Muswada wa Sheria ya Mapitio ya Katiba: Download na pitia uone kilichomo na usambaze

Muswada wa Sheria ya Mapitio ya Katiba: Download na pitia uone kilichomo na usambaze

Watanzania tuwe makini sana maana vitu vingine sio kuingia kichwa kichwa. naupita itarudi
 
Watanzania tuwe makini sana maana vitu vingine sio kuingia kichwa kichwa. naupita itarudi
unajua mimi sina tatizo kubwa sana na katiba iliyopo kama JK angekuwa rais mwenye uwezo mkubwa wa kuongoza.. Katiba iliyopo inampa mamlaka makubwa sana ya kushughulikia matatizo sugu ya nchi yetu kama vile Ukiritimba, urasimu na kwa ujumla wake Ufisadi..

Katika hali tuliyofikia Tanzania bado inahitaji rais dikteta na katiba yenye kumpa mamlaka makubwa kupiga vita umaskini wa nchi hii ambao ni wa kujitakia na nitasema ukweli daima kwamba katiba mpya haiwezi kuondoa tatizo la umaskini tulonao isipokuwa katiba mpya inahitajika zaidi kisiasa kwani hadi leo hii hatuna mfumo wa vyama vingi isipokuwa tupo ktk haarakati hizo na katiba yetu ndio kikwazo..

Niaminivyo mimi katiba haiwezi kuwa tiba ya matatizo yetu kiuchumi sawa na kusema kubadilisha au kutengeneza Biblia au Kuran mpya hakuwezi kuondoa au kupunguza madhambi ya waumini waliokusudia kutofuata misingi ya imani hizo..
Isipokuwa kama swala ni kukomesha kabisa maasi hayo ni sheria kuchukua nafasi kubwa ya kusimamia maadili ya imani husika..
Na ndio maana Waislaam hudai sheria law kuwa kipimo cha haki kwa waumini wake kufuata mwongozo wa dini yao.
Sasa Tanzania kikatiba tunalaani rushwa na kusema sintatoa wala kupokea rushwa lakini ukweli ni kwamba -Rushwa ndio inatawala maisha yetu.

Kwa hiyo kinachotakiwa zaidi kwetu wananchi ambao tunapigika kila siku na maisha magumu wakati rasilimali na maliasili zetu zikichukuliwa kwa nguvu ya mfumo dume unaowapa nguvu zoote chama tawala..Tunahitaji Rais - KIONGOZI mwenye uwezo wa kuongoza na sii Mtawala wala fisadi
kwanza.
Na kama hawezi kupatikana chini ya mfumo wa katiba iliyopo basi mkazo mkubwa uwekwe kumbana rais, CCM na viongozi wanaopewa madaraka kuwa waajiriwa wa wananchi na sii Watawala wa wananchi..

Tatizo kubwa la nchi yetu sii tu mamlaka ya JK au rais isipokuwa nguvu kubwa inayoshikwa na chama tawala kiasi kwamba vyama vingine vinaonekana kuwa ni matawi ya chama hicho..

Katibu mkuu wa CCM ana nguvu kuliko hata mawaziri na hata wale wa mikoa na majimbo wana nguvu kuliko wabunge au hata mkuu wa mkoa..

Sasa kwa kuutazama muswada ulowakilishwa bungeni, binafsi pamoja na kutokuwa mwanasheria au kusomea sheria bado natambua kwamba rais JK bado ana haki zote kikatiba kuteua tume kwa sababu bado ana nguvu zake zote kikatiba..

Malalamishi mengi nayoyaona ni kama vile tayari JK kisha vuliwa mamlaka alokabidhiwa kikatiba na kuyarudisha au kukabidhiwa bunge.. Utata huu wengi wenu mnashindwa kuelewa kwamba JK bado ana mamlaka yote chini ya katiba hii, isipokuwa yeye ndio dhaifu na kashindwa kuongoza, hivyo hata hizi kelele za katiba mpya ni kutokana na udhaifu wake kiutawala.

Tungekuwa na mtu kama Kagame sidhani wananchi wangeitaka katiba mpya sasa hivi kwani Ufisadi wa nchi za kiafrika hauwezi kuondolewa pasipo kiongozi dikteta na mshenzi kuwakabiri washenzi..

Halafu pia kuna utata mkubwa kwa Wazanzibar ambao nao hawalitambui bunge la Muungano isipokuwa bunge la Zanzibar pamoja na kuwa na wawakilishi wa kila jimbo visiwani ktk bunge la Muungano..yaani Wazanzibar wanalichukulia bunge la muungano kama ni bunge la Bara na hata rais wa Jamhuri kwao ni kiongozi wa bara labda awe Mzanzibar..

Ni Fikra finyu kabisa lakini ndio reality ya Wazanzibar na bado swala la Uislaam na Ukristu, wanawake na wanaume na kadhalika..Haya ndio husema muhimu sana kutazama WATU na MAZINGIRA.....

Hivyo kwa mtu kama mimi ambaye nimekaa nje ya kabati la fikra, kutofungwa na ushabiki naliona tatizo la Katiba ni kubwa kuliko wengi mnavyofikiria na kibaya zaidi JK ni rais weak vibaya sana ambaye ndio sababu kubwa ya matatizo mengi mnayoyaona kuwa haki yenu leo ingawaje yalikuwepo toka enzi za mwalimu....
Muungwana wa kiswahili hata siku moja hawezi kuongoza WATU - Watanzania ktk MAZINGIRA haya hata kidogo..
 
twafwa jamaa ndo wameshika mpini.... Kunyongw ndo imesashindikana na watoto wao wanaenjoy free political ride...... Tutaloloma wenzetu wanabuunyaaa

Kwenye hivi vita vya haki hatutaki waoga kama ninyi. Sisi tumedhamiria na kwakua tuna dhamira njema tunashindi kabla ya vita kuisha. Hakuna kurudi nyuma wala kukata tamaa tuko mbele kwa mbele kulikomboa taifa letu dhidi ya mabeberu weusi. Wawe wameshika mpini ama makali it doesn't matter what matters is our decision to say enough is enough and come what may! Hata makali nayo yanasehemu ya kukata na sehemu nyingine hushindwa!
 
Wadau, tumeshaona dalili mbaya za tunakopelekwa kuhusu hatima ya Muswada wa Katiba. Tusipokuwa makini na huenda ndicho kitakachotokea, Wabunge hasa wa CCM kwa kutumia wingi wao watapitisha Muswada huo mbovu! Huwezi amini watu na akili zao wanashindwa kuona mapungufu makubwa ktk Muswada huo? Simply, wameweka maslahi yao mbele na si ya taifa. Kilio cha wengi ni sauti ya Mungu! Muswada usipitishwe na ukaandikwe upya kunusuru damu za Watanzania walio wengi na raslimali zao zinazofujwa na wachache!

Watanzania tuamke!!!!
 
Tanzania itajengwa na wenye moyo..........:mmph:
 
Kwenye hivi vita vya haki hatutaki waoga kama ninyi. Sisi tumedhamiria na kwakua tuna dhamira njema tunashindi kabla ya vita kuisha. Hakuna kurudi nyuma wala kukata tamaa tuko mbele kwa mbele kulikomboa taifa letu dhidi ya mabeberu weusi. Wawe wameshika mpini ama makali it doesn't matter what matters is our decision to say enough is enough and come what may! Hata makali nayo yanasehemu ya kukata na sehemu nyingine hushindwa!
mkuu nadhani hujaelewa hoja zetu... Sii swala la woga ila ni swala la kutambua mbinu chafu za CCM na uwezekano wa kupata katiba mpya kwa sabau wewe na wengineo mnaweka imani ktk kitu kisichowezekana au kutokuwepo akilini mwa Utawala uliopo madarakani.. CCM hawawezi kukupa Katiba mpya iwanyonge - haiwezekani...

CCM haiwezi kuwapa katiba mnayoitaka na watacheza kiduku na nyie hadi muijue ngoma yao hivyo kutahadhari ni kitu muhimu zaidi unapojipanga upya kupinga muswada uliopo laa sivyo mtapoteza muda na blaa blaa nyingi huku miaka ikiyoyoma..
 
Hata kama tungekuwa na mtu (kiongozi) kama Kagame bado tungetaka Katiba Mpya kwa huko baadaye tutakapopata kiongozi ambaye si kama Kagame. Bado Mungu anatusaidia maana hapo tukichelewa na tukampata dikteta mbaya tutakuwa tumechelewa maana sharti watu wamwage damu ili kupata mabadiliko ya Katiba. Wakati ni huu kuondoa utata hapo baadaye. Anachodhamiria Rais si tofauti na wananchi kasoro mchakato wake na hapo tukubaliane na wananchi, tatizo nini ambach hakisemwi wazi?
 
Utapeli sasa unajidhihirisha Tanzania. Tusiruhusu watupite kama vipofu.

"If we must die, let it not be like hogs
Hunted and penned in an unglorious spot ..."
 
Wanajf,
Huu muswada unaendeleza mtindo wa kizungu. Hautoi fursa sawa kwa wote. Naamini hata hapa jf sio wote watakaouelewa kwa sababu nchi ni ya waswahili lakini lugha ya muswada ni ya kimombo. Huu ni utumwa na inaonesha sio viongozi tu wa nchi hii, bali hata wasomi wa nchi hii ni watumwa wa utumwa na tunaendelea kujiweka chini ya utumwa maana tunajifanya tunajua sana kiingereza ikiwa na maana tumeasahau wale wasiojua kiingereza katika nchi hii.

Hitimisho. Muswada huu haukidhi wakati tulionaoa na unamalengo ya kuendeleza utawala wa kinyonyaji na mabavyu tuliridhi kutoka kwa wakoloni na ndio maana hata lugha iliyotumika inaeleweka tu kwa waingereza wa kitanzania.
 
JK na CCM yake wanafanya mzaha kwenye jambo la msingi kiasi hiki? Wamekosa aibu mpaka wanaleta usanii kwenye mkataba wa wananchi na serikali yao.

Tunaomba Chama chenye uchungu na nchi hii, Mtuonyeshe Tahrir Square ya kila Mkoa tuanze mapambano. Nguvu ya Umma iwavamie kama Tsunami ya Japan.
 
utaratibu wa kuunda katiba ni rahisi sana,

1. serikali iitishe mkutano mkuu wa kitaifa wa makundi yote ya kijamii
2. makundi ya kijamii yaunde tume ya kukusanya maoni
3. tume iandae hadiju za rejea halafu mkutano mkuu wa kitaifa uzipitishe au la.
4.Tume ya katiba ikusanye maoni nchi nzima kulingana na hadiju za rejea.
5. tume ikimaliza kukusanya maoni iyapitie na kuandaa majumuisho.
6. mapendekezo hayo yapelekwe kwenye bunge maalum la katiba kwa ajili
ya kuidhinishwa tu kwani hawana uhalali wa kupindisha maoni ya wananchi
kwani wao ni watumishi tu.
7. baada ya kutoka bungeni yatarudishwa kwa wananchi kwa ajili ya kupigiwa
kura ya maoni (referendum) na wananchi wote na kama yakipita basi katiba
inakuwa halali kwa maana imetokana na wananchi wenyewe.

kinyume na hapa serikali itakuwa inajitakia matatizo yasiyo na msingi kwani wananchi wamechoka kuburuzwa kwani tusingependa kilichotokea nchi zingine kitokee hapa.

1.Makundi ya kijamii?...hapo mpaka makabila yatataka kuwakilishwa,lipi ni kundi la kijamii na lipi sio?
2.Eeh! makundi yaunde tume?...ya watu wangapi?Hebu tupe composition ya hiyo tume with regards to makundi.
3.Hadidu za rejea zipitishwe na mkutano mkuu wa kitaifa?...wajumbe watakuwa kina nani?
4.Poa!..hiyo tume ataichagua nani?Kama bunge mmeliwa pia!
5.okay!
6.Kwa hiyo kwanini tupeleke kwenye hilo bunge tukijua fika hawatasema hapana?
7.Okay!
 
JK na CCM yake wanafanya mzaha kwenye jambo la msingi kiasi hiki? Wamekosa aibu mpaka wanaleta usanii kwenye mkataba wa wananchi na serikali yao.

Tunaomba Chama chenye uchungu na nchi hii, Mtuonyeshe Tahrir Square ya kila Mkoa tuanze mapambano. Nguvu ya Umma iwavamie kama Tsunami ya Japan.
Ndg yangu Anko Sam Huyu jamaa President anajua fika nguvu ya huo mswada mpya wa katiba. Anajua hao ndugu zake mafisadi wataumbuka!! Katiba mpya itakuwa na kila kitu; Human wrights bills,ant corruption bills, an independent elector commission, free and independent judicially commission, independent law enforcing firms, transparency and integrity commission. So vitu vyote hivyo vikiwekwa kazini na katiba, mafisadi wote kazi kwisha.
Huyo Mheshimiwa Raisi anajua yote hayo, ndiyo maana ana hijack hiyo Agenda ili afanye atakavyo yeye!!!!!!
Ebu fikiria huyu mtu kapewa kazi na wananchi pale Magogoni ili asimamie utawala wa nchi ya Tanzania, kupitia katiba. Ambayo watawaliwa wa Tanzania wameikataa kuwa haifai tunahitaji katiba mpya yenye maslahi kwa taifa letu; Sasa huyu Bwn anakurupuka na mfano wa katiba eti ijadiliwe bungeni ipitishwe kwa wananchi, kwa muda mfupi ambao haumpi mwananchi kufikiri na kutafakari iwe katiba ya namna gani??????
Najua hapa JF kuna watu wa utawala wanafutilia maoni ya wadau wa JF kuhusu maandlizi ya katiba mpya; Kwa maoni yangu muda huu Mheshimiwa Raisi atulie awaachie wadau wataalamu wa katiba walio huru na mashirika mbali mbali tena wawe na muda wa kutosha; maana KATIBA NI YA KUDUMU, si ya SISIEM wala CDM au serikali iliyoko madarakani (Vyote hivi vinapita tena kwa kasi) ni YA WATANZANIA WOTE HATA WALE AMBAO HAWAJAZALIWA!!!!!!!
Hivyo unapoandaa mchakato wa katiba mpya fikiria future ya Tanzania, si kwa wakati huu peke yake bali mpaka baadae unataka Tanzania ya namna gani???????? Tilia maanani matokeo ya Misri, Libya, Yemen, Somalia na kwingineko kwenye vurugu; maana viongozi hawakuwasikiliza wananchi, hivyo wananchi wakadai haki zao kwa nguvu. Serikali si kazi yake kupanga namna ya kutawala Watanzania, bali wananchi ndio wapange kwa ridhaa yao ni namna gani serikali inayo pewa nchi itatawala nchi yetu;
Bila rushwa, wizi, dhuruma, uonevu, unyanganyi, ufisadi na ubabe.
Serikali na bunge lake la Anna Makinda na vyombo vyake vya dola na unpredictable judicially system yake (Ambayo inapita;Think Man.) itulie wananchi na wadau mbali mbali taratibu kwa ufundi mkubwa waandae katiba maana wataalamu wapo. Ili tuweze kupata KATIBA BORA BEFITTING our beloved state Tanzania!!!!!!! Vinginevyo wasipowasikiliza wananchi watumie ubabe, majibu ya wananchi watayapata maana watu watadai katiba na nchi yao iliyobakwa na corrupt system!!!!!! Waasalam.
 
Hii katiba ni ya tanzania,na munafahamu kuwa muungano ni baina ya nchi mbili,sasa hapa munajadili katiba ya tanganyika au ya tanzania ? na kama tunajadili ya tanzania kwa nini tusikae tume huru ambazo kutoka tanganyika na zanzbar,sio tanzania na zanzbar ...

Inamana huu ndio usaniii ? Hapa hakuna lolote lile,rais anafahamu kuwa ikiwa atafanya tume huru basi ataondolewa madaraka makubwa sana juu ya urais wake na ndio maana kataka kulisimamia yeye mwenyewe,ili aweze kuvipinga vipengele fulani.

Hata hapa zanzbari vile vile juzi kulipelekwa mswada katiba bunge la zanzbar ,,,spika kaupinga mswaada huo wa kujadili muungano,na hii ndio shindikizo la rais wa zanzbar,hi yote kulinda nyazifa zao.

Kuna kazi kweli kweli hapa wananchi lazima tuwe makini.
 
ULAGHAI WA KIKWETE KUHUSU KUUNDWA KWA KATIBA YENYE WANANCHI KWENYE STERINGI SASA TUNASEMA BASI: TUNATAKA SERIKALI YA MPITO KUSHUGHULIKIA KATIBA NCHINI NA KUKAMILISHA KILA KITU 2014

CHADEMA,Asasi za Kiraia nchini, Vyuo Vikuu na Nchi Wahisani tunaomba mtuelewe kwamba sasa uzalendo umetushinda na huu utani wote na kiburi ya Mhe Kikwete - tunataka serikali mpya ya mpito sasa hivi kushughulikia katiba!!!

Wananchi; kila mmoja mahala ulipo wakati umefika wa kuachana na mchezo katika mambo ya msingi ambayo tumejaribu kutafuta kiungwana ndio hivo imeshindikana. Hakuna haja kuendelea kubisha mlango usiofunguliwa bali hapa ni kutafuta njia njingine kabisa kwa uwezo wa Nguvu ya Umma.

Cha msingi sasa sisi wenyewe tena vijana, kwa njia zetu zile, TUNAIPA SERIKALI YA Mhe Kikwete hadi April 08, 2011 iwe imewashirikisha wadau wote na mawazo yetu, katika hatua zote za ushiriki, usimamizi na uendeshaji wa mambo ya katiba kwa kuzingatia matakwa ya wananchi na wala si kutulazimiza na matakwa ya watawala ambao ndio haswa tunaowalalamikia kwa unyanyasaji.

Vijana tuliowengi nchini tusimame kutetea haki zetu kwani haki hapewi mtu hata siku moja. Endpo serikali haitotii hayo maoni yetu basi Vijana kote nchini pamoja na taasisi marafiki wa UTAWALA WA KIDEMOKRASIA NA USHIRIKISHWAJI WA WANANCHI MOJA KWA MOJA tujiweke tayari kwa maandamano ya amani kote nchini mpaka matakwa haya yatimizwe au serikali inaposhindwa basi ikatupishe njia haraka!!

Tunasema katika huu mzaha wa serikali kuhusu tume HURU YA BUNGE kugeuzwa kuwa TUME TEGEMEZI YA RAIS ikibarikiwa na Bunge; Vijana tumefika Tamati tena hadi hapa!!!

Kumbe Kupatikana kwa Katiba Mpya chini ya Uongozi wa CCM haiwezikani bila serikali kututwisha MADALALI kwenye mambo ya kuundwa kwa Katiba Mpya nchini.

CHADEMA tusikilizeni, tunahitaji kwana SERIKALI YA MPITO kumbe yenye jukumu moja tu kushughulikia Katiba kwa MUJIBU WA MATAKWA WA WANANCHI katika hatua zote za usimamizi na maamuzi.

BAVICHA na matawi yetu yote ya CHADEMA nchini tueleweni kwamba wananchi sasa tunasema baaasi na Serikali ya CCM iondoke madarakani sasa hivi. Sote tunao uwezo wa kubadilisha haya mambo yote kabla hatujaingizwa porini zaidi.

Mwenye kupata ujumbe huu na akawajulishe vijana wengine 10 juu ya ulaghai uliotangazwa na serikali majuzi kutupora haki ya kusimamia kuundwa kwa katiba mpya bila kuingiliwa na dola.

Lengo lao likiwa ni kuleta katiba waitakayo MAFISADI nchini, kuchelewesha muda tuingie uchaguzi 2015 bila katiba mpya, na vile vile kukiundia CHADEMA mikesi ya kuchonga kisiasa ili baadhi ya wale tunaowapenda wasigombee.

SASA TUNASEMA KATIBA MPYA NA TUME HURU YA UCHAGUZI BARA NA VISIWANI YOTE YAWEZEKANA BILA CCM, TUPISHENI NJIA!!!

Uwezotunao,

Pengine mimi niongezee kwenye jina lako tu kwamba,SABABU TUNAZO NA NIA TUNAYO ya kuleta mabadiliko ya KATIBA MPYA YA NCHI YETU TANZANIA.

Kwa uchungu kabisa toka moyoni nasema kwamba SERIKALI YA CCM wanatafuta kitu wanachokitaka nacho ni NGUVU YA UMMA.
CCM NA SERIKALI YAKE ni watu waliochoka kufikiri na kama alivyosema mmoja wa kada wao wa UVCCM kuwa wakati wa KUFIKIRI KWA KUTUMIA TUMBO UMEPITA ni wakti wa KUFIKIRI KWA KICHWA. CCM WAACHE KABISA MCHEZO WA KUFIKIRIA MATUMBO YAO BAALI WAFIKIRI KWA AKILI WALIZOPEWA NA MUUMBA WETU KWAMBA KAMA WATAFANYA MZAHA KWENY SWALA HILI LA MABADILIKO YA KATIBA BASI napenda kuwahakikishia CCM kuwa:

KILE AMBACHO TUMEKIONA TUNISIA,MISRI,LIBYA,YEMENI na sehemu nyingine ambako NGUVU YA UMMA IMEZIONDOSHA SERIKALI ZA KIDIKTETA,KIMABAVU,KANDAMIZI na ZISIZOJALI MATAKWA YA WANANCHI ndizo zinaenda kuikumba TANZANIA.

CCM tunawatahadharisha kuwa KAMA HAWATAKI MABADILIKO YA KATIBA NI AFADHALI WAACHANE NA MCHAKATO HUU NA WAKAE PEMBENI WATUACHIE WANANCHI TUJADILI NA KUTOA MAONI JUU YA KATIBA TUNAYOITAKA.

CCM MSIFIKIRI KUWA WATANZANIA WA KIZAZI HIKI NI WALE WA ENZI ZA MIAKA YA 47 MBUMBUMBU MZUNGU WA RELI, WATU WANAOPELEKESHWA, KUDANGANYWA NA KUDHULUMIWA HAKI ZAO HUKU WAKISEMA WANADUMISHA AMANI NA MSHIKAMANO. HIZO ENZI SIYO HIZI.

CCM MSIJIFANYE VIPOFU NGUVU YA UMMA HAIKO MBALI SANA.WATANZANIA SIYO MALAIKA WASIOTAKA MABADILIKO YA KATIBA.
WATANZANIA WANATAKA KATIBA MPYA NA SI VIRAKA VYA KATIBA. HATUWAELEWI CCM MNA MAANA GANI MNAPOZUIA WATU WASIGUSE MAMLAKA YA KUPITILIZA ALIYONAYO RAIS,MAMBO YA BUNGE,MAHAKAMA NA MUUNGANO. Tunajua yote haya yako kwenye Katiba ya sasa ambayo haitakiwi. Sasa mnapozuia yasihojiwe mnataka Watanzania tujadili nini????

Rais Kikwete TUNAKUSIHI UACHE USANII WA KUTAKA KUWAGHILIBU WATANZANIA ILI CCM IENDELEE KUTAWALA. TUNAJUA WEWE UKO KWENYE KIPINDI CHAKO CHA MWISHO. NI DHAHIRI KWAMBA KWA KIPINDI CHA KWANZA HAKUNA LOLOTE LA MAANA ULILOTUFANYIA WA-TZ ZAIDI YA KUFANYA MAISHA YETU KUZIDI KUWA MACHUNGU NA MAGUMU. SERA ZAKO ZA MAISHA BORA KWA KILA M-TZ ZILIKUWA POROJO ZA KUOMBEA KURA TU. MAISHA BORA ULIYOAHIDI WA-TZ KUMBE ILIKUWA NI MAISHA BOMU!!!UFISADI UMEKUSHINDA! CHAMA CHAKO KIMEKUSHINDA NA SASA KINAENDA KUKUFIA MIKONONI.

SIJUI WA-TZ WATAKUKUMBUKA KWA KITU GANI EWE ******! NI AFADHALI UJITAHIDI HILI LA KATIBA ULISIMAMIE KWA HAKI BILA KUCHAKACHUA ILI UKIONDOKA WA-TZ WAKUKUMBUKE KWA HILI. NAKUPA POLE SANA MHE.RAIS WA WANA-CCM!!
 
nawasikiliza wenzangu tunaamua nini.... maana CCM inatuzungusha kwenye mduara
 
Well,if you believe at least the parliament to be legal,i.e it represents the mass proportionally,then submit your motion to the floor and lobby for the votes/support,if not try 2015 may be you will have the majority in the parliament.Just because you get crowds in your demos doesn't constitute that your party has the majority support.

CDM or other groups can choose to submit their different motions in the parliament but if they are sure to loose, I don't see the point why not try the use of legal street demos. If successful, it implies big crowds in demos can constitute that the party has majority support. We have same examples from other parts of the world.

In order the whole country to be in piece and harmony of which CCM stands for, CCM as a ruling party that owns the government has to stop games of the jungle on 'CONSTITUTIONAL ISSUE'' instead it has to consider broadview opinions from the whole society otherwise CDM and the people can choose to play jungle-games too.
 
CDM or other groups can choose to submit their different motions in the parliament but if they are sure to loose, I don't see the point why not try the use of legal street demos. If successful, it implies big crowds in demos can constitute that the party has majority support. We have same examples from other parts of the world.

In order the whole country to be in piece and harmony of which CCM stands for, CCM as a ruling party that owns the government has to stop games of the jungle on 'CONSTITUTIONAL ISSUE'' instead it has to consider broadview opinions from the whole society otherwise CDM and the people can choose to play jungle-games too.
Mkuu Tom this friend of ours Mr Kobelo may be is staying in his own world, if he cant see what is hapenning around us then is blind. If that is the concept of his masters SISIEM then we are in real trouble. Then tujiandae kwa mapambano kudai KATIBA YETU YA TANZANIA. Niliisha sema kuwa kama SISIEMU na serikali yao wataziba msikio wasiwasikilize Watanzania wanataka nini; watasababisha moto uwake hapa nchini na huo utakuwa ni mwisho wa utawala wa Mheshimiwa Kikwete. Kama anadai aliwekwa na watu kidemokrasia kutawala sio udekiteta basi watu watatumia njia za maandamano kudai haki zao na kumuondoa Raisi madarakani. Mbona mambo yako wazi, si watu wanaona wenzao wanafanyaje??????? Tanzania sio kisiwa wala hatuishi mwezini, tena mambo yanakwenda spidi kubwa, awe nani SISIEMU, CDM au yeyote hawezi kuzuia watu kudai haki zao, kwani Libya wanaongozwa na chama gani???????? Kuna mwisho wa kuvumilia kuongozwa na mafisadi, wezi, wanaozika watu wazima wazima kwenye migodi eti wasiulizwe, nchi imekuwa ya nani???????? Uongozi huu sio ule wa Nyerere ni wa mafisadi, watu watachoka tena karibuni wakisukumwa na ubabe wa serikali kuweka katiba feki, watadai nchi yao watazinduka!!!!!!!!
 
Kama nilivyosema hapo awali, wananchi wasitegemee kabisa kwamba CCM na rais JK wataachia mamlaka ya kuunda tume vyombo vingine ambavyo havina nguvu kikatiba kwa sababu wananchi wametaka iwe hivyo..

Tanzania ni nchi inayotawaliwa na hizi hadithi za kusema wananchi ndio tumemwajiri rais ni usanii mtupu kwani CCM kama utawala wa Ivory Coast hawawezi kukubali hatua zozote zinazoweza kuwadhoofisha na hata kuondolewa madarakani..

Kibaya nachokiona mimi CCM wameanza kutumia mbinu za kuligeuza swala hili liwe la kisiasa na sii muhimu kwa wananchi..

Nitarudia kusisitiza tena kwamba kwa mazingira ya nchi hii, katiba mpya haiwezi kupatikana kupitia nje ya nguvu ya dola, aidha tukubali JK achague tume yeye au nguvu ya Umma itumike kinyume cha hapo hii kitu imekaa vibaya sana.. Ni sawa na kumwondoa mkoloni hali wakijua watapoteza kila kitu walichojenga na kujinufaisha..

Baada ya jana nina hakika CCM, watajaribu kwa kila hila kukemea vyama vya upinzani na vijana kuwa wao hawana lengo la kuipata katiba mpya yenye manufaa kwa nchi nzima isipokuwa manufaa kwa vyama vyao..

Nimemsikiliza Tendwa na Hosea jana wakizungumza na nikahisi wanakopelekea malalamishi yao ni kwa vyama vya upinzani hasa Chadema ya wananchi kuwa waloshiriki ktk mjadala wa jana ni wafuasi wa vyama vya upinzani na sii wananchi wanaotaka kujenga hoja Kitaifa.

Hata kama muswada huu utarudishwa na kuandaliwa upya, maswala yote muhimu mnayoyataka ndio kinga na nguvu ya CCM na rais kutawala, hivyo hawawezi kukubali kuwakabidhi panga kirahisi hivyo..

Sii rahisi kwa jambazi la Kitanzania kujipeleka polisi au mzinifu kumkabidhi panga mwenye mke na kumwambia nimezini na mkeo, chukua hatua unayotaka.. Hayo
Yatakuwa maajabu ya Firaun...
 
Kama kweli tunataka kuwa na katiba mpya ambayo itaweza kulinufaisha Taifa letu na kuwa na Tanzania ambayo itakuwa njema kwa kila mmoja wetu ingefaa tukaiga wenzetu hawa hebu soma uone na ndio maana wanaendelea Kuliko sisi .

tafadhali chukua muda kidogo soma utanufaika na mengi na hata ukitaka kutoa maoni unaweza kupata mambo ya kuongezea.
 

Attachments

Back
Top Bottom