Nimejitahidi kuyatafsiri hayo uliyoyanukuu kwa kiingereza, pengine yatatusaidia kufahamu zaidi kwa lugha yetu ya Taifa ya kiswahili. Nairudia ya Kiingereza na Tafsiri yake ipo chini hapo ni kama ifuatavyo:
(2) In the implementation of subsection (1), the Commission shall adhere to national values and ethos and shall, in that respect, observe inviolability and sanctity of the following matters:
(2) Katika utekelezaji wa kifungu kidogo cha kwanza (1), Tume itakuwa ikizingatia imani, maadili na itikadi ya taifa, na kwa matilaba hayo, itahakikisha inaheshimu kutokuwepo utenguaji na utakatifu wa mambo yafuatayo:
(a) the Union of Tanganyika and Zanzibar;
(a) Muungano wa Tanganyika na Zanzibar;
(b) the existence of the Executive, Legislature and the Judicature;
(b) kuwepo wa Serikali, Bunge na Mahkama;
(c) the Presidency;
(c) Urais (inakusudiwa Raisi na madaraka ya Uraisi)
(d) the existence of the Revolutionary Government of Zanzibar;
(d) kuwepo kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar;
(e) national unity cohesion and peace;
(e) mshikamano wa umoja wa kitaifa na amani;
(f) periodic democratic election based on universal suffrage:
(f) uchaguzi wa kidemokrasia kwa kuzingatia dhima ya Haki ya lazima ya upigaji kura kwa mwanadamu:
(g) the promotion and protection of human rights;
(g) ya kuendeleza na kulinda haki za binadamu;
(h) human dignity, equality before the law and due process of law;
(h) utu, usawa mbele ya sheria na taratibu zote za haki za Kisheria;
(i) the secular nature of the United Republic; and
(i) kutofungamana na udini kwa Jamhuri ya Muungano, na
(j) the independence of the Judiciary.
(j) uhuru wa Mahakama.
Suala kubwa hapa kutojadiliwa na kutenguliwa muungano wenyewe kama kifungu (a) kinavyotaka kwahiyo majadiliano hayo ya katiba yatatufikisha wapiiiii? Jee katika mjadala wa katiba tukagundua muungano hautufai, si watatubana hawa kwa hadidu rejea za makubaliano juu ya mjadala wa katiba utavyoendeshwaa? Kwahiyo ni sawa sawa kwa WaZanzibari kukaa na msimamo wa kukataa kujadili muungano kwa masharti kama haya.
Ati muungano usijadiliwe hadi kutenguliwa kwa utakatifu wake. Hivi muungano huu wa kijizi jizi una utakatifu gani? Labda kwa Tanganyika lakini sio kwa Wazanzibari.amahani hapa wasomaji kwa jazba. Inaudhi sana mara nyengine kusoma maandiko yao hawa wataalamu wa Janjanyika. Labda wawaeleze wadanganyika tu.
Au kifungu (c) kinachosema Uraisi hivi Uraisi na hasa huu wa Kitanzania una ukamilifu gani na utakatifu gani hata uwe usiguswe katika kujadiliwa katiba?
Kifungu (d) kuwepo kwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. Jee tukiamuwa sio Serikali ya Mapinduzi tena badala yake ni Serikali ya Zanzibar tu, na hilo iwe tumeliamuwa sisi wenyewe WaZanzibari wenyewe tutakuwa hatuna haki? Pengo la fikra hilo katika utungaji wao.
Kwa vifungu e,f,g, h, na i utaona wameyaandika maelezo vizuri sana. Lakini uzowefu wetu wa miaka 47 unatuonesha hakuna hata moja katika haya wanaloliheshimu sawa sawa kama inavyotakikana hasa kwa upande wa Zanzibar. Sasa sijui utukufu wake upi huo tuulinde katika kuijadili Tanzania na mambo hayo. Chaguzi sio za kidemokrasia na za uwazi kama inavyotakiwa ni wizi wa kura tu na vurugu. Amani na utulivu na umoja ndio unazidi kuyoyoma kila siku zikienda. Huko Tanganyika ndio hawatambuani na udini. Sisi Zanzibar wamejitahidi kutuletea fitna za umajimbo, tushukuru Mungu tumeamka sasa. Ni wao Tanganyika ndio wakipalilia tafauti za Wazanzibari. Sasa sijui wana utukufu gani katika hili la kuwa waheshimike.
Tanzania hakuna utu kwa kiwango cha kusifiwa duniani. Ujambazi uliotopea na Polisi ndio washiriki wakubwa, Mazeruzeru wanauliwa ovyo ovyo n.k n.k. Sasa heshima ya utu na haki za binaadamu hizo zenye utukufu ziko wapi za kulindwa?
Tanzania tunaambiwa nchi haina dini. Nenda Tanganyika utizame Udini unavyoingizwa kwenye mambo ya Serikali dhahiri dhahiri. Ati uhuru wa Mahkama. Hivi kweli Mahkama ziko huru kama inavyotakiwa?
Sasa inaposemwa katika kujadili katiba tuhakikishe kutotengua na kuucha utukufu uliopo, ni utukufu upi na lipi ambalo tusilitengue kutokana na uzuri wake. Yote yanatengulika na kufanywa upya kutokana na uoza uliopo.
Nawakilisha hoja
SOSI: MZALENDO.NET