Must see Movies

Wakuu kuna anaefahamu muvi nzuri za Kihindi za kutumia akili nyingi mfano wa 3 idiots hivi anipe list hapa nizisake niburudishe akili
Wahindi wana zile actions zao amazing sana huwa nazikubali sana[emoji16], jaribu kugugo movies zao halafu ingia sites kama fzmovies utazukuta mingi tu
 
Wahindi wana zile actions zao amazing sana huwa nazikubali sana[emoji16], jaribu kugugo movies zao halafu ingia sites kama fzmovies utazukuta mingi tu
Nina miaka sasa sijaangalia muvi ya kihindi hata moja. Huwa nahofia sana kupoteza MB zangu. Naona sio salama kutupia MB kwenye muvi za Kihindi
 
Unaogopa yale mapigo ya kuua mtu na ndizi[emoji16][emoji16]
Kuna clip moja ya kihindi niliiona sijui kama kweli imetoka kwenye muvi, kulikuwa kuna ndege ipo matatizoni huko angani nusu ipate ajali, lakini kuna ndege ilikuwa jirani ikabidi watoe msaada wakaifunga ndege iliyo matatizoni na kamba wakaunganisha na ndege yao Kisha wakawa wanaivuta. Yaani ndege inaivuta ndege nyingine na kamba na wote wapo angani.
Aisee tangu siku ile hawa jamaa nawaheshimu sana na sitaki hata kushobokea muvi zao[emoji23][emoji23]
 
Wahindi wanavituko sana. Niliona moja hiyo jamaa anapigana sijui na adui kwenye ghorofa A halafu kuna surgery ya moyo anafanyiwa mtu ghorofa B. Yule mwamba alimpiga sijui ni ngumi yule adui moyo wake ukachomoka ukaenda mpaka ghorofa B kwa yule mgonjwa aliekuwa anafanyiwa surgery, alikuwa ashapasuliwa kifua ule moyo ukadumbukia pale na hapohapo ukaanza kudunda jamaa akapata nafuu. Asieee nilishangaa sana inakuaje watu wazima mnaandaa movie hata mwez mzima halafu mnakuja vichekesho kama hvo[emoji16][emoji16]
 
Maproducer wa kihindi ni wabongo wenye rangi nyeupe

Sent from my CPH2159 using JamiiForums mobile app
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kabisa mkuu[emoji16][emoji16]
Wahindi walikuwa zamani enz za Amita Bachan, Sunny deol,Sanjay Dat,Omrish Pur,Jack Shrof,Ajay Devgan,King SRK,Akshay Kumar, Hrithik Roshan,Sunil Shetty n.k waliteka sana soko yaani walikuwa wanatoa vyuma tupu usipolia kwenye story tamu kama Kal Ho Nao(Nani anaijua Kesho),utaguswa na Tere Naam(Jina lako) au hisia zitaamshwa na Qayamat(Kiama) apo tumeacha Aandha Kanon(sheria kipofu) oyaaa hawa jamaa walikuwa wanajua mpaka wanakera japo movie masong kibao sometime masaa hadi ma3 unaangalia tu movie moja lakin huchoki.

Sent from my CPH2159 using JamiiForums mobile app
 
Hongera kwanza kwa kuyajua hayo majina mpaka kiswahili[emoji16][emoji16]. Mabanda umiza yatakuwa yanakujua sana.
Movie za kihindi wana action za uongo sana...unaweza kuta movie Kali ila hizo action utoto mtupu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…