Muswada wa Bima ya Afya kwa wote wasomwa Bungeni

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Muswada wa Sheria ya Bima ya Afya kwa Wote umewasilishwa bungeni ambapo mwajiri wa sekta ya umma na binafsi rasmi atapaswa kumsajili mwajiriwa katika skimu ya bima ya afya ndani ya siku 30 tangu kuanza kwa mkataba wa ajira.

Muswada huo uliosomwa kwa mara ya kwanza leo, Ijumaa Septemba 23,2022, utakwenda kujadiliwa katika kamati kabla ya kumalizia mchakato mwingine wa utungaji wa sheria.

Pamoja na mambo mengine unatoa masharti ya mwajiri wa sekta ya umma na sekta binafsi kuwasilisha katika skimu asilimia sita ya mshahara wa mwajiriwa, ambapo ndani yake mwajiri atachangia nusu au zaidi ya kiwango hicho, na kiwango kilichosalia kitachangiwa na mwajiriwa.

Aidha, waziri kwa kushauriana na waziri mwenye dhamana ya masuala ya fedha, ataainisha viwango vya uchangiaji kwa ajili ya sekta isiyo rasmi, kama itakavyoainishwa katika kanuni, kwa kuzingatia tathmini ya uhai na uendelevu wa skimu za bima ya afya katika utoaji wa kitita cha mafao ya msingi.

Pia muswada huo unabainisha kuwa waziri, kwa kushirikiana na mamlaka zinazohusika, na kwa kupitia kanuni, ataweka utaratibu na namna ya utambuzi wa watu wasio na uwezo.

Amesema watu watakaotambuliwa kama watu wasio na uwezo watakuwa na haki ya kujumuishwa chini ya skimu ya bima ya afya kwa namna itakayoainishwa kwenye kanuni.

Aidha, Waziri mwenye dhamana ya masuala ya fedha, kwa kushauriana na Waziri, ataainisha vyanzo mahususi kwa ajili ya ugharamiaji wa huduma za bima ya afya kwa watu wasio na uwezo.

Pia amesema iwapo mwanachama anayechangia kupitia makato ya mshahara wake atafariki, wategemezi wake wataendelea kunufaika na huduma kwa kipindi kitakachoinishwa katika kanuni.

“Iwapo mwanachama anachangia kwa utaratibu wa michango kwa mwaka atafariki, wategemezi wake wataendelea kunufaika na huduma kwa kipindi kilichosalia cha mkataba wa uanachama,”amesema.
 
Safi sana ila hiyo Sheria itavunjwa sana.
 
Another TRASH TAKATAKA in the MAKING.

Take it, or Leave it.

NHIF iko hoi, ni TAKATAKA.

iCHF ni MZOGA kabisa unaonuka.

Suluhisho, Wanaamini ni Bima ya Afya kwa WOTE.

Yaani WATU ( Wote ) wachangie halafu hao watu watakaochangia, kwa akili yao WATAKUWA hawaugui MARA KWA MARA wala Kwenda kwenye VITUO VYA AFYA Mara kwa MARA.

Na hivyo, pesa zao walizochangia WATAZICHUKUA na KULIPA MADENI na STAREHE za NHIF ili kunusuru MFUKO.

Nasubiria VILIO na BOMU zito litakalolipuka.
 
Muswada wa Sheria ya Bima ya Afya kwa Wote umewasilishwa bungeni ambapo mwajiri wa sekta ya umma na binafsi rasmi atapaswa kumsajili mwajiriwa katika skimu ya bima ya afya ndani ya siku 30 tangu kuanza kwa mkataba wa ajira.

Muswada huo uliosomwa kwa mara ya kwanza leo, Ijumaa Septemba 23,2022, utakwenda kujadiliwa katika kamati kabla ya kumalizia mchakato mwingine wa utungaji wa sheria.

Pamoja na mambo mengine unatoa masharti ya mwajiri wa sekta ya umma na sekta binafsi kuwasilisha katika skimu asilimia sita ya mshahara wa mwajiriwa, ambapo ndani yake mwajiri atachangia nusu au zaidi ya kiwango hicho, na kiwango kilichosalia kitachangiwa na mwajiriwa.

Aidha, waziri kwa kushauriana na waziri mwenye dhamana ya masuala ya fedha, ataainisha viwango vya uchangiaji kwa ajili ya sekta isiyo rasmi, kama itakavyoainishwa katika kanuni, kwa kuzingatia tathmini ya uhai na uendelevu wa skimu za bima ya afya katika utoaji wa kitita cha mafao ya msingi.

Pia muswada huo unabainisha kuwa waziri, kwa kushirikiana na mamlaka zinazohusika, na kwa kupitia kanuni, ataweka utaratibu na namna ya utambuzi wa watu wasio na uwezo.

Amesema watu watakaotambuliwa kama watu wasio na uwezo watakuwa na haki ya kujumuishwa chini ya skimu ya bima ya afya kwa namna itakayoainishwa kwenye kanuni.

Aidha, Waziri mwenye dhamana ya masuala ya fedha, kwa kushauriana na Waziri, ataainisha vyanzo mahususi kwa ajili ya ugharamiaji wa huduma za bima ya afya kwa watu wasio na uwezo.

Pia amesema iwapo mwanachama anayechangia kupitia makato ya mshahara wake atafariki, wategemezi wake wataendelea kunufaika na huduma kwa kipindi kitakachoinishwa katika kanuni.

“Iwapo mwanachama anachangia kwa utaratibu wa michango kwa mwaka atafariki, wategemezi wake wataendelea kunufaika na huduma kwa kipindi kilichosalia cha mkataba wa uanachama,”amesema.
This is another skunk potentially for the Tanzanians' exploitation under the umbrella of health care improvement
 
Hawa waajiriwa sekta ya umma na binafsi ndiyo wanatakiwa kuwabeba wakulima, wavuvi, wafugaji, machinga, mama-ntilie n.k ? Kwanini wabebeshwe mzigo wa asilimia 70 wanaofanya shughuli zingine binafsi.

Huu mfuko wa bima ya afya lazima utaelemewa labda serikali iseme pia itakuwa inatenga fedha kwenda mfuko huo kwa ajili ya wale wengi amvao siyo waajiriwa ktk serikali na sekta rasmi ya binafsi.
 
Hii bima ya Afya ndio ingegharamiwa kwa tozo sasa.
 
Another TRASH TAKATAKA in the MAKING.

Take it, or Leave it.

NHIF iko hoi, no TAKATAKA.

iCHF in MZOGA kabisa unaonuka.

Suluhisho, Wanaamini no Bima ya Afya kwa WOTE.

Yaani WATU ( Wote ) wachangie halafu hao watu watakaochangia, kwa akili yao WATAKUWA hawaugui MARA KWA MARA wala Kwenda kwenye VITUO VYA AFYA Mara kwa MARA.

Na hivyo, pesa zao walizochangia WATAZICHUKUA na KULIPA MADENI naSTAREHE za NHIF ili kunusuru MFUKO.

Nasubiria VILIO na BOMU zito litakalolipuka.

Lengo zuri but not feasible kwenye nchi husika.
 
Hawa waajiriwa sekta ya umma na binafsi ndiyo wanatakiwa kuwabeba wakulima, wavuvi, wafugaji, machinga, mama-ntilie n.k ? Kwanini wabebeshwe mzigo wa asilimia 70 wanaofanya shughuli zingine binafsi.

Huu mfuko wa bima ya afya lazima utaelemewa labda serikali iseme pia itakuwa inatenga fedha kwenda mfuko huo kwa ajili ya wale wengi amvao siyo waajiriwa ktk serikali na sekta rasmi ya binafsi.
Uwe unasoma kuelewa sio kujibu

Sent from my 220333QAG using JamiiForums mobile app
 
Hii ni mipango ya zimamoto ambayo haina uhalisia. Tujiulize kwanza, kama mipango ya hifadhi ya jamii haifanyi kazi kwa ufanisi hadi leo hiyo bima ya afya kwa wote itafua dafu?

Huu ni mpango utakaoinufaisha Serikali zaidi kuliko mwananchi mwenyewe na hasa mafisafi watakaotokana na nyufa kwenye mpango huu. .... Tujiulize? Ule mpango wa afya kwa wote ifikapo mwaka 2000...Ulifanikiwa?

PHC "Health for all by the year 2000" ilipitia bungeni kwa mbwembwe na sheria ikatungwa pamoja na kanuni zake, Je lengo lilifikiwa? 🤔
 
Muswada wa Sheria ya Bima ya Afya kwa Wote umewasilishwa bungeni ambapo mwajiri wa sekta ya umma na binafsi rasmi atapaswa kumsajili mwajiriwa katika skimu ya bima ya afya ndani ya siku 30 tangu kuanza kwa mkataba wa ajira.

Muswada huo uliosomwa kwa mara ya kwanza leo, Ijumaa Septemba 23,2022, utakwenda kujadiliwa katika kamati kabla ya kumalizia mchakato mwingine wa utungaji wa sheria.

Pamoja na mambo mengine unatoa masharti ya mwajiri wa sekta ya umma na sekta binafsi kuwasilisha katika skimu asilimia sita ya mshahara wa mwajiriwa, ambapo ndani yake mwajiri atachangia nusu au zaidi ya kiwango hicho, na kiwango kilichosalia kitachangiwa na mwajiriwa.

Aidha, waziri kwa kushauriana na waziri mwenye dhamana ya masuala ya fedha, ataainisha viwango vya uchangiaji kwa ajili ya sekta isiyo rasmi, kama itakavyoainishwa katika kanuni, kwa kuzingatia tathmini ya uhai na uendelevu wa skimu za bima ya afya katika utoaji wa kitita cha mafao ya msingi.

Pia muswada huo unabainisha kuwa waziri, kwa kushirikiana na mamlaka zinazohusika, na kwa kupitia kanuni, ataweka utaratibu na namna ya utambuzi wa watu wasio na uwezo.

Amesema watu watakaotambuliwa kama watu wasio na uwezo watakuwa na haki ya kujumuishwa chini ya skimu ya bima ya afya kwa namna itakayoainishwa kwenye kanuni.

Aidha, Waziri mwenye dhamana ya masuala ya fedha, kwa kushauriana na Waziri, ataainisha vyanzo mahususi kwa ajili ya ugharamiaji wa huduma za bima ya afya kwa watu wasio na uwezo.

Pia amesema iwapo mwanachama anayechangia kupitia makato ya mshahara wake atafariki, wategemezi wake wataendelea kunufaika na huduma kwa kipindi kitakachoinishwa katika kanuni.

“Iwapo mwanachama anachangia kwa utaratibu wa michango kwa mwaka atafariki, wategemezi wake wataendelea kunufaika na huduma kwa kipindi kilichosalia cha mkataba wa uanachama,”amesema.

Chanzo: Mwananchi
 
Back
Top Bottom