Must see Movies

Glass onion..The knives out mystery.

Death on the nile fulani hivi kwa mbali..
 
Mi hata sijaiona, kama ina rates za ajabu basi ngoja niachane nayo
Halafu kuna watu walikuwa wanaisifia Violent Night humu, leo nimeiangalia. Mbona ni muvi ya kawaida sana hii
kama vP ishi nayo kwani trailer yake ipo vP
 
Unajua yule mzee wa Nobody ile ndio filamu yake ya kwanza kuiona sikuwahi kuona filamu zake za nyuma!! Japo nimeshazigugu kesho nitaanza kushusha moja moja
Hahahaa yule mzee ni comedy sana mule ndio kacheza serious na nadhani hana muvi nyingi za action pia
 
Yani umeweka hadi vikatuni kweli nikaharibu bando? [emoji848][emoji848][emoji848][emoji848]
Paws of Fury ni kali mara mia ya Violent Night[emoji41][emoji41]
Sio level moja kabisa, kaiangalie kwanza halafu ndo uje kuijudge
Hata mimi Violent Night nimeiangalia kwanza, halafu ndo nikaijudge
Nyongeza ya animations hiyo hapo
Minions: Rise of Gru
Sea Beast
Chickenhare and The Hamster of Darkness
The Bad Guys, etc
Movies nyingi umeziona, ila kuanzia mwaka unaanza (January) muvi nilizozikubali ni
Uncharted 2022
Sonic The Hedgehog 2 2022
Adam Project 2022
Carter 2022
The Man from Toronto 2022
Dayshift 2022
Doctor Strange the multiverse of madness 2022
The Takedown 2022
Bullet Train 2022
Troll 2022
Texas Chainsaw Massacre 2022
Seoul Vibe 2022
The Grayman 2022
Topgun Maverick 2022
Restless 2022
Beast 2022
Prey 2022
Silverton Siege 2022... na nyingine nyingi ambazo nina imani umeshaziona
 
Sikuhizi ukiona movie ya Bruce Willis kaa nayo mbali hamna kitu humo!
Sijajua ni umri au director kamtupa.
Halafu kuharibu movie kunaanza pale star anapokuwa ndiye director, ndo story writer na executive producer. Nikishaonaga hivi najua tu bando lilienda bure. The same to Wills new movie the day to die. Yaani jina linashawish humo ndani Sasa ni ujinga ujinga mwingi uliopakwa wese unga'e
 
Labda director kamtupa au budget yake ndogo sana maana wapo actors wenye umri kama wake na movie zao bado nzuri mfano mzee Taken!!
Movie mpaka inafika katikati hata haivutii.
 
Trailer nililiona liko fresh tu
Ila umenipa idea nitakuwa naangalia ratings kabla sijadownload movie
Hapana kuna muda watu huwa wanapuuzia kuangalia movie ko hata rates huendana na watu wangapi wameangalia pia wakaipenda movie husika ko sio lazima kuzingatia rates maana kuna movie nyingine utopolo lakini utakuta 9 rates [emoji23].

Trailer nimeicheck inashawishi iko moto jitoe muhanga 300 mbs kitu gani bhana mimi mwenyewe naishusha baadae [emoji23].
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…