Muujiza wa Tony Kapola: Je aliombea mtungi mkubwa au mdogo?

Muujiza wa Tony Kapola: Je aliombea mtungi mkubwa au mdogo?

Mkuu, kuna uzi uliandika kwamba umeokoka. Ulokole wako unakuruhusu kuwaita walokole wenzako "majuha"? Umewashutumu kwamba wametukana halafu mwenyewe umeingia kwenye mtego huohuo wa matusi.

People who live in glass houses shouldn’t throw stones.
Akina Tony na Wote wa aina yake sio Walokole kamwe. Tofautisha hapo Walokole na hao Makanisa ya Kileo
Makanisa ya Kileo huwezi kufuatilia chanzo chao wala kiongozi wao. Wanaibuka popote.
 
Pasta Tony kwenye harakati za kuujaza mtungi gas
IMG-20250808-WA0010.jpg
 
Tony Kapola anatumia nguvu nyingi sana kuusafisha uongo wa mkewe kwenye muujiza wa gesi.. Anatumia cover up ya Biblia takatifu na vijembe vyenye matusi ndani yake! Lakini hatafanikiwa bali ndio anazidi kuharibu
Ukweli ni kwamba hakuna watu mahiri wa kutoa mifano ya uongo kama hawa wahubiri na wake zao.. Kuna wakati mtu anatoa mfano wa uongo ama ushuhuda feki mpaka inakera
Mke wa Tony Kapola alichotoa ni ushuhuda wa muujiza feki ambao hakutegemea kama utaenda viral mitandaoni
Waumini ni kama mikondoo . huwa hawahoji kwakuwa wanahubiriwa na wanachotakiwa kufanya ni kuamini... Sasa kwa dunia ya leo ya utandawazi unaweza kuwa control waumini wako lakini si watu wengine nje ya waumini wako
Twendeni na huu uhalisia wa maisha muone yule mama na mumewe walivyo majuha
Kwa ukwasi walionao na maisha wanayoishi haiingii akilini hata siku moja kwamba wanatumia jiko la gesi lisilo na option ya umeme.. Never!
Kwa maisha wanayoishi haiingilii akilini kwamba wanatumia gesi yenye regulator ya kawaida isiyoonesha kiwango cha gesi.. Siku hizi kuna regulator za kisasa zinazokuonesha kiwango cha gesi kilichopo
Kwa maisha ya ukwasi wanayoishi haingilii akilini kabisa kwamba hawana wafanyakazi wa ndani kama mpishi, mfanya usafi nknk
Inawezekana hata kama wapo wafanyakazi lakini mzee hupenda kula kilichopikwa na mkewe ama kuna siku mama huamua kuingia mwenyewe jikoni! Na siku hiyo ndiyo ikawa hivyo na kukutana na gesi ikiwa imekwisha!
Hapa kuna jambo lingine la kuzingatia.. Kwakuwa mama si mpishi wa mara kwa mara hivyo hajui kwamba kuna wakati regulator hufungwa na mtu aliyetumia mara ya mwisho...Hapo bila kuifungua regulator iruhusu gesi kupita, kule kwenye burner hakutawaka!

Pengine bila kulijua hili mama akaripoti kwa mzee .. Mzee akaja jiloni akapiga maombi akaupuliza mtungi ukajaa gesi akafunguq regulator. Mama akawasha kwenye burner.. Gesi ikawaka kwa kasi.. Na ikawa ni muujiza tayari😂😂😂
Hapa kuna mtu aliingizwa cha kike naye akaenda kuwaingiza wengine! Mtungi wa gesi sio puto jamani.. Kwamba utapuliza na kuona kabisa linajaa hewa! Kapola yeye kapuliza mtungi wa gesi na kuujaza gesi.. Sasa sijui ni ule mkubwa au ni ile inayogawiwa vijijini maarufu kama mitungi ya mama!?🤔😩

Kwa uzoefu wangu kwenye miujiza ya dharura kama hiyo.. Hakukuwa na haja Tony aanze kuupuliza mtungi bali ilikuwa ni kitendo cha kuamrisha ama kuomba kiimani na jambo likawa!

Ni kama tu wale wachawi konki.. Wao hawahitaji pesa! Maana hawana matumizi nazo kwakuwa kila watakacho hukipata kwa kutamka tu!
Kapola alikuwa na uwezo wa kutamka shibe na wakashiba.. Alikuwa na uwezo wa kutamka chakula kiive bila gesi na ikawa nknk.. Lakini muujiza wa kupuliza mtungi mtupu na ukajaa gesi ni uongo uliopitiliza!View attachment 3435472
wanawake wa siku hizi hawapiki,chakula chake kinapikiwa sinza na mdada anayeuza uji pale church kwake kama anabisha nilete ushahidi
 
Mshana Jr nimeona nikujibu maana wewe ni gangwe. Hicho alichokisema Mke wa Pastor Tony kina ukweli 💯. Kwenye biblia Nabii Elia aliombea Unga na Mafuta kwa yule Mama Mjane na walipika na havikuisha walipika na kula kwa siku alizokuwa Elia kahifadhiwa. Kwa habari zaidi soma
1 Wafalme 17:12-14. Wewe kama mdau mkubwa epuka kupotosha. Pastor Tony anahistoria yake, hiyo miujiza ni ya kweli na Mungu wake anatenda miujiza kweli kweli. Nadhani umeelewa.
Kapola mwenyewe kwenye moja na mbili
 
Back
Top Bottom