Mbunge Musukuma ameelezea kisa cha kumfurahisha kilichomtokea alipokuwa China ambapo dereva taxi aliwashusha kwenye gari yeye na mkalimani wake baada ya kuanza kumjadili rais wa China.
Hilo jambo lilimfurahisha sana Musukuma hadi leo akichangia bungeni akapendekeza na kusisitiza na sisi Tanzania tunapaswa kuelekea muelekeo huo. Asichofahamu Musukuma ni kwamba tukifuatisha njia ya China yeye Musukuma asingeweza kuwa mbunge kamwe, sidhani kama hata udiwani anaweza kuupata kama tukichukua njia ya CCP.