This guy is smart, Siamini kama ni darasa la saba kweli ama ni zuga tu.Habari waungwana,
Mwenyekiti wa CCM mkoani Geita na mbunge wa Geita vijijini, Joseph Kasheku almaarufu kama msukuma ameamua kujibu kombora la mwanasheria mkuu wa CHADEMA, Tundu Lissu kuhusu sakata la ndege ya serikali kuzuiwa nchini Canada baada ya wadeni kusema wanaidai Tanzania.
Msukuma kasema deni hilo halijatokana na serikali ya awamu ya tano kwani kazi ilifanyika mwaka 1999 lakini kama Rais haiwezakani kukataa deni la serikali inalodaiwa, ameongeza kuwa suala hilo liko mahakamani na katika hatua za mwanzo sana.
Msukuma ameongeza kuwa kwa sasa ndege hiyo ipo kwa watengeneza ndege kwani hata mitandaoni inaonekana na sio kwamba imekamatwa ila wadai wameenda kufungua kesi kuizuia isiondoke na serikali itapeleka utetezi wake.
Anadai suala hilo limewekewa 10% ili watu waweke presha ili ikatanda kwenye nchi watu waende wakavute 10%. Ametaka serikali ya awamu ya tano isiendelee kusikiliza maneno ya kipuuzi na watanzania pamoja na kuwa na haki ya kuangalia mitandao kusikiliza hizo presha, wangejikita katika maendeleo na kuachana nazo kwani nchi ina madeni mengi.
Msukuma amedai hata ndege za kwanza zilipokuja na kumwagiwa maji, Lissu alidai zimechemsha na wananchi wa kijijini wakaamini ilhali ilikuwa mila na desturi ya ndege mpya kumwagiwa maji, baadae wakadai zinaharibikia njiani wakati bado wanapanda nao.
Msukuma amesema kuchelewa ndege kwa mwezi mmoja kusiibue mjadala na kuwatoa kwenye 'mood' kisha kuwataka wabunge wenzake warudi kwenye majimbo kwani watanzania waliowachagua wana matatizo mengi na wao wanahitaji kwenda kuwasikiliza.
Kideo kwa hisani ya Millard Ayo
Duh! Nimemsikiliza huyu jamaa nimechoka.Habari waungwana,

Inapotokea jambo lolote linalomhusu Lissu wasemaji wa serikali wanakuwa wengi sana. Hata humu JF wapo.Msukuma ni msemaji wa ccm au serikali?
Sent From Ikulu-Magogoni street
Na kipimo cha mkojo kinapima nini?Kama kuna kipimo cha hekima unaweza ukampima mtu mwenye masters kikaonyesha wisdom negative na darasa la saba aliyefeli kikaonyesha positive. Siasa hasa ni hekima za mtu
Sent using Jamii Forums mobile app