Muujiza wa Tony Kapola: Je aliombea mtungi mkubwa au mdogo?

Muujiza wa Tony Kapola: Je aliombea mtungi mkubwa au mdogo?

Hawa matapeli wa kila aina waliotapakaa nchini, wanatakiwa siku moja wasafishwe wote ili nchi iwe safi.

Shida kubwa ipo kwa msafishaji mkuu ambaye pia ndiye mlinzi na pia mfugaji mkuu wa hao matapeli, huku watu wa tabaka la chini wakiendelea kuathiriwa na hao matapeli.
Hao sioni kama ni tatizo maana MAKONDOO yanaenda yenyewe, nchi hii shada kubwa ni SISIEMU.
 
Afungue kituo cha gesi sasa
Acha wivu bwana Mshana Jr . Hapa wachawi mmeshapigwa bao na ''watu wa Mungu''. Mmezidiwa sasa mnaamua kukashifu miujiza. Hatudanganyiki ng'o. Hatutanunua tena gesi.... Au pengine ''alipuliza'' kwa kutumia ile hewa chafu inayotoka kinyume-nyume wakati wa haja kubwa mama watoto akaona aibu kusema...
 
Tony Kapola anatumia nguvu nyingi sana kuusafisha uongo wa mkewe kwenye muujiza wa gesi.. Anatumia cover up ya Biblia takatifu na vijembe vyenye matusi ndani yake! Lakini hatafanikiwa bali ndio anazidi kuharibu
Ukweli ni kwamba hakuna watu mahiri wa kutoa mifano ya uongo kama hawa wahubiri na wake zao.. Kuna wakati mtu anatoa mfano wa uongo ama ushuhuda feki mpaka inakera
Mke wa Tony Kapola alichotoa ni ushuhuda wa muujiza feki ambao hakutegemea kama utaenda viral mitandaoni
Waumini ni kama mikondoo . huwa hawahoji kwakuwa wanahubiriwa na wanachotakiwa kufanya ni kuamini... Sasa kwa dunia ya leo ya utandawazi unaweza kuwa control waumini wako lakini si watu wengine nje ya waumini wako
Twendeni na huu uhalisia wa maisha muone yule mama na mumewe walivyo majuha
Kwa ukwasi walionao na maisha wanayoishi haiingii akilini hata siku moja kwamba wanatumia jiko la gesi lisilo na option ya umeme.. Never!
Kwa maisha wanayoishi haiingilii akilini kwamba wanatumia gesi yenye regulator ya kawaida isiyoonesha kiwango cha gesi.. Siku hizi kuna regulator za kisasa zinazokuonesha kiwango cha gesi kilichopo
Kwa maisha ya ukwasi wanayoishi haingilii akilini kabisa kwamba hawana wafanyakazi wa ndani kama mpishi, mfanya usafi nknk
Inawezekana hata kama wapo wafanyakazi lakini mzee hupenda kula kilichopikwa na mkewe ama kuna siku mama huamua kuingia mwenyewe jikoni! Na siku hiyo ndiyo ikawa hivyo na kukutana na gesi ikiwa imekwisha!
Hapa kuna jambo lingine la kuzingatia.. Kwakuwa mama si mpishi wa mara kwa mara hivyo hajui kwamba kuna wakati regulator hufungwa na mtu aliyetumia mara ya mwisho...Hapo bila kuifungua regulator iruhusu gesi kupita, kule kwenye burner hakutawaka!

Pengine bila kulijua hili mama akaripoti kwa mzee .. Mzee akaja jiloni akapiga maombi akaupuliza mtungi ukajaa gesi akafunguq regulator. Mama akawasha kwenye burner.. Gesi ikawaka kwa kasi.. Na ikawa ni muujiza tayari😂😂😂
Hapa kuna mtu aliingizwa cha kike naye akaenda kuwaingiza wengine! Mtungi wa gesi sio puto jamani.. Kwamba utapuliza na kuona kabisa linajaa hewa! Kapola yeye kapuliza mtungi wa gesi na kuujaza gesi.. Sasa sijui ni ule mkubwa au ni ile inayogawiwa vijijini maarufu kama mitungi ya mama!?🤔😩

Kwa uzoefu wangu kwenye miujiza ya dharura kama hiyo.. Hakukuwa na haja Tony aanze kuupuliza mtungi bali ilikuwa ni kitendo cha kuamrisha ama kuomba kiimani na jambo likawa!

Ni kama tu wale wachawi konki.. Wao hawahitaji pesa! Maana hawana matumizi nazo kwakuwa kila watakacho hukipata kwa kutamka tu!
Kapola alikuwa na uwezo wa kutamka shibe na wakashiba.. Alikuwa na uwezo wa kutamka chakula kiive bila gesi na ikawa nknk.. Lakini muujiza wa kupuliza mtungi mtupu na ukajaa gesi ni uongo uliopitiliza!View attachment 3435472
Tatizo linalokija ni kuwa watumishi wa siku hizi hawajui maadili ya kibiblia ktk kumtumikia Mungu. Wanafanya huduma kibiashara. Ukisoma Biblia unakutabkuwa miujiza ambayo Yesu alifanya na hata mitume wake ilikuwa inajitangaza yenyewe. Yaani wanamwombea mtu anapona na watu ndio wanashangaa. Mtumishi hana muda wa kutangaza muujiza bali kumtangaza Yesu Kristo. Sasa kwakuwa hawa wa sasa wanataa kujichukulia utukufu basi ndio maana hutangaza miujiza ili kuvuta watu wawaendee na kuwa watu maarufu ili wapige hela. Hivyo, yanayomkuta kwenye mitandao kayataka mwenyewe!
 
Mkuu hilo suala la kawaida sana sijanunua gesi Nina miezi 8 huwa naiombea na kupaka mafuta ya upako ukiwasha moto tu chuma ni mpya

#ulikuwepo
Hatari sheikh. Huoni kuwa unaikosesha mapato serikali yako inayokujengea barabara!
Hii dunia imekuwaje sijui
 
Acha wivu bwana Mshana Jr . Hapa wachawi mmeshapigwa bao na ''watu wa Mungu''. Mmezidiwa sasa mnaamua kukashifu miujiza. Hatudanganyiki ng'o. Hatutanunua tena gesi.... Au pengine ''alipuliza'' kwa kutumia ile hewa chafu inayotoka kinyume-nyume wakati wa haja kubwa mama watoto akaona aibu kusema...
😭😭😭😂😂😂🙌🏿🙌🏿🏃🏿🏃🏿 walishindia maharagwe na mayai ya kuchemsha hapo lazima itoke gesi grade one!
 
Hatari sheikh. Huoni kuwa unaikosesha mapato serikali yako inayokujengea barabara!
Hii dunia imekuwaje sijui
Hiki kitu nimeongelea masikhara tu ila hata ivyo hayo mapato ninayokosesha serikali ndiyo hayo yakipatikana yanatumika kukandamiza haki za raia wake ?🤔 Au
 
Kuwa mganga mbona hela unapiga tu kwann watu wasijiseme sisi ni WAGANGA WA KIENYEJI mbona hela zipo tu raia watakuja

Sheikh Yahya mpka anaondoka Duniani alikua boss na mihela kibao alikua na Kijiji chake cha wanaomkubali.

Sasa kila siku wachungaji wachungaji wakati ki uhalisia ni ma WITCH DOCTOR
 
Back
Top Bottom