Musukuma: Kuna wanasiasa wameahidiwa 10% kuweka presha ndege kuzuiwa

Habari waungwana,

Mwenyekiti wa CCM mkoani Geita na mbunge wa Geita vijijini, Joseph Kasheku almaarufu kama msukuma ameamua kujibu kombora la mwanasheria mkuu wa CHADEMA, Tundu Lissu kuhusu sakata la ndege ya serikali kuzuiwa nchini Canada baada ya wadeni kusema wanaidai Tanzania.

Msukuma kasema deni hilo halijatokana na serikali ya awamu ya tano kwani kazi ilifanyika mwaka 1999 lakini kama Rais haiwezakani kukataa deni la serikali inalodaiwa, ameongeza kuwa suala hilo liko mahakamani na katika hatua za mwanzo sana.

Msukuma ameongeza kuwa kwa sasa ndege hiyo ipo kwa watengeneza ndege kwani hata mitandaoni inaonekana na sio kwamba imekamatwa ila wadai wameenda kufungua kesi kuizuia isiondoke na serikali itapeleka utetezi wake.

Anadai suala hilo limewekewa 10% ili watu waweke presha ili ikatanda kwenye nchi watu waende wakavute 10%. Ametaka serikali ya awamu ya tano isiendelee kusikiliza maneno ya kipuuzi na watanzania pamoja na kuwa na haki ya kuangalia mitandao kusikiliza hizo presha, wangejikita katika maendeleo na kuachana nazo kwani nchi ina madeni mengi.

Msukuma amedai hata ndege za kwanza zilipokuja na kumwagiwa maji, Lissu alidai zimechemsha na wananchi wa kijijini wakaamini ilhali ilikuwa mila na desturi ya ndege mpya kumwagiwa maji, baadae wakadai zinaharibikia njiani wakati bado wanapanda nao.

Msukuma amesema kuchelewa ndege kwa mwezi mmoja kusiibue mjadala na kuwatoa kwenye 'mood' kisha kuwataka wabunge wenzake warudi kwenye majimbo kwani watanzania waliowachagua wana matatizo mengi na wao wanahitaji kwenda kuwasikiliza.

​

Kideo kwa hisani ya Millard Ayo

This guy is smart, Siamini kama ni darasa la saba kweli ama ni zuga tu.
 
Wale waliochelewesha kulipa ndio wana 10%.. Deni kutoka 40billion mpaka 90 billion si mchezo.
 
Habari waungwana,

Mwenyekiti wa CCM mkoani Geita na mbunge wa Geita vijijini, Joseph Kasheku almaarufu kama msukuma ameamua kujibu kombora la mwanasheria mkuu wa CHADEMA, Tundu Lissu kuhusu sakata la ndege ya serikali kuzuiwa nchini Canada baada ya wadeni kusema wanaidai Tanzania.

Msukuma kasema deni hilo halijatokana na serikali ya awamu ya tano kwani kazi ilifanyika mwaka 1999 lakini kama Rais haiwezakani kukataa deni la serikali inalodaiwa, ameongeza kuwa suala hilo liko mahakamani na katika hatua za mwanzo sana.

Msukuma ameongeza kuwa kwa sasa ndege hiyo ipo kwa watengeneza ndege kwani hata mitandaoni inaonekana na sio kwamba imekamatwa ila wadai wameenda kufungua kesi kuizuia isiondoke na serikali itapeleka utetezi wake.

Anadai suala hilo limewekewa 10% ili watu waweke presha ili ikatanda kwenye nchi watu waende wakavute 10%. Ametaka serikali ya awamu ya tano isiendelee kusikiliza maneno ya kipuuzi na watanzania pamoja na kuwa na haki ya kuangalia mitandao kusikiliza hizo presha, wangejikita katika maendeleo na kuachana nazo kwani nchi ina madeni mengi.

Msukuma amedai hata ndege za kwanza zilipokuja na kumwagiwa maji, Lissu alidai zimechemsha na wananchi wa kijijini wakaamini ilhali ilikuwa mila na desturi ya ndege mpya kumwagiwa maji, baadae wakadai zinaharibikia njiani wakati bado wanapanda nao.

Msukuma amesema kuchelewa ndege kwa mwezi mmoja kusiibue mjadala na kuwatoa kwenye 'mood' kisha kuwataka wabunge wenzake warudi kwenye majimbo kwani watanzania waliowachagua wana matatizo mengi na wao wanahitaji kwenda kuwasikiliza.

​

Kideo kwa hisani ya Millard Ayo

Duh! Nimemsikiliza huyu jamaa nimechoka.
Huyu mtu reasoning yake ni ya kiwango cha chini, au siasa zimemvuruga ubongo maana anajichanganya tu.
Kumbe anajibu ili mradi atoe tu majibu!
 
Msukuma angewahi QT amalize vidato vyoote then aende chuo akimaliza asubiri awe awe experince kama , Lisu ndio tutamsikiliza , zaidi ya hapo akusanyedaftari standard 7 B
 
610e8787a9183e6337fcc40116b046c6.jpg
Hii ndio kata funua. Uzalendo wakati watu wanataka kuchukua ikulu. Lazima tutafute sababu za kuwatoa ikulu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kumbe ndege imezuiliwa mwezi mzma?Au inatengenezwa mwezi mzma?Sasa kipi nafuu maana ndege inayotengezwa mwezi mzma haiponi hiyo ni skrepa
 
Naona kila mtu anajipima ubavu kwa Lissu kadri anavyoona anaweza kufanya hivyo katika eneo lake ili aonekane naye anajua....
 
Kama kuna kipimo cha hekima unaweza ukampima mtu mwenye masters kikaonyesha wisdom negative na darasa la saba aliyefeli kikaonyesha positive. Siasa hasa ni hekima za mtu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unajua unaweza kupewa kila kitu katika ulimwengu huu,lakini ukinyimwa akili ni hatari sana kwako na kwa jamii inayo kuzunguka.Mbaya zaidi pale unapokuwa ni kiongozi alafu hufikirii kwanini watu walikuchaguwa na wewe ni darasa la saba.Ingekuwa mimi ni Msukuma hata kusimama bungeni ningeona aibu asee.Darasa la saba unaanzaje kumsema mtu ambaye ana taaluma yake?Mungu nisamehe,ila hawa watu wa pande za uko kwa Sizonje wana utindio wa ubongo.

Darasa la Saba a.k.a King Std Seven Oyeeeeeeeeeee.
 
Kama kuna kipimo cha hekima unaweza ukampima mtu mwenye masters kikaonyesha wisdom negative na darasa la saba aliyefeli kikaonyesha positive. Siasa hasa ni hekima za mtu

Sent using Jamii Forums mobile app
Na kipimo cha mkojo kinapima nini?

In white-collar crime, there are ink stains instead of bloodstains.
 
Back
Top Bottom