Musukuma: Kuna wanasiasa wameahidiwa 10% kuweka presha ndege kuzuiwa

Musukuma: Kuna wanasiasa wameahidiwa 10% kuweka presha ndege kuzuiwa

Msukuma kweli wee darasa la 4..

Unapingana mpaka na msemaji wa serikali..

Kwaiyo ili uamini ndege imekamatwa ulitegemea uki google utaiona ipo Polisi Post za huko Canada??

Akili zako wewee ni mwisho wa hiyo pua yako..

Mtu asikufananishe hata siku moja na hawa Wabunge wa CCM.. Pigana.
 
Samahani naomba kuuliza "....hivi baadhi ya waheshimiwa wabunge ndio wasemaji wa serikali siku hizi?"
au... au... au...
 
Atutolee upuuzi tangu lini yeye akawa msemaji wa serikali... Kama nnamuona vile kiboda boda nacho kinajipanga kikurupuke nacho na kutema shombo zake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
b2cbb76d17ad6fb0967fed8545a5a2d0.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Katiba inaruhusu kila mtu kutoa maoni yake.
Ya msukuma ndio haya katika hili.
Mungu ibariki Tanzania.
 
anasisitiza sirikali isimsikilize lakini yeye anamsikiliza na kumjibu. huyu anavinasaba na kibajaji?
 
Habari waungwana,

Mwenyekiti wa CCM mkoani Geita na mbunge wa Geita vijijini, Joseph Kasheku almaarufu kama msukuma ameamua kujibu kombora la mwanasheria mkuu wa CHADEMA, Tundu Lissu kuhusu sakata la ndege ya serikali kuzuiwa nchini Canada baada ya wadeni kusema wanaidai Tanzania.

Msukuma kasema deni hilo halijatokana na serikali ya awamu ya tano kwani kazi ilifanyika mwaka 1999 lakini kama Rais haiwezakani kukataa deni la serikali inalodaiwa, ameongeza kuwa suala hilo liko mahakamani na katika hatua za mwanzo sana.

Msukuma ameongeza kuwa kwa sasa ndege hiyo ipo kwa watengeneza ndege kwani hata mitandaoni inaonekana na sio kwamba imekamatwa ila wadai wameenda kufungua kesi kuizuia isiondoke na serikali itapeleka utetezi wake.

Anadai suala hilo limewekewa 10% ili watu waweke presha ili ikatanda kwenye nchi watu waende wakavute 10%. Ametaka serikali ya awamu ya tano isiendelee kusikiliza maneno ya kipuuzi na watanzania pamoja na kuwa na haki ya kuangalia mitandao kusikiliza hizo presha, wangejikita katika maendeleo na kuachana nazo kwani nchi ina madeni mengi.

Msukuma amedai hata ndege za kwanza zilipokuja na kumwagiwa maji, Lissu alidai zimechemsha na wananchi wa kijijini wakaamini ilhali ilikuwa mila na desturi ya ndege mpya kumwagiwa maji, baadae wakadai zinaharibikia njiani wakati bado wanapanda nao.

Msukuma amesema kuchelewa ndege kwa mwezi mmoja kusiibue mjadala na kuwatoa kwenye 'mood' kisha kuwataka wabunge wenzake warudi kwenye majimbo kwani watanzania waliowachagua wana matatizo mengi na wao wanahitaji kwenda kuwasikiliza.


​

Kideo kwa hisani ya Millard Ayo

Msukuma ameamua kua kichaa.
Wether its is true or false. Inatusaidia nini?
Serikali ambayo ni strong INA deal na kila kitu fair and square.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
sio kama ndege imekamatwa ila imezuiliwa isitoke.....
Joseph plus josep= msukuma +msukuma ..naona wanasukumana
 
Kweli lissu kiboko. Kaongea siku kwa nnusu saa ccm nzima wanajibu Leo siku ya tano
 
Back
Top Bottom