Musukuma: Kuna wanasiasa wameahidiwa 10% kuweka presha ndege kuzuiwa

Hahaha jamani mi hata sielewi hawa viongozi wengine huwa wanawashwa kuongea au sasa musukuma ndugu yangu unaongea nini hapo daaah
 
Mazungumzo ya Makinikia nayo tukiangukia pua watapeleka lawama kwa wanasiasa. Tunataka tusikie mwisho wa siku nani mshindi kama ni serikali basi zile Trilion 400 za TRA tutalipwa
 
Moja yamambo yanayoiaibisha ccm ni kuruhusu kila mmoja aijibie. Ona sasa ugoro kama huu! hapo si ndio ameharibu zaidi na kufanya muzidi kuonekana wajinga?
Hamjiulizi kwanini Mbawala mwenye wizara yenye hiyo ndege yuko kimya? Dr Mpango mwenye Deni la hayo mabilioni kimya? hata Mahiga aliyesafiri kwa siri kwenda Kanada kaufyata na kukwepa kutia neno? Sasa wanakuja kama Musukuma na Polepole ambao hata hivyo kimsingi sio wasemaji au wajibu hoja za serikali wanaleta ngwe ngwe ngwe!
This is bull shit!
 
Msukuma inabidi aelewe kwamba uwezo (kiuelewa) wake unaishia kwenye mambo mepesi mepesi yanayohitaji kubishana tuu. Lakini katika hili bora angenyamaza kwa sababu;
1. Si msemaji wa serikali
2. Halihusiani na vyama vya siasa.
3. Ni nje kabisa ya upeo wa taaluma yake
4. Anawapa kazi wahusika ya kuanza kufikiria namna ya kuweka sawa pale ambapo wasio wahusika wanazungumzia yasiyo wahusu.
5. Siye aliyepaswa kujibu masuala yalozungumziwa na Lisu.
6. Ni utovu wa nidhamu kuingilia mamlaka isiyokuhusu (hata kama chama chako ndicho tawala)

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kumbe ni uzushi?
Sasa yule msemaji wa serikali aliyethibitisha hilo alikuwa anazusha au? Au naye kavuta 10%
By the way, Musukuma kama kawaida yake...atueleze hayo maneno ya wanasiasa wa Tanzania yanawasaidiaje wanaotudai kukamata mali zetu hadi waweke dau la 10%?
 
Hakika!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…