Must see Movies

Farzi umeicheki?
 
Naisubiri season 2 kwa hamu sana. India kwenye story wako poa sana humo ndani wamefanya unyama sana. Hiyo Farzi kuna kipindi nilikuwa naicheki yanakuja mawazo na mimi nitengeneze mzigo wa Farzi yaani ilifikia nikaishika noti ya 10k nikaichunguza kwa umakini sana.

Mkuu icheki Thunivu imetoka mwaka huu, ni hatari sana.
Farzi a.k.a Fake tamu sana
 
Nilikuwa nataka kudownload RRR baada ya kukaa miaka 3 bila kuangalia muvi ya Kihindi lakini kila nikitaka kufanya uamuzi nafsi inanisuta sana na kunikumbusha bando nililochoma miaka mitatu iliyopita kisa hawa jamaa.
Ikabidi niangalie trailer lake kwanza. Nimeona bado Wahindi hawajabadilika, yaani sehemu za action kama kawaida yao ni Slow Motion mwanzo mwisho, halafu nikaona kuna mtu kaikanyaga pikipiki kwa nguvu kisha ikaruka hewani na ikazunguka juu kwa juu round moja halafu akaituliza chini, nikaghairi hapohapo kuidownload [emoji23][emoji23]
 
Kana kwamba anacheza mpira wa miguu
 
Dude lina MB 450
 
[emoji23][emoji23][emoji23] unataka kuwa kama artist....hiyo thunivu ngoja niishushe nilikuwa nahofia kuchoma MBs zangu
 
Iangalia kaka [emoji16][emoji16][emoji1787][emoji1787]ukiachana na mtu kurusha pikipiki movie inastory nzuri sana
 
Nilikuwa nafuatilia series ya mwaka jana inaitwa "1899". Hii series ina story nzuri sana ya kufikirisha lakini nilipofika episode ya pili nikaona scene ya ushoga. Nikaishia hapohapo nikafuta na episode zote mbili ila bila ushoga series ilikuwa inaelekea kuwa tamu. Siku hizi Netflix wanapenda sana LGBT sijui shida nini. Bahati mbaya Hadi Wakorea nao wanaonesha huu ushenzi katikati ya muvi zao kama Project Wolf au series zao kali kama Squid Game.

Nikaona sio mbaya, nimeona kila mtu anaisifia Cobra Kai ingawa imefika season 4 sijui 5 na mimi nikaamua nianze nayo Season 1 na season 4 nitaifikia muda sio mrefu, maana episode zake zina MB chache sana halafu episode moja ni nusu saa tu. Huu mzigo binafsi nimeuelewa. Naendelea nao sasahivi. Hao 1899 wabaki na ushoga wao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…