Musukuma ashangaa kuwaona mitaani wanaoeneza taharuki sakata la bandari, ataka hatua zichukuliwe

Musukuma ashangaa kuwaona mitaani wanaoeneza taharuki sakata la bandari, ataka hatua zichukuliwe

Mbunge Musukuma ameshangazwa kuendelea kukutana mitaani na watu walioneza propaganda kuhusu miaka 100 kwenye mkataba wa Bandari kati ya Serikali ya Tanzania na kampuni ya DP World. Musukuma amedai vyombo vya ulinzi na usalama wamekuwa wapole na haiwezekani kwenda kwa namna hiyo bila hatua kuchukuliwa.

Musukuma amesema siku za mbeleni yatakuja mambo makubwa kuliko hayo na yakasumbua. Musukuma amewaasa watu wanaomiliki uchumi wa Tanzania kuungana kwani ndio wanaopata adha bandarini

Mwambieni Musukuma kuwa Watanzania wanaishangaa TAKUKURU kwa nini Musukuma yupo mtaani huku ana tuhuma ya kuhongwa gari V8, dola 50,000 na kulipiwa gharama za utalii.
 
Hili kuondoa conflict of interest, Wabunge wa Kamati ambao walioshiriki kwenda India na Dubai ,wazuiwe kuijadili hoja hii bungeni bali wahusike kujibu maswali yatakayoulizwa na wabunge ambao hawakuhusika na safari.

Sababu, kwanza kwa mujibu wa Mbunge wa uzi huu,inaonekana wabunge hawa waliosafiri wako upande wa serikali, na wanaitetea serikali wakati kiutaratibu Mawaziri na Manasheria Mkuu wa serikali ndiyo kazi yao.
 
STOCK-DP-WORLD-JEBEL-ALI-PORT_18138efba14_large.jpg

DpWorld Jebel Ali Port mizigo haikai hapo ni mwendo wa masaa tu mzigo uko Dukani.
 
Mbunge Musukuma ameshangazwa kuendelea kukutana mitaani na watu walioneza propaganda kuhusu miaka 100 kwenye mkataba wa Bandari kati ya Serikali ya Tanzania na kampuni ya DP World. Musukuma amedai vyombo vya ulinzi na usalama wamekuwa wapole na haiwezekani kwenda kwa namna hiyo bila hatua kuchukuliwa.

Musukuma amesema siku za mbeleni yatakuja mambo makubwa kuliko hayo na yakasumbua. Musukuma amewaasa watu wanaomiliki uchumi wa Tanzania kuungana kwani ndio wanaopata adha bandarini

Anaongea akili zake

Uhuru wa maoni umelindwa.

Anaona ana uhuru kuliko wengine
 
Huyo punguani atuonyeshe kikao cha wananchi au Baraza la Madiwani lililomtuma kuunga mkono kuuzwa bandari. Usitusemee ujinga
 
Tununue teknolojia hii tuendeshe wenyewe!!!
Hatuwezi, hizo machine tutazinunua kwa mara ishirini ya bei halisi Machine mbili tu zitatucost matrilioni ya fedha kuzisafirisha pia tutapiga mara kumi ya bei halisi ya usafirishaji.
 
Hatuwezi, hizo machine tutazinunua kwa mara ishirini ya bei halisi Machine mbili tu zitatucost matrilioni ya fedha kuzisafirisha pia tutapiga mara kumi ya bei halisi ya usafirishaji.
Hili neno hatuwezi mara zote Lina nikera.
===
Njia ya kukwepa kulipa mara ishirini kwanza ni kuwapiga stop watu wa Procurement! Tuandae utaratibu maalumu wa kupata Mashine hizi bila mawaa kwa kutumia sheria zetu ulinzi na usalama wa nchi.
 
Hili neno hatuwezi mara zote Lina nikera.
===
Njia ya kukwepa kulipa mara ishirini kwanza ni kuwapiga stop watunwa Procurement! Tuandae utaratibu maalumu wa kupata Mashine hizi bila mawaa kwa kutumia sheria zetu ulinzi na usalama wa nchi.
Labda kizazi kijacho nacho ni kujitia moyo tu ,hebu ngoja tuone atakayekuja baada ya CCM.
 
Huyu na kishimba wakiendelea kusikilizwa kuhusu hoja za elimu wataliangamizs Taifa, wanakandya wasomi kwa sababu ya mafanikio ya biashara waliyoyapata. Kila akiongea lazima akandye wasomi. Watoto wanaweza kuamini kuwa elimu Haina manufaa kwa Taifa
 
Back
Top Bottom