Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,681
- 8,887
Naibu spika wa Bunge, Mussa Zungu akiwa kwenye mkutano wa ITAC unaohusu ushiriki wa wananchi kwenye maendeleo ya nchi, ameipongeza Serikali kwa kuwasikiliza wananchi na kupunguza Tozo.
Zungu ametaka kujivunia na kufunga mkanda kujenga wenyewe badala ya kutegemea misaada kwani inaenda kupungua kutokana na vita inayoendelea Ukraine
=======
Mussa Zungu: Kwanza mimi niipongeze Serikali kwa kuwasikiliza wananchi, wananchi wamepiga makelele na Serikali imesikiliza vizuri na Rais ameagiza ipitiwe(Tozo) na makelele yakazidi Rais akaagiza ipitiwe tena, imepitiwa na imepunguzwa sana.
Huu ndio uwajibikaji na uwazi ambao wananchi wamepeleka hoja kwa Serikali na mheshimiwa Rais ametoa maelekezo kwa Serikali yake na mmeona juzi gharama zimeshuka sana.
Pamoja na hayo zinajenga vituo, zinajenga hospitali ambayo wewe na mkeo mnakwenda kujifungua.
Tujivunie kujenga vitu vyetu tusingoje misaada, misaada huko mbele itapungua kutokana na vita ile nchi zenyewe zinazotusaidia zenyewe zina matatizo makubwa sana, na sisi wenyewe tujifunge mkanda tujenge chetu.
Kitu muhimu pesa hakuna, isitumike kwenye matumizi ambayo sio sahihi, matumuzi ya anasa, zitumike kwa maendeleo ya wananchi.