Musukuma: Maprofesa wanatuchanganya; wakati wa Magufuli walisema hakuna Corona na wakati huu wa Samia wanasema tuchanjwe

Hata hawa wa ndani, wengi wao wamesoma PhD zao huko huko nje anakotaka wakachukuliwe
Labda anahisi walipomaliza shule waliweka vitabu kwenye makabati..hawakuendelea kujiongeza...things change everyday...wanasayansi wengi wazungu wanaipinga chanjo ya Corona, huku wakwetu wakirecommend...mkanganyiko huu unamzingua msukuma...
 
Msukuma amtafute aliyemnyima kwenda au kuendelea na shule wayamalize. Naona anajitahidi kupamvana na walioenda shule kila kukicha.
 
Kujishangaa Ni dalili za kuchanganyikiwa akili....Kama huyo Kasheku hakuweza kuuliza enzi za mwendazake, kwa Sasa anatupigia kelele anyamaze kimya.
 

Unafiki wa Wabongo hauna justification. Leo hii mtawala aliyepo akiondoka halafu akaja mtawala mwingine mwenye msimamo tofauti na wa huyu wa sasa, Wabongo hawa hawa watamgeuka mtawala wa sasa na misimamo yake.

We’re quintessential sh**hole countrymen and women!
 
Kama walisema hakuna corona nyungu za kichawi ulizokuwa unapiga zilitoka wapi ?
 
Msukuma yupo makini sana walitupiga fumigation hawa jamaa
 
Kwa hiyo na wewe unaamini Corona ya mapapai ya mwendazake? Hivi kweli mapapai yawe na Korona? Corona hushambulia mfumo wa upumuaji, Je, papai lina huo mfumo wa upumuaji unaoweza kuathiriwa na Corona? JIWE kaondoka na akili za wengi
Hata china walipruv hiyo corona ipo kwenye vitasa, nguo, mabomba, na hasa viganja ndo sbb unanawa
 
Msukuma amtafute aliyemnyima kwenda au kuendelea na shule wayamalize. Naona anajitahidi kupamvana na walioenda shule kila kukicha.
Msukuma anapambana na wasomi kama akina Chenge,Prof. Lipumba n.k
 
Enz za mwendazake kulikuwa na option mbili huku ikikupasa kujihadhar nazo n zile tulizokuwa tunatumia shuleni

1 EDUCATION IS BETTER THAN MONEY

2 MONEY IS BETTER THAN EDUCATION

.Ukichagua elimu mwendazake anakuzka mzmamzma

Ukichagua pesa bas itakubid upindishe yote ya ukwel na vyeo utapata BASHIRU ALLY alichagua PESA ndio maana Leo anadharaurika
 
Mfumo wetu wa elimu ni mbovu so Msukuma yupo right... maana sisi wenyewe raia Tunashuhudia Machifu wetu Mangungu wanayoyafanya... hata watoto wa nursery wanastaajabu... and am sure watakuja wasoma sana hawa Mawaziri na Maprofessor uchwara wetu... am sure wasomi wengi Tanzania wametumia sana vibomu kwenye Mitihani yao... yaani kuibia ibia like elimu ya hapa na pale
 
Acha uongo kwahyo yale mapapai ni ww uliyafanyia utafiti?
Kila mwenye akili anajua kuwa hakuna utafiti wa mapapai au kwale uliofanywa. Ni tamko tu lilikusudiwa ili watu wasipimwe corona na iwe rahisi kusema kuwa haipo
 
Naona unasema uongo. Lazima utakuwa na ndugu wa umri mkubwa au wenye matatizo mengine ya afya waliokufa kwa korona ila wote kama sisi wenzako mkaficha vichwa mchangani kwa kumuogopa Magufuli. Na wale wakubwa serikalini mwaka jana na mwaka huu je?
 
Jizungumzie wewe. Ukiwa kama Musukuma, ukaongea sana ukapigiwa makofi, na ukaona watu hawakumpigia makofi sana profesa mbunge (pengine alishindwa kuwarahisishia akina Musukuma), unaweza kudhani unawazidi au kwamba huo ndio uwezo pekee wa profesa. Nakuhakikishia kuwa kazi, shughuli, maandiko na mashauriano yote ya kila siku ya taifa la leo yanafanywa na maprofesa. Hakuna wajinga duniani watakaofikiria mchango wa Musukuma kwenye msimamo rasmi wa serikali kwa jambo lolote la kisasa. Watu wa nje, na wale wa vizazi vijavyo, wakitaka kuelewa jambo sawasawa watasoma aliyoandika profesa, siyo aliyosema Musukuma. Hata wewe
 
Dah Msukuma ana aleji na maporofesa............ mapprofesa Maprosoo
Yeye badala ya kusoma alijilazimisha kuwa "mfumu" na kuchunga ng'ombe... sasa maprosoo wakimla senti zake apatazo kijanjajanja katika biashara zake pindi wamwandikiapo maandiko lazima azidi kuwachukia + wivu...
 
Kwahiyo mwendazake alikuwa na uhakika kuwa hakuna Corona?
 
Maprofesa pia walikudanganya ukaenda kujenga sauna Jimboni kwako kwa ajili ya wananchi wa Jimboni kwako kujikinga na Corona?
 
Msukuma wewe Kila wakati unaponda maprofesa.Kasome bado umli unaruhusu kuliko kuendelea kuwa kituko bungeni.Wabunge wenzako wanakuona Kama laughing stock
 
Bahati nzuri na yeye mwenyewe corona ilimtafuna mapema sn
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…