Wote walihukumiwa kunyongwa.

Yule alificha silaha makaburini. Ndicho kilichomwangusha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…