Lady Whistledown
JF-Expert Member
- Aug 2, 2021
- 1,147
- 2,008
Kijana Mussa Ally (21), Mvuvi na Mkazi wa Sahare Jijini Tanga anaendelea na matibabu Hospitali ya Mkoa wa Tanga Bombo na kwa sasa amepata nafuu baada ya kushambuliwa nyumbani kwa Bondia Hassan Mwakinyo alfajiri March 04,2025 na kufikishwa Hospitali akiwa mahututi na majeraha mwilini.
Akiongea Hospitalini hapo Kijana huyo amesema Mwakinyo alimshambulia kwa kisu na kumfungulia mbwa sita saa 12 alfajiri alipokuwa akiokota nazi zilizokuwepo barabarani katika mtaa wa
Sahare anaoishi Mwakinyo "Mimi ni Mvuvi nafanya kazi za Baharini, siku ya tukio niliamka kwenda kufanya kazi ya kuchomeka nguzo maeneo ya Tanga Beach hii ni kazi tu niliyoipata kwa siku hiyo"
"Niliwa njiani nikaziona nazi zimepangwa na nikaanza kuziokota, ghafla Hassan Mwakinyo alifika akiwa na Kijana wake wa kazi wakaniuliza nazi nimetoa wapi? nikajibu nimeziokota, Mwakinyo akajibu umeyakanyaga na kuanza kunishambulia kwa kunipiga mtama na kuniburuzia nyumbani kwake, zile nahisi kama zilitegeshwa"
"Mwakinyo wakati anaendeelea kunishambulia akamuagiza
Kijana wa kazi kisu na kuanza kunikata miguu na kunivua nguo na kufungulia mbwa waliokuwa wakinijeruhi kwa zaidi ya lisaa limoja, nikakaa pembeni nikiwa nimekata tanaa nasubiri kufa tu, akaja Mwenyekiti baadaye wakaja Polisi nikawasikia wanasema ameshakufa huyu tumburuze tu, baadaye nikajikuta Hospitali"
Kwa upande wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Tanga limethibitisha kumshikilia Hassani Mwakinyo (29), Mkazi wa Sahare Jijini Tanga kwa mahojiano kuhusiana na tuhuma za kushindwa kudhibiti mbwa wake, ambao walimshambulia na kumjeruhi Mussa Ally (21), Mvuvi na Mkazi wa Sahare Jijini Tanga "Tukio hilo limetokea nyumbani kwa Mwakinyo baada ya mbwa hao kuachiliws huru katika eneo la nyumbani kwake
Chanzo: Millard Ayo