Musukuma: Kuna wanasiasa wameahidiwa 10% kuweka presha ndege kuzuiwa

Musukuma: Kuna wanasiasa wameahidiwa 10% kuweka presha ndege kuzuiwa

Habari waungwana,

Mwenyekiti wa CCM mkoani Geita na mbunge wa Geita vijijini, Joseph Kasheku almaarufu kama msukuma ameamua kujibu kombora la mwanasheria mkuu wa CHADEMA, Tundu Lissu kuhusu sakata la ndege ya serikali kuzuiwa nchini Canada baada ya wadeni kusema wanaidai Tanzania.

Msukuma kasema deni hilo halijatokana na serikali ya awamu ya tano kwani kazi ilifanyika mwaka 1999 lakini kama Rais haiwezakani kukataa deni la serikali inalodaiwa, ameongeza kuwa suala hilo liko mahakamani na katika hatua za mwanzo sana.

Msukuma ameongeza kuwa kwa sasa ndege hiyo ipo kwa watengeneza ndege kwani hata mitandaoni inaonekana na sio kwamba imekamatwa ila wadai wameenda kufungua kesi kuizuia isiondoke na serikali itapeleka utetezi wake.

Anadai suala hilo limewekewa 10% ili watu waweke presha ili ikatanda kwenye nchi watu waende wakavute 10%. Ametaka serikali ya awamu ya tano isiendelee kusikiliza maneno ya kipuuzi na watanzania pamoja na kuwa na haki ya kuangalia mitandao kusikiliza hizo presha, wangejikita katika maendeleo na kuachana nazo kwani nchi ina madeni mengi.

Msukuma amedai hata ndege za kwanza zilipokuja na kumwagiwa maji, Lissu alidai zimechemsha na wananchi wa kijijini wakaamini ilhali ilikuwa mila na desturi ya ndege mpya kumwagiwa maji, baadae wakadai zinaharibikia njiani wakati bado wanapanda nao.

Msukuma amesema kuchelewa ndege kwa mwezi mmoja kusiibue mjadala na kuwatoa kwenye 'mood' kisha kuwataka wabunge wenzake warudi kwenye majimbo kwani watanzania waliowachagua wana matatizo mengi na wao wanahitaji kwenda kuwasikiliza.


​

Kideo kwa hisani ya Millard Ayo

Hahaha, absolute toilet ... utafikiri Gigi Money ndo kaongea siyo mbunge!
 
Monday, August 21, 2017
Mbunge Msukuma Kamjibu Tundu Lissu Kuhusu Ndege Kukamatwa Canada Kisa Deni






Mbunge wa Geita (CCM), Joseph Kasheku Msukuma amefunguka na kusema kuwa Rais Magufuli hausiki katika sakata la kuvunja mkataba ambao umepelekea ndege ya Tanzania Bombadier Q-400 Dash 8 kushikiliwa nchini Canada na kusema wapinzani wanatafuta kiki.

Mbunge Msukuma amesema kwa upeo wake jinsi alivyosikiliza upande wa upinzani na majibu ya serikali anaona wazi kuwa ni kweli baadhi ya wapinzani wa nchii hii wanahusika katika kukwamisha jambo hilo kama ambavyo serikali ilivyosema na kudai Rais Magufuli hausiki katika jambo hilo.

"Binafsi yangu naamini kabisa majibu ya serikali kuwa hili suala linauchochezi wa wanasiasa, kwanza vitu vingi walivyosema wapinzani kuhusu sakata hili la ndege ni vya uongo ukianzia lile suala la kuwa Rais Magufuli amekuwa akiiitia hasara serikali hii.

"Tatizo lililopo mahakamani la kampuni inayodaiwa kuishtaki Tanzania kampuni hiyo imefanya kazi mwaka 1998-99 wakati Magufuli hakuwa Rais wa Tanzania" alisema Mbunge Msukuma

Aidha Mbunge huyo aliendelea kudai jumla ya deni la bilioni 87 ambayo serikali ya Tanzania inadaiwa na kampuni ya Stirling Civil Engineering Ltd kwa kuvunja mkataba wa kazi halijatokana na serikali ya awamu ya tano ya Rais John Pombe Magufuli.

"Deni hili siyo kwamba limetokana na uongozi wa serikali ya awamu ya tano lakini kama Rais huwezi kukataa deni ambalo serikali inadaiwa akiwa madarakani lakini pia suala hili lipo mahakamani na hatua iliyofikia ni hatua ya mwanzo kabisaa, na si kweli kwamba ndege imekamatwa unaweza kuingia mitandaoni ukaiona ndege ilipo, bado ipo kwao hao Bombadier hivyo Tundu Lissu anaposema ndege imekamatwa siyo kweli.

"Hao watu hao wanaotudai wameenda kufile kesi ya kuzuia mali za Tanzania zisiondoke na serikali inaweza kutoa utetezi wake kwa hiyo hili suala ni kama linawekwa udalali na yote yanafanyika kutokana na umakini wa serikali ya awamu ya tano kwa hiyo wapinzani wanatafuta kiki tu" alisisitiza Msukuma

Siku ya Jumamosi ya tarehe 19 Agosti serikali ilikiri wazi kuwa ni kweli kuna mgogoro uliopelekea ndege hiyo kushindwa kuingia nchini Tanzania mwezi Julai kama ambavyo ilitangazwa awali na kusema serikali imeanza kufanya jitihada mbalimbali kuhakikisha inamaliza mgogoro huo.


Wasomi chuo kikuu wanahangaika kutafuta majibu ya kumjibu Tundu Lissu leo eti Mbunge Msukuma anayeomba kilimo cha bangi kiwe halali ndiye amjibu Tundu Lissu kweli hii inawaingia akilini. Mbunge Tundu Lissu abaki kujibiwa hoja zake na makao makuu ya polisi au Ikulu siyo na watu kama mbunge Msukuma , Jamani Tundu Lissu ni wa hadhi nyingine walio karibu na mbunge Msukuma wamweleze hivyo tena kwa kisukuma maana lugha ingine yoyota Msukuma hata ielewa.
 
Huyu mtu anajitutumua sana. Nadhani anajigamba kwa kinga yake ya uganga wa kienyeji. But kwenye ukweli uganga utakaa pembeni
 
Darasa la 7 anapojadili mambo makubwa,anapingana hadi na msemaji wa serikali!
 
Habari waungwana,

Mwenyekiti wa CCM mkoani Geita na mbunge wa Geita vijijini, Joseph Kasheku almaarufu kama msukuma ameamua kujibu kombora la mwanasheria mkuu wa CHADEMA, Tundu Lissu kuhusu sakata la ndege ya serikali kuzuiwa nchini Canada baada ya wadeni kusema wanaidai Tanzania.

Msukuma kasema deni hilo halijatokana na serikali ya awamu ya tano kwani kazi ilifanyika mwaka 1999 lakini kama Rais haiwezakani kukataa deni la serikali inalodaiwa, ameongeza kuwa suala hilo liko mahakamani na katika hatua za mwanzo sana.

Msukuma ameongeza kuwa kwa sasa ndege hiyo ipo kwa watengeneza ndege kwani hata mitandaoni inaonekana na sio kwamba imekamatwa ila wadai wameenda kufungua kesi kuizuia isiondoke na serikali itapeleka utetezi wake.

Anadai suala hilo limewekewa 10% ili watu waweke presha ili ikatanda kwenye nchi watu waende wakavute 10%. Ametaka serikali ya awamu ya tano isiendelee kusikiliza maneno ya kipuuzi na watanzania pamoja na kuwa na haki ya kuangalia mitandao kusikiliza hizo presha, wangejikita katika maendeleo na kuachana nazo kwani nchi ina madeni mengi.

Msukuma amedai hata ndege za kwanza zilipokuja na kumwagiwa maji, Lissu alidai zimechemsha na wananchi wa kijijini wakaamini ilhali ilikuwa mila na desturi ya ndege mpya kumwagiwa maji, baadae wakadai zinaharibikia njiani wakati bado wanapanda nao.

Msukuma amesema kuchelewa ndege kwa mwezi mmoja kusiibue mjadala na kuwatoa kwenye 'mood' kisha kuwataka wabunge wenzake warudi kwenye majimbo kwani watanzania waliowachagua wana matatizo mengi na wao wanahitaji kwenda kuwasikiliza.


​

Kideo kwa hisani ya Millard Ayo

hahahahaha kuna vituko duniani eti msukuma kamjibu lissu kuna watu wanachekesha sana.msukuma huku si bungeni kwamba utapigiwa makofi na mbumbumbu wenzako kaa kimya we saizi yako ni bashite
 
Huyo akaendelee na ujambazi ndiyo fani yake, haya kina Lisu hayawezi ni kama kumlinganisha Shakespeare na mchora katuni za kipepe ama madenge
 
Hovyo kabisa wewe, nadhani tumbo linafanya kazi badala ya kichwa.
 
Anatushauri tuendelee kujenga uchumi wetu wa viwanda.....cherehani nne na blender tatu.

Sasa hivi kila mtu kageuka kuwa Msemaji wa Serikali. Hii confusion sio ya kawaida.
 
Nchi imetikisika, kila mmoja,Lisu,lisu,lisu,wakutukana wanatukana, wakupotosha não wako bize, Polisi wanatafuta jinsi ya kuiokoa serikali, wasomi wamepagawa wanaandika mashahiri na kuyafuta, huyu mkata Umeme ni hatari,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Moja yamambo yanayoiaibisha ccm ni kuruhusu kila mmoja aijibie. Ona sasa ugoro kama huu! hapo si ndio ameharibu zaidi na kufanya muzidi kuonekana wajinga?
Hamjiulizi kwanini Mbawala mwenye wizara yenye hiyo ndege yuko kimya? Dr Mpango mwenye Deni la hayo mabilioni kimya? hata Mahiga aliyesafiri kwa siri kwenda Kanada kaufyata na kukwepa kutia neno? Sasa wanakuja kama Musukuma na Polepole ambao hata hivyo kimsingi sio wasemaji au wajibu hoja za serikali wanaleta ngwe ngwe ngwe!
This is bull shit!
Uko sahihi kabisa. Hivi baada ya Lisu kuongea umemsikia Mnyika, Lema, Msigwa au hata Mbowe wakiitisha press conf nyingine na kuongeza au kupunguza maneno ya Lisu?

ACHA nikae KIMYA...!
 
Samahani naomba kuuliza "....hivi baadhi ya waheshimiwa wabunge ndio wasemaji wa serikali siku hizi?"
au... au... au...
 
Back
Top Bottom