Muswada wa Marekebisho ya Sheria mbalimbali 2021 wapitishwa

Muswada wa Marekebisho ya Sheria mbalimbali 2021 wapitishwa

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Kamati ya Bunge zima leo imepitisha Muswada wa Marekebisho ya Sheria Mbalimbali wa Mwaka 2021 baada ya kuipitia Ibara kwa Ibara.

Muswada huo unalenga kufanya marekebisho katika Sheria zipatazo Tatu kwa lengo la kuondoa matumizi ya Kiingereza kama Lugha ya Sheria na Mahakama, na badala yake kutumia Kiswahili.

Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson amesema kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania, Muswada huo ambao umepitishwa utaelekea kwa Rais.
 

Attachments

Hivi hili bunge la CCM, halioni mambo ya msingi kurekebisha kwenye sheria za nchi hii zaidi ya kuwa wakalimani. Vipi kuhusu sheria zilizowapa nguvu Wakuu wa wilaya kuweka mtu ndani saa 48? Sheria kibao zina mapungufu lakini wamekaa kimya.

Ujinga na upuuzi mtupu.
 
Mahakama hakuna nchi hii.

Unataka kuniqmbia akina Sugu, Lema, Mbowe na wengineo walikaa gerezani miezi minne kila mmoja kwa uwonevu kwasbb sheria ziko kwa kiingereza??

Kuna tatizo la katiba nchi hii. Huyu msukuma asiyejua chochote leo hii katiba inampa mamlaka ya kuqmua chochote ni hatari.

Somo la historia anaamua yy
Wanyama kupelekwa Chato anaamua yy
Sheria ziwe za kiswahili anaamua yy
Chato kuwa jiji anaamua yy
Kura ziibiwe kwenye mabegi anaamua yy
Chanjo ya korona isije nchini anaamua yy
N.k

Kuna tatizo!!!
 
Hivi hili bunge la CCM, halioni mambo ya msingi kurekebisha kwenye sheria za nchi hii zaidi ya kuwa wakalimani. Vipi kuhusu sheria zilizowapa nguvu Wakuu wa wilaya kuweka mtu ndani saa 48?? Sheria kibao zina mapungufu lakini wamekaa kimya.
Ujinga na upuuzi mtupu.

Hakuna ujinga kwenye nchi kama sheria kutungwa ili kukidhi utashi wa kiongozi aliye madarakani.
 
Hivi hili bunge la CCM, halioni mambo ya msingi kurekebisha kwenye sheria za nchi hii zaidi ya kuwa wakalimani. Vipi kuhusu sheria zilizowapa nguvu Wakuu wa wilaya kuweka mtu ndani saa 48?? Sheria kibao zina mapungufu lakini wamekaa kimya.
Ujinga na upuuzi mtupu.
Hizi zikirekebishwa zitawaondolea nguvu ya kuminya upinzani.
 
Viongozi wanatafuta historia isiyo na sababu.

If you don't know English language,learn it,but not to brush your ignorance.Je,Kuna tatizo kubwa lililoonekana kutokana na majaji na mahakimu kutumia lugha ya kiingereza wakati wa kesi?

"The intelligence of the ruler can be estimated by looking at the people he has around him" . ( Niccolo Machievelli).
 
Kwenye hili tumejikomboa, vya kurithi sasa, bado mitaala ya elimu na Katiba

Ni wakati sasa wa kutumia kila mizimu ya wazungu, tunataka Uhuru kamili
 
Mahakama hakuna nchi hii.

Unataka kuniqmbia akina Sugu, Lema, Mbowe na wengineo walikaa gerezani miezi minne kila mmoja kwa uwonevu kwasbb sheria ziko kwa kiingereza?
Sio hayo tu ata sheria inayohusu uhuru wa kujielezea kwenye katiba umeminywa haswa kwa wandishi wa habari.

Access to information inasema kila mtu ana haki ya kukusanya taarifa na kukaa nazo vilevile kutoa maoni binafsi bila kuingiliwa.

Media service act inasema una mipaka ya kukusanya taarifa

Ukiend kwenye policy ile ya mwaka 2003 inasema unasema serikali aiingilian na vyombo ya habari vya umma ila swali linakuja je hayo yanatendeka kiuhalisia?

Hakuna haki yoyote katika taarifa kam mwananchi kwa ujumla
 
Viongozi wanatafuta historia isiyo na sababu.
If you don't know English language,learn it,but not to brush your ignorance.Je,Kuna tatizo kubwa lililoonekana kutokana na majaji na mahakimu kutumia lugha ya kiingereza wakati wa kesi????
"The intelligence of the ruler can be estimated by looking at the people he has around him" . ( Niccolo Machievelli).
"Kill him not, live him free"- jaji
Alie quot "kill him, not live him free"


Hapo maisha ya mtu yakaenda kisa utopolo
 
Back
Top Bottom