Jamaa ni kama ana mambo yake nje ya uigizaji maana sijui ni instructor wa ngumi na anatambulika kabisa.
Pia niliwahi soma sehemu kwamba hana mahusiano mazuri saaaana na Hollywood (nahisi ndio maana hajawahi kuwa a leading actor kwenye hizi movies kubwa huko Hollywood).
Pia kuna mdau nilisoma comment yake mtandaoni ambayo kwa kiasi kikubwa inaweza kuwa ndio sababu anaelezea kwamba Hollywood kuna actors wengi sana na wako vizuri kwenye kila kona, wametoa maisha yao kwa ajili ya acting muda wote wako on diet, gym, training etc and available. Profiles zao kuanzia kimuonekano wa nje mpaka kiuigizaji zinawabeba, na wanaweza cheza katika majukumu tofauti tofauti, yani leo anaweza cheza action movie na akafanya poa na bado ukimuingiza kwenye comedy anacheza vizuri vilevile (mf Samuel Jackson na The Rock) ndio maana bwana Scott inamuwia vigumu kutoboa pale kama tunavyodhania.
Hivi bwana Scott nje na mapambano/mapigano ni kitu gani kingine kizuri kwenye acting anaweza kukupatia?!