Must see Movies

Mwanangu upo kama mimi Moja Kati ya vitu vilivyonichosha ni video graphics zake yaani ilinipa kizunguzungu mpaka nikaona niishie dk 30 tu nilishindwa kuimaliza aisee nikaamua niifute kabisa ila nimejifunza kitu tusipende download tu movie kwasababu wengi wamesema nzuri au promo nikubwa
 
Carter ni ya kiboya sana.

Nadhani watu tuna perception tofauti kuhusu muvi, kwa wengi kwao muvi ni action tu hata kama quality mbovu, story mbovu hata acting mbaya.

Binafsi kwangu muvi iwe kali basi kila sehemu ijitahidi kuanzia story, cinematography, visuals, acting, sounds n.k.

Nadhani wengi wanaolalamika muvi mbovu wapo kundi hili nililopo mimi.
 
Kwa promo tu walifanya kazi yao kwa ufasaha ila kawaida tu. Na hao jamaa walioedit mara camera inazunguka, mara chini mara juu wale wameharibu, movie haijatulia, vile vipande ukiangalia unaweza sema ni music video ndio tunaona edit za hivyo.
 
Mnafeli wapi muvi nzuri sana hiyo. Huwezi linganisha na muvi aina ya dr strange na kina captain america muvi za vile nilipenda moja tu inaitwa Birds of Prey
 
Kwa promo tu walifanya kazi yao kwa ufasaha ila kawaida tu. Na hao jamaa walioedit mara camera inazunguka, mara chini mara juu wale wameharibu, movie haijatulia, vile vipande ukiangalia unaweza sema ni music video ndio tunaona edit za hivyo.
Huo ni upekee wa hiyo muvi sijawahi one muvi imetendewa haki kwenye kucheza na camera kama hiyo. Mmezoea animations za marvel kama unacheza GTA
 
Mnaigana kizunguzungu? Basi cameramen walifanya vyema
 
Huo ni upekee wa hiyo muvi sijawahi one muvi imetendewa haki kwenye kucheza na camera kama hiyo. Mmezoea animations za marvel kama unacheza GTA
Mkuu umependa vile jinsi kamera zinazunguka zunguka mara uvunguni, mara pembeni, mara kama wana zoom out etc?! Binafsi sijapenda nkajikuta nazungusha sana shingo mpk zile scenes zikiisha nakuwa kama kizunguzungu. Na pia zile effects za moto hazijakaa sawa mkuu, moto wa uongo uongo yani movie inakuwa kama low budget movie japo kwenye mapigano wamejitahidi
 
Jamaa anajitahidi kuwatetea lakini ukweli graphics ya movie yao ilikuwa ovyo na walizidisha computer sana
 
Nyie jamaa, kuna mtu ameiona Thor, mi nimeiangalia jana sijaridhika nayo kabisa naipa 4/10 yani ni tofauti kabisa na zilizopita, fiction zimekua za kipuuzi puuzi tu..
 
Nyie
ACCIDENT MAN 2: HITMAN'S HOLIDAY

naomba link nikaishushe hiyo muvi haraka sana bila kuchelewa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…