Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kuna wild card ya Jason statham
kuna movie inaitwa John Wick starring ni keanu reeves yule jamaa wa matrix.ni bonge la movie aiseee....ni moja kati ya best movies za 2014
kuna movie inaitwa John Wick starring ni keanu reeves yule jamaa wa matrix.ni bonge la movie aiseee....ni moja kati ya best movies za 2014
Yaani nilimkubali sana mwandishi wa "script" ya hii movie. Keanu ndio kabisa yaani kavaa uhusika barabara!
Dah! Hii movie ni kali ajabu...full action
kweli kabisa mkuu, alieandika script ya ile movie John Wick ni noma sana yani.imetulia sana aisee, haichoshi hata kidogo...pia ni kweli kabisa kua Keanu amevaa uhusika ipasavyo yani, na yule mzee Viggo nae amenogesha sana movie
Nilienda kuangalia John Wick pale M'City na shemeji yenu mpaka leo anakumbuka pale viggo anapomwmbia mwanawe "that fuc**n nobody, is John Wick".
hahahahahaaa,yani kaka mi mwenyewe mpaka leo kile kipande sichoki kukiangalia.hayo maneno ya Viggo ndo my best quote kwenye ile movie...hiyo ilikua ni baada ya Viggo kumwambia mwanae "it's not what you did, son, that angers me so...it's who you did it to." na mwanae baada ya kujibu "who? that fuc**ng nobody!!!" Viggo ndo akasema yale maneno ambayo shemeji yetu bado anayakumbuka mpaka leo, kama ambavyo nami nayakumbuka pia.
Kiukweli bongo bado tupo nyuma sana kiuandishi na uigizaji pia, ndo maana mtu ukizoea kuangalia movie kali kama John Wick na series kama 24 ya Jack Bauer zenye script kali na waigizaji wazuri ni ngumu sana kupenda bongo movie ambazo kiukweli zinahitaji mapinduzi ya hali ya juu
"I'd like a dinner reservation for twelve" Mimi na shemeji na naamini wengi tulioangalia ile sinema kwa mara ya kwanza siku ile tukadhani jamaa anatafuta suluhu baada ya kuamini labda wale waliomvamia na kuwaua ndio wagomvi wake duh! Walipokuja kuchukua maiti ndio nikachoka.
Hata ukisoma review ya hawa jamaa THE FINE ART DINER: Specialized Waste Disposal: John Wick yaani utaona jinsi wenzetu wanavyopata tabu kuandaa filamu zao na matokeo yake mazuri ndio tunayaona.
Hivi, wakipeleka(ga) sinema zao bodi ya filamu huwa nini haswa kinakaguliwa? Na, Je, Tanzania kuna wakosoaji wa filamu kabla haijatoka ambao hupata fursa ya kutoa ushauri kwa wasanii wetu???
hahahahaaa,ni kweli kabisa kaka. mi pia nlipocheki ile sinema kwa mara ya kwanza na kuskia John Wick akimwambia mtu kwenye simu "i'd like to make a dinner reservation for twelve" baada ya kuwaua wale jamaa nlikua na mawazo "exactly" kama hayo mliyokua nayo kwa mara ya kwanza pia. nkashangaa kumuona yule mzee charlie na vijana wake wamefuata maiti, ambapo baadae nlipokuja kuhesabu jamaa waliouliwa na mtaalamu John Wick nkakuta wapo exactly "twelve" ndo nkachoka kabisa yani.
nashkuru kwa hiyo review kaka,ndo nimeipitia sahivi kwa mara ya kwanza. kwa nilichokisoma kwenye ile review nimekubali kua wenzetu wako "serious" sana na mambo yao,na hakika matunda ya kazi zao yanaonekana.
sidhani kama Tanzania kuna wakosoaji wa filamu kabla haijatoka,na wala sidhani kama kuna jitihada zozote za makusudi za kukuza ubora wa filamu zetu za kitanzania.
nliwahi kuskiliza mahojiano ya msanii mmoja maarufu wa bongo movie, na nkashangaa sana aliposema yeye ana uwezo wa kutoa hata filamu tano ndani ya mwaka mmoja.
kwa hali hiyo ubora wa filamu zetu lazima utakua chini sana, maana filamu za wenzetu wakati mwingine zinachkua miaka kadhaa kabla ya kutoka, na ikitoka inakua na ubora wa hali ya juu.