Muujiza wa Familia ya Nigeria ulivyoishangaza Sayansi

Muujiza wa Familia ya Nigeria ulivyoishangaza Sayansi

Wangekuwa wamezaliana kijiji cha ikuti mbeya ambapo hakuna mtu mweupe hata mmoja stori ingekuwa haina shaka ila wapo uingereza halafu tunapangwa tukubali maajabu.
 
Mnamo mwaka 2010, wanandoa wa Nigeria waliokuwa wakiishi Uingereza, Ben na Angela Ihegboro, walipata mtoto wao wa kike aliyeitwa Nmachi, aliyezaliwa akiwa na nywele za rangi ya dhahabu, macho ya bluu, na ngozi nyeupe, licha ya Ben na Angela wote kuwa na asili ya Nigeria na kutokuwa na historia yoyote inayojulikana ya mababu wenye asili ya kizungu. Ben Ihegboro alisema kuwa mwanzoni alishangazwa na kustaajabu, na kwa utani akauliza kama mtoto huyo ni wake, lakini hakuwa na shaka na uaminifu wa mke wake.

Wanandoa hao waliamua kumpa binti yao jina Nmachi, lenye maana ya "Uzuri wa Mungu," na walimchukulia kama “mtoto wa kimiujiza.” Wataalamu wa matibabu walivutiwa na tukio hilo na kutoa nadharia kadhaa. Nadharia iliyotolewa ni kwamba huenda kulikuwa na vinasaba vya kizungu vilivyojificha, ambavyo vingeweza kurithiwa kutoka kwa mababu wa mbali.

#EastAfricaTV #HainaKuchoka ✍️@_centralboy View attachment 3178778 😁 Sasa unafikilia Nini ila watu🤣
Mbona ilishatokea pia South Africa, tena kwa Wazungu kumzaa mtoto maeusi? Japo baba yake alimkataa kabisa, ilikuja kufahamika baadaye binto akiwa ameshakuwa mtu mzima kuwa alikuwa mtoto halali wa Mzungu. Wazazi wake walikuwa na "damu" ya Kiafrika.
 
Unajuaje wazazi ni mweusi na mweupe?

Herufi tatu tu zinamaliza mjadala.

DNA.

Issue ni hii, mtoto wa muafrika na mzungu lazima awe chotara. Sasa hapa baba na mama wote ni weusi, halafu wanazaa mtoto blonde with blue eyes. Hiyo ni muujiza ama walimbadilishia mtoto. Lkn si kuchepuka.

DNA inaweza kutatua hili
 
Issue ni hii, mtoto wa muafrika na mzungu lazima awe chotara. Sasa hapa baba na mama wote ni weusi, halafu wanazaa mtoto blonde with blue eyes. Hiyo ni muujiza ama walimbadilishia mtoto. Lkn si kuchepuka.

DNA inaweza kutatua hili
Unajuaje baba na mama wote ni weusi?
 
Hapo hujaona wamesema social father wake au mme wa huyo mzazi si ni mweusi?
Kwani lazima mme wa mwanamke ndiye awe baba wa mtoto?

Unaelewa kuwa bila DNA test hatuwezi kuwa na uhakika kuwa huyo ni hata mtoto wa huyo mama, achilia mbali huyo baba?
 
Hapa Tanzania tungegawana majengo ya serikali
 
Sasa hapo mbona ipo wazi. Huitaji akili kubwa kubaini kuwa Jamaa kapigwa.
 
Back
Top Bottom