Muujiza wa Tony Kapola: Je aliombea mtungi mkubwa au mdogo?

Watumishi wanamezesha kwanza sumu ya uaminifu kwa waumini kabla ya kila kitu kisha kuanza kuwapa hadithi za uongo na ulaghai kwahy wak inakua rais kuingia kwenye mtego wa kwa bwana hakuna kinachoshindka
 
Kuna siku nipo YouTube nakawa namsikiliza mtoto wa Nyerere anaitwa Rosemary Nyerere (RIP).

Huyu alisema kipindi wanasoma , walilazimika kufuga kuku ili kupata hela ya Ada na wakati huo baba alikuwa Rais.

Nikawa nawaza Mimi Babu yangu alikuwa muhasibu , mwenye Diploma na amefanya Kazi na wakoloni pamoja na Nyerere Ila watoto wake wore walisoma vizuri na Shule bora mpaka wengine walisoma nje.

Na huyo alikuwa mfanyakazi tu Ila watoto wa Rais ili wapate Ada ilibidi wafuge Kuku aaah!!!


Najaribu kuangalia ukwasi wa Kapora na kuishiwa gas na kupuliza na kurejea mtoto wa Nyerere Rosemary.
 
Mfano wa gesi ni mfano wa uongo mkubwa ulioenda viral bila kutegemea
 
WaAfrika t una shida mahali
 
Mshana Jr nimeona nikujibu maana wewe ni gangwe. Hicho alichokisema Mke wa Pastor Tony kina ukweli πŸ’―. Kwenye biblia Nabii Elia aliombea Unga na Mafuta kwa yule Mama Mjane na walipika na havikuisha walipika na kula kwa siku alizokuwa Elia kahifadhiwa. Kwa habari zaidi soma
1 Wafalme 17:12-14. Wewe kama mdau mkubwa epuka kupotosha. Pastor Tony anahistoria yake, hiyo miujiza ni ya kweli na Mungu wake anatenda miujiza kweli kweli. Nadhani umeelewa.
 
Watu weusi wanapenda kudanganywa sana.
Ni kweli na hiyo ni Fursa - ILA sasa watu weusi wadanganyaji (Matapeli) hawajui kujipanga kimaandalizi na Kimkakati . Wanapwaya sana kiasi kwamba mbinu ya ulaghai wao hugundulika kirahisi mno na kwa haraka sana. Sio Maprofesheno. Ukiondoa biblia na wao ndo kwishney.
 
Dah! Any way; gangwe wako atajibu lakini mm nachangia tuu. Kwanza Unatakiwa uone mazingira ya kisa cha Nabii Eliya kwa mapana yake.(Mjane wa Sarepta) i.e. huyo mama mjane alikuwa na mtoto mgonjwa (alikufa lakini akafufuliwa na Eliya) mjane alikuwa amefikia ukomo wa matuamaini (haijasemwa kama alikuwa ameomba/sala kwa muda gani) ......na ndo mana siku hiyo akajibu "...nami ninaokota kuni mbili ili niingie nijipikie nafsi yangu na mwanangu, tuule tukafe". Tukirudi kwa hili la Tony: Je, huyo Tony na Mke wake walikuwa hawana tena namna/mbadala i.e. wangekufa kama wasingepata hiyo gesi? BTW, Ni kweli Mungu anaweza yote na kwa namna na muda atakavyo lakini sidhani na wala siamini kama Mungu anapenda kuamrishwa kwa matakwa ya kibinadamu tena ya kijinga kama ya Bwn. Tony i.e. Unamtia Mungu majaribuni!! mfano wa Ibilisi aliyesema... ..."Kama ww ni mwana wa Mungu amuru mawe haya yawe mkate......"
- Je, mkaa ulikuwa umeisha? -Je, Fedha ya kununua gesi iliisha, Je, muda ilikuwa ni usiku hawezi tena kuagiza hata boda gesi iletwe? n.k.n.k. Mm nahitimisha kwamba huyo mungu wa bwn. Tony ni mungu wa kijiweni.(Samahani lakini kama nimekukwaza)
 
Bosi wewe ni Mkristo ila imani yako ni ndogo sana maana unatumia akili yako kuamini. Kumbuka Yesu Kristo alisema β€œ
Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambia, Yeye aniaminiye mimi, kazi nitendazo mimi atazitenda na yeye; tena atafanya kuliko hizi, kwa kuwa mimi naenda kwa Baba.” (Yohana 14:12)”.

Hivyo ukiamini Mungu anaweza kukutendea makubwa zaidi ya hayo watendayo akina Pastor Tony. Mshana Jr nilimstahi ili kumjulisha tu kuwa hivyo vitu vipo na vinawezekana. Na nikuhakikishie tena kuwa kila aaminiye hata kama ni Muislamu anafanikiwa!
 
Mkuu, kuna uzi uliandika kwamba umeokoka. Ulokole wako unakuruhusu kuwaita walokole wenzako "majuha"? Umewashutumu kwamba wametukana halafu mwenyewe umeingia kwenye mtego huohuo wa matusi.

People who live in glass houses shouldn’t throw stones.
 
Msaidieni huyu matunguri yameanza kumzidi nguvu. Asipoangalia kondoo watatawanyika na kukimbilia mazizi mengine, si dalili nzuri japo yeye anaweza furahia kwamba anatrend
 
Hiyo miujiza ya aina hiyo ingekuwa inafanya kazi Nigeria lingekuwa Taifa tajiri zaidi duniani.
Kuna msitari mwembamba sana kati ya mnachoita miujiza na uchawi.
Acheni kutumia ukristo kuficha utapeli, wizi na uchawi kwa kutumia mistari ya biblia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…