Katiba ni chombo muhimu kwa mustakabli wa chi yeyote. hata hivyo Wananchi wa Tanzania walio wengi hawaelewi nini umuhimu wa katiba. Juzi nilikuwa naangalia mjadala uliokuwa unaendeshwa katika Televisheni moja hapa nchini, nikakumbana na kioja kilichotokana na mchangiaji na hapa ninamnukuu, .............. tusije tukajdili katika na watu ambao wakati katiba hii inatekelezwa hawatakuwapo....... mwisho wa kunukuu, kwa mujibu wa mchangiaji huyo watu ambao hawatakuwepo wakati katiba inafanya kazi ni wazee kwa sababu watakuwa wamekufa. Nilimshangaa sana tene alikuwa anasema maneno haya mchana kweupe bila soni. amesahau kuwa wazee hawana satari nyingine ya kwenda kuishi iwapo katiba itatekelezwa wakati bado wanaishi. maana ya kuchangia hivi ninaona kuna umuhimu wa watanzania kufahamu kuwa kila kundi la kijamii lina mahitaji muhimu kama kundi na mahitaji hayo yanastahili kuangaliwa kwa mapana yake na katiba ya nchi yetu. Iwapo hatutakuwa makini tunaweza kuwaachia kundi moja likahodhi haki ya kujadili katiba na kwa vyovyote vile kama ilivyo kwa mwamba ngoma maslahi makubwa yatakayo kuwa addressed na katika hiyo yata focus kundi hilo. ninawasihi watanzajia wote wasikae chini wakadhani walioko katika kundi fulani watawasemea wasomi watatetea maslahi ya wasomi, wakulima watatetea masliahi ya wakulima hivyo hivyo kwa wakulima na wafugaji na vikundi vya dini , na walemavu na .....na.......
Mheshiwa Serukamba jana kwa kuwa yeye ni msomi alichangia bungeni wakati wanajadili bajeti ya wizara ya Ardhi nyumba na maendeleo ya makazi kwa kurudia mara kadhaa wasomi wakitoka vyuoni wakute nyumba nyingi zipo.Mheshimiwa huyu hata mara moja hakusema tuangalie utaratibu wa kuwakopesha wakulima vifaa ili waweze kujenga nyumba bora na ili waweze kupata makazi mazuri. mwamba ngoma huvutia kwake huu ni mfano mmoja kati ya mingi. Haya shime Watanzania kila kundi lisilale wakati wa mchakato wa katiba kwani ni muhimu kwa mustakbali wa nchi hii.