Muswada huu ukipita na kuwa Sheria Magufuli Day itakuwa Machi 29 kila mwaka na itakuwa siku ya mapumziko

Muswada huu ukipita na kuwa Sheria Magufuli Day itakuwa Machi 29 kila mwaka na itakuwa siku ya mapumziko

Corticopontine

JF-Expert Member
Joined
Sep 20, 2019
Posts
666
Reaction score
1,277
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Dkt. Eliezer Feleshi amewasilisha muswada wa sheria ya marekebisho ya sheria mbalimbali wa mwaka 2023 Bungeni Jijini Dodoma ikiwemo Sheria ya Mazishi ya Viongozi wa Kitaifa, Sura ya 419 ambapo pamoja na mambo mengine marekebisho haya yanakusudia kutoa mamlaka kwa Rais kutangaza tarehe ya maziko ya Rais aliyefariki akiwa madarakani kuwa ni siku ya mapumziko.

“Sehemu ya Tano ya Muswada inapendekeza marekebisho kwenye Sheria ya Mazishi ya Viongozi wa Kitaifa, Sura ya 419 ambapo kifungu cha 6 kinapendekezwa kufutwa na kuandikwa upya kwa lengo la kuboresha masharti kuhusu mamlaka ya Rais kutoa tangazo la kifo cha Kiongozi wa Kitaifa au Kiongozi mahsusi aliye madarakani.

“Marekebisho hayo pia yanampa mamlaka Kiongozi mahsusi aliye madarakani kutoa tangazo la kifo cha Kiongozi mahsusi mstaafu, vilevile marekebisho haya yanakusudia kutoa mamlaka kwa Rais kutangaza tarehe ya maziko ya Rais aliyefariki akiwa madarakani kuwa ni siku ya mapumziko.

“Lengo la mapendekezo haya ni kuweka bayana na kutofautisha mamlaka zinazopaswa kutoa matangazo ya vifo vya Viongozi wa kitaifa na Viongozi mahsusi, vifungu vya 9 na 10 vinapendekezwa kurekebishwa ili kutoa Mamlaka kwa Kiongozi mahsusi aliye madarakani kutoa tangazo la kifo cha Kiongozi mahsusi mstaafu, lengo ni kutambua utaratibu unaotumika sasa ambapo pamoja na kwamba Sheria imemtaja Rais kama mamlaka ya kutoa tangazo la kifo cha Kiongozi mahsusi mstaafu, matangazo ya aina hiyo kwa kawaida yamekuwa yakitolewa na Viongozi mahsusi walio madarakani.”
 
kwa staili hiyo tukifikisha miaka 400 itakua tunatumia mwezi mzima au siku 27 zote kwa mapumziko tunaadhimisha vifo
 
Hii inahusu Marais waliofia Madarakani TU.
Ukifa kama Mstaafu siku ulokufa watu wanapiga kazi kama kawaida
 
Ikiwezekana iadhimishwe Uwanja wa taifa na pia itengewe bajeti ya kutosha kwa maonyesho ya kijeshi nakadhalika ili wananchi waichukulie siriaz
 
Marekani Hadi sasa Ina viongozi wengi waliofia madarakani ila hawana hayo mambo ya ajabu, siku moja inatosha kumbukumbu ya viongozi wote ,tusiendekeze sana uvivu sikukuu kibao taifa maskini
 
Ikiwezekana iadhimishwe Uwanja wa taifa na pia itengewe bajeti ya kutosha kwa maonyesho ya kijeshi nakadhalika ili wananchi waichukulie siriaz
Itakuwa na maslahi gani kwa taifa tuacheni ujinga, single day for our late leader inatosha
 
Wanamashaka na siku aliyo kufa?

Si ibaki ileile walio tangaza?
 
Wakati dunia inapambana na kudorora kwa uchumi tanzania tunazidisha ujinga na upumbavu wa kuongeza siku za kupumzika abadani laana ya ccm ni kuubwa
 
Back
Top Bottom