Muswada wa Sheria ya Mapitio ya Katiba: Download na pitia uone kilichomo na usambaze

Muswada wa Sheria ya Mapitio ya Katiba: Download na pitia uone kilichomo na usambaze

Katiba ni chombo muhimu kwa mustakabli wa chi yeyote. hata hivyo Wananchi wa Tanzania walio wengi hawaelewi nini umuhimu wa katiba. Juzi nilikuwa naangalia mjadala uliokuwa unaendeshwa katika Televisheni moja hapa nchini, nikakumbana na kioja kilichotokana na mchangiaji na hapa ninamnukuu, .............. tusije tukajdili katika na watu ambao wakati katiba hii inatekelezwa hawatakuwapo....... mwisho wa kunukuu, kwa mujibu wa mchangiaji huyo watu ambao hawatakuwepo wakati katiba inafanya kazi ni wazee kwa sababu watakuwa wamekufa. Nilimshangaa sana tene alikuwa anasema maneno haya mchana kweupe bila soni. amesahau kuwa wazee hawana satari nyingine ya kwenda kuishi iwapo katiba itatekelezwa wakati bado wanaishi. maana ya kuchangia hivi ninaona kuna umuhimu wa watanzania kufahamu kuwa kila kundi la kijamii lina mahitaji muhimu kama kundi na mahitaji hayo yanastahili kuangaliwa kwa mapana yake na katiba ya nchi yetu. Iwapo hatutakuwa makini tunaweza kuwaachia kundi moja likahodhi haki ya kujadili katiba na kwa vyovyote vile kama ilivyo kwa mwamba ngoma maslahi makubwa yatakayo kuwa addressed na katika hiyo yata focus kundi hilo. ninawasihi watanzajia wote wasikae chini wakadhani walioko katika kundi fulani watawasemea wasomi watatetea maslahi ya wasomi, wakulima watatetea masliahi ya wakulima hivyo hivyo kwa wakulima na wafugaji na vikundi vya dini , na walemavu na .....na.......
Mheshiwa Serukamba jana kwa kuwa yeye ni msomi alichangia bungeni wakati wanajadili bajeti ya wizara ya Ardhi nyumba na maendeleo ya makazi kwa kurudia mara kadhaa wasomi wakitoka vyuoni wakute nyumba nyingi zipo.Mheshimiwa huyu hata mara moja hakusema tuangalie utaratibu wa kuwakopesha wakulima vifaa ili waweze kujenga nyumba bora na ili waweze kupata makazi mazuri. mwamba ngoma huvutia kwake huu ni mfano mmoja kati ya mingi. Haya shime Watanzania kila kundi lisilale wakati wa mchakato wa katiba kwani ni muhimu kwa mustakbali wa nchi hii.
 
Kwa wale wanaouliza kwanini wajumbe wawe sawa kutoka Zanzibar na Tanganyika, hio mbona iko logic kabisa.Mwauliza leo kama mbona kule watu wake ni kidogo, hamkujua hivyo siku ile babu yenu Nyerere alipopeleka majeshi kupinduwa ?

Safari hii wapemba tumechachamaa huku, huyo babu yenu Sitta Samueli akae sawa mara anapigwa makofi:thinking:
 
Katika suala zima la KUANDIKWA UPYA KWA KATIBA CHINI YA USIMAMIZI WA WANANCHI WENYEWE, ni vema CCM kikatahadharishwa ya kwamba chelea chelea hizi watu msijelaumu nafsi zenu baadaye pindi mtakapogundua mwana si wenu tena.

Tahadhari siku zote zaweza kuchukuliwa na hata kudharauliwa vile vile.
 
aisee wana jf - nawasalim ktk jina kuu la bwana yesu na kusema nimerudi tena in full swing. Before i continue nasema ule mwanamke wasiri kommbani afae kabisa - watanzania tusikubali kupelekwa tuu kama bumbuwazi ni lazima sisi we have to decide for the constitution and not them deciding for us.

Hongera mzee warioba uwamabia ukweli. They think they can brain washed us by doing and deciding everything for us ---- hapana. Kwanza rais anatakiwa kwa rais tuu ---- rais atakiwe decision maker for kila uhamuzi ya watanzania. Tunakata na lazima avue jukumu nyingi ambae anazo. Wasitunge sheria yakuwafaidi ---- tunakata.
 
jamani wana jf kuna nakala ya muswada kwa kkiswahili , mbona siuoni kwenye link hapa. msaada tafadhali.
 
Blessing samahani hapa ama ulikuwa unaandika kwa haraka? hujui vizuri kiswahili? na kiingereza pia kinasumbua, au ni vipi?
aisee wana jf - nawasalim ktk jina kuu la bwana yesu na kusema nimerudi tena in full swing. Before i continue nasema ule mwanamke wasiri kommbani afae kabisa - watanzania tusikubali kupelekwa tuu kama bumbuwazi ni lazima sisi we have to decide for the constitution and not them deciding for us.

Hongera mzee warioba uwamabia ukweli. They think they can brain washed us by doing and deciding everything for us ---- hapana. Kwanza rais anatakiwa kwa rais tuu ---- rais atakiwe decision maker for kila uhamuzi ya watanzania. Tunakata na lazima avue jukumu nyingi ambae anazo. Wasitunge sheria yakuwafaidi ---- tunakata.
 
je n kwel wanaopigania kuhusishwa kwa watanzania katika kujadili katiba mpya wanapigania watanzania kuhusishwa kwel? Au tunatumia kivuli cha watanzania kutaka kupitisha matakwa yetu?
 
kwa maoni yangu wanaopigania watanzia kuhusishwa katika majadiliano hayo wangeanza kutufundisha watanzania kwanza katiba yenyewe n nn tufahamu katiba tulio nayo tukisha ijua basi tutajua mapungufu yake alafu ndo tutakua na uwezo wa kuamua nn hatukitaki na kipi kiongezwe maana tutakua tunavijua vilivyomo maana yangu n kwamba wimbi kubwa la watanzania wapo vijijini hawaijui hata hiyo katiba ya zaman ambayo mnawaambia n mbayya kwao mnajuaje kama kwao n mbaya hamuoni pia mme waamulia hata kwa hilo pia? N vema mkawapa elimu kwanza alafu wenyew waone kama hiyo katiba haiwafai na n nn wanataka kibadilishwe na co kusema wanainchi wanataka mabadiliko ya kitu ambacho hawakijui.
 
kweli watanzania, hatujui lililomo kwenye katiba yetu.....
 
:crazy:Katiba hii emeegemea upande mmoja tu si kwa manufaa ya wananchi na umma kwa ujumla bali CHAMA na kwa mfumo huo Tanzania itaendela kulalama kuwa inchi maskini hadi kiama .
 
cha ajabu zaidi ni kwamba mswaada hauna future plan kama wao wazaniavyo,one thing si kweli wao watatawala mda wote au milele manake basi badaye watapata taabu kwa mambo walioyatengeneza wenyewe note hawa waliopo watakuwa hawapo hivyo basi vijana tuangalie katiba mpya kama muhstabali wa maisha yetu yajayo hawa wazee wao wanataka kuficha maovu yao kwa mda huu tusishangilie kwa itikadi za kisias tuu bali tuangalie tuendako.
ni kweli ipo siku hii nchi itashikwa na kichaa tukaja kujuta kwa mambo ambayo tunayashangilia sasa
Tanzania amka vijana amka ni hayo tuu
 
Katiba mpya katika Tanzania ni chombo kinachohiajika sana ili Mtanzania halisi aweze kufaidika na Vyote vinavyomuhusu kama Mtanzania, kuanzai kufaidika na rasilmali na uhuru wa kuishi popote atakapo Tanzania.Katiba tuliyokuwa nayo tangu Uhuru Mwaka 1961 Ni katiba iliyotungwa na Makaburu ili kuwawezesha kuendeleza utawala wao kwa urahisi bila kutumia nguvu kama wakati wa ukoloni.Ni dhairi kwamba mabadiliko katika Katiba yamekuwepo kwa sheria mpya kupitishwa katika vikao vya bunge na hivyo basi katiba tuliyonayo sasa si sawa kiukamilifu na ile ya mwaka 1961.Kila mara kipengele kinapobadilishwa au kuongezwa basi katiba inakuwa mpya.
Mswada wa kubadilisha katiba yote kwa mara moja kwa kweli ni ulaghai na wizi mtupu kwani ni jambo ambalo kamwe halitawezekana.Watanzania wanapaswa kukaa chini na kuchunguza haswa ni vipengele gani vinavyopaswa kubadilishwa kwa haraki na kuhakikisha kwamba bunge linawajibika kufanya kazi hiyo kwa kushughulikia vile vipengele vilivyo vya msingi kwanza na katika muda mwafaka katiba inaweza kubadilika kwa maslahi yetu wote.
Kubailishwa kwa katiba nzima kutahitaji Pesa nyingi za walipa kodi na kama tunavyoshuhudia kutooka nchi zinginezo zilizochukua jukumu hilo,mwisho wake ni kuchanganyikiwa kwa wananchi wote na viongozi haswa kunapofikia wakati wa kutekeleza mabadiliko hayo.Nchi ya Kenya ni mfano mzuri wa waliochanganyikiwa baada ya kutumia pesa nyingi katika mchakato mzima wa kubadilisha katiba bila mafanikio.Nchi nyingi za Afrika zimembadilisha katiba mara kwa mara zaidi tu kufanya maisha ya wananchi wao kuwa kushneyh zaidi.
Katiba "mpya" ni muhimu haswa kufanikisha muungano wetu wa Afrika Mashariki.Aidha tusikubali kucheza ngoma tusiyoijua kwa kupitisha katiba tusiyoijua kwani ni mwanya wa Mabepari watakaofadhili sehemu ya mabadiliko haya kuweka vipengele vitakavyotukwaza hapo baadaye.Wengi watakaopigia kura katiba mpya ni wanachi wenye upeo mdogo na wengine wasiojua hata kusoma licha ya kuwa na uezo wa kutafsiri katiba yenyewe...Mchakato mzima wa kutaka katiba mpya kwa mara moja ni kuhujumu haki ya Watanzania na kunapaswa kuwa na subira kufanya mabadiliko kwa wakati unaofaa na kuepuka kutumia kodi tunazochanga kiholelaholela...
Haya sasa, ngoma hiyo...cheza ujuavyo
 
kaka Filipo naomba unisaidie kitu hapa naitaji KITABU CHA KATIBA YA ZAMANI kama uanacho cha kiswahili kwani hichi nilichonacho ni cha kizungu kinanizingua sana pls nikupate wapi ili nije kuchukua naamaanisha tafadhali pls
 
Last edited by a moderator:
ni kama ulikuwepo ndugu yangu watanzania wengi hawajui kilichopo katika katiba ya zamani ndo maana wanashindwa hata kuleta maoni yenye maana katika katiba hii mpya inayoandaliwa tumekuwa mbumbumbu mzungu wa reli sijui itakuwaje ni wachache sana tu ndo wanaotambua na kujua yaliyomo katika katiba ya nyuma hapo nakupa bigup mkuu htc
 
Last edited by a moderator:
kwani wewe hujui kizungu waambie wanakamati watudadavulie kwa kiswahili humu ndani usione aibu kwanza mm nawashangaa sana hawa wajumbe wa baraza la kamati ya katiba mpya kwani Tanzania ni watumiaji wa lugha ya kizungu mpaka watumie lugha hiyo katika muswada jamani eti Maxence Melo tusaidie kwa hapa tuletee link ya kiswahili ya muswada
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom