elmagnifico
JF-Expert Member
- Jul 7, 2011
- 8,261
- 9,733
Tarehe 3 mwezi wa 4 mwaka 2008, Mr Tom Wiles mmiliki wa kampuni iitwayo National Flight Services, inayohusika na kufanya matengenezo ya ndege, kufundisha kurusha ndege, na shughuli zote zinazohusiana na ndege ikiwa na makao makuu Ohio lakini ikiwa na ofisi Florida, Texas na Canada, akiwa nyumbani kwake kalala alipokea meseji kwenye simu yake kutoka kwenye namba ya simu ya mwanaye Robert iliyokuwa ikimtaka afungue email yake kama anataka kumpata mwanaye Robert akiwa hai.
Meseji hiyo ilikuwa ni ya pili baada ya awali kutoifungua kwakuwa alikuwa kalala. Alipofungua email yake alikuta ametumiwa email ikimwelekeza kuwa kama anataka kumuona mwanaye Robert akiwa hai basi, apeleke kiasi cha pesa kipatacho dola 750,000 ofisini zikiwa zimefungwa vizuri na ziwekwe kwenye ofisi ya Robert.
Pia ilimwelekeza kuwa asithubutu kuwahusisha polisi na asijifanye mjanja maana asipofuata alichoambiwa atapoteza mwanaye, na ikalizika kwa mtekaji kuandika kuwa anaitwa Group X. Mr Tom alichanganyikiwa sana na akamuonyesha email hiyo mkewe, na baada ya kushauriana waliamua wawataarifu polisi.
Polisi walifika nyumbani kwa Mr Tom, na baada ya kuonyeshwa hiyo email walikubariana kuwa kiasi cha pesa waliyodai kiandaliwe na kuwekwa ofisini kwa Robert pale NFS kama email ilivyoelekeza, ila ifungwe video camera ya siri ambayo itakuwa inarekodi matukio yote yatakayo kuwa yanaendelea mle ofisini, na kuyarusha kwa polisi ili wapate kumuona ni nani atakaye kuja kuchukua hiyo pesa maana walihisi ni mfanyakazi wa kampuni ya NFS.
Kwakuwa email ilimtaka asihusishe polisi, walimuuliza ni mfanyakazi gani anayemuamini pale NFS, ambaye ndiye polisi wanaweza mkabidhi hiyo kazi ya kuweka hiyo pesa na pia kufunga hiyo camera ya siri.
Mr Tom akawambia Operation manager Mr Stobert Holt ndiye anayemuamini zaidi. Hivyo walimtaka apigiwe simu aombwe kufika kwa Mr Tom mara moja.
Baada ya kupigiwa simu Holt alifika kwa boss wake Mr Tom na baada ya kupewa maelezo ya nini kimetokea na nini kinatakiwa kufanyika alikubari.
Kweli Mr Holt alipewa hiyo ela akaipeleka ofisini kwa Robert pale NFS pia alafunga hiyo kamera ya siri ambayo iliwawezesha polisi kufuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea pale ofisini.
Baada ya hapo wafanyakazi wengine hawakuambiwa nini kilichokuwa kinaendelea na wala kama Robert katekwa hivyo shughuli ziliendelea kama kawaida pale ofisini huku polisi wakisubiri kuona ni nani atakaye enda kuchukua ile pesa.
Siku ikaisha pasipo mtu yotote kuchukua ile pesa, na kesho yake ikawa hivyo hivyo. Polisi wakaingiwa na wasi wasi labda huenda mtekaji kajua kuwa amewekewa mtego. Jambo hilo liliwafanya wajiulize atakuwa kajuaje maana siri ilikuwa baina yao, Mr na Mrs Tom na Holt tu.
Polisi wakahisi labda uenda Mr Tom ndiye anacheza huo mchezo baada ya kugundua ya kwamba kiasi cha pesa lilichoombwa na watekaji ni sawa na kiasi kile kile ambacho Robert alikuwa kakatiwa Bima iwapo atatekwa au kuawa.
Hili lilifanya polisi wahisi hapa kuna mchezo mchafu unachezwa, labda inawezekana Mr Tom Wiles akawa na tatizo la kipesa hivyo wakaanza kuchunguza mwenendo wa kipesa wa Mr Tom, lakini wakagundua ana pesa ya kutosha wala hana madeni kampuni yake inaingiza faida kubwa sana.
Polisi wakasubiri wakitegemea mtekaji labda atatuma ujumbe mwingine wa madai au maelekezo lakini siku tatu zikapita hakuna chochote ndipo wakahisi hali ya hatari, ikawabidi waanze fanya upelelezi kuanzia ofisini kwa kuwahoji wafanyakazi.
Tom Wiles na mkewe (Baba na mama yake Robert)
Robert Wiles
Holt Toby
SEHEMU YA PILI
Polisi walianza uchunguzi pale NFS kwa kuwahoji wafanyakazi mbali mbali kuhusu Robert, lakini hawakuweza kupata jambo lolote la kuwasaidia kuweza kung'amua Robert alipo au ni nani anaweza kuwa kahusika na utekaji wake.
Katika upelelezi wao ilibainika kwamba tarehe mbili mwezi wa nne mwaka 2008, yani siku moja baada ya siku ya mwisho Robert kuonekana katika ofisi za NFS, Robert ilikuwa asafiri kwenda Dallas kwenye maonyesho ya kiboashara.
Lakini katika uchunguzi polisi walibaini kuwa Robert hakupanda ndege wala kufika kabisa uwanja wa ndege.
Walizidi jiuliza maswali, ni nani ambaye angejua kuwa Robert ana Bima ya Utekwaji ambayo thamani yake ni 750,000 USD, kiasi kile kile ambacho mtekeja alitaka apewe.
Jibu likawa lazima atakuwa mtu wa karibu wa hiyo familia, pia polisi wakaanza kuwa na wazo la huenda Robert ndiye kaamua kucheza huo mchezo. Pia wakahisi labda Robert ameamua tu kuondoka baada ya kutopenda jinsi maisha yake yanavyoenda kwakuwa baba yake alitaka aje kuwa msimamizi na mrithi wa NFS huko mbeleni labda huenda yeye Robert hakupenda.
Katika kujaribu kupeleleza kujua uhusiano baina ya Robert na baba yake ulikua vipi, watu wengi walidai kwamba Robert alikuwa karibu sana na baba yake na alikuwa anapenda na kufurahia kazi yake.
Kwakuwa habari juu ya kupotea kwa Robert ilikuwa ishasambaa polisi walianza kupokea simu zenye taarifa mbalimbali. Simu moja ambayo walienda kuonana na mpingaji simu ambaye alikuwa mwanamama aliwambia kuwa, aliwahi zungumza na Robert na Robert akadai kuwa hapendi kazi anayofanya ambayo baba yake anamlazimisha aje kurithi.
Pia alidai Robert alimwambia ipo siku atatoroka apotee aende kuanza maisha mapya. Kwa taarifa hiyo polisi walianza pia kuzingatia dhana ya kwamba huenda Robert katoroka mwenyewe, lakini baadae waliachana nayo kwakuwa haikuwa na mashiko.
Muda ulizidi kwenda na hawakuwa na jambo lolote la maana la kuwasaidia ndipo waliamua kurudi mezani kuanza upya kwa kupitia maelezo ya watu wote waliokuwa wamehohijiwa huenda kuba taarifa ambayo hawakuizingatia.
Katika kupitia taarifa za watu mbalimbali hasa wafanyakazi, jina moja lilikuwa likiibuka naye ni Holt.
Kwanza Holt hata yeye alikiri kuwa ndiye alikuwa mtu wa mwisho kumuona Robert akiondoka pale ofisini. Pili mfanyakazi aitwaye Grief naye alisema kuwa wakati anaondoka kutoka kazini siku Robert alipopotea, aliwaacga Holt na Robert ndiyo bado wako kazini.
Mfanyakazi mwingine aitwaye Meuer naye alisema alirudi ofisinu mida ya saa kumi na moja na alimkuta Holt bado yupo maeneo ya ofisi, na kilichomrudisha kuna vitu alikuwa kafuata na wakati anaondoka aliona kwenye parking kuna gari la Robert na gari la Holt.
Polisi walishtuka wakagundua huenda, Holt ndiye mtu anayehusika na utekaji wa Robert. Pia waliogopa kuwa huenda Robert anaweza kuwa ameshauawa kama kweli Holt ndiye mhusika, na polisi ndiye walimshirikisha kupeleka pesa na kutefesha kamera kumbe mhusika huenda ndiye yeye.
Polisi ikabidi warudi kuhoji wafanyakazi juu ya uhusiano wa Robert na Holt, na haikuwa chukua muda kutambua kuwa kulikuwa na mvutano baina yao na Robert mara nyingi alikuwa anawahamasisha wafanyakazi wamseme vibaya Robert kuhusu utendaji wake wa kazi.
Kuthibitisha hilo, polisi waligundua kuwa kuna vikao vilikuwa vikifanyika ili kushawishi uongozi umuhamishe Robert kwenda ofisi za Texas.
Pia waliweza pata email ambazo Holt alikuwa alituma kwa watu mbalimbali akimsema vibaya Robert.
Baadhi ya emails hizo hizi hapa chini.
Ukisoma hizo emails utaona kuwa kulikuwa na mvutano baina yao na Holt alikuwa mara kwa mara akilalamika kuhusu utendaji wa Robert. Walipozidi kuchimba zaidi kuhusu Holt, polisi walibaina kuwa pia Holt alikuwa siyo mtu safi kama alivyokuwa anajionyesha au alitaka aonekane mbele ya jamii.
Holt alikuwa na wanawake wengi, na alikuwa anapenda malaya. Pia waligundua Holt alikuwa akiingia mikataba na wateja wa NFS akiwa anazingatia kujinufaisha yeye zaidi kuliko masrahi ya kampuni.
Polisi ilibidi wamwite Holt kwenye chumba cha mahojiano ili awaeleze alikuwa wapi na alifanya nini siku hiyo ambapo Robert inadhaniwa alitekwa.
Nitaendelea baadae......
miss chagga
Nimekutag tayari