Muundo wa Muungano: Tanganyika tunataka 'Serikali moja, nchi moja, taifa moja'!

Muundo wa Muungano: Tanganyika tunataka 'Serikali moja, nchi moja, taifa moja'!

Hivi, katika hizo serikali tatu ina maana kila mojawapo ya hizo serikali itakuwa na rais wake, makamu wake, pamoja na mabaraza yake ya mawaziri au inakuwakuwaje hasa?

SERIKALI YA TANGANYIKA NA YA ZANZIBAR
101.(1) Kutakuwa na Serikali ya Tanganyika na ya Zanzibar ambazo zitakuwa na mamlaka katika Tanganyika na Zanzibar juu ya mambo yote yasiyo ya Shirikisho kwa mujibu wa Katiba hii;
(2) Serikali ya Tanganyika na ya Zanzibar zitaundwa na kutatekeleza madaraka yake kwa mujibu wa Katiba hii na Katiba ya Tanganyika na Zanzibar;
(3) Kiongozi Mkuu wa wa Serikali ya Tanganyika na pia Kiongozi Mkuu wa Serikali ya Zanzibar ataitwa Gavana wa Tanganyika na Gavana wa Zanzibar;
(4) Kutakuwa na kiapo rasmi cha Gavana wa Tanganyika na cha Gavana wa Zanzibar kitakachosimamiwa na Jaji Mkuu wa Tanganyika na Jaji Mkuu wa Zanzibar ambapo viongozi wote wawili wataapa kuitii, kuilinda na kuitetea Katiba hii, kiapo cha utii mbele ya Rais wa Jamuhuri ya Shirikisho la Tanzania, na kiapo kingine chochote kwa mujibu wa Katiba ya Tanganyika na Katiba ya Zanzibar.

102. (1) Magavana wa Tanganyika na Zanzibar watachaguliwa kwa mujibu wa Katiba ya Tanganyika na Katiba ya Zanzibar;
 
Pole sana Mwanakijiji kwa kuyarudia matapishi yako! Yapo wapi yale madharau na kejeli ulizozielekeza kwa Wazanzibari? Naona ile sitizai niliyokwambia imekuumbuwa.
Mbona umeshachelewa kwani kalamu zenu zimeshafanya kazi ambayo hamkuitarajia?

Leo Iwapi ile Zanzibar bye bye
yako ya siku tatu nyuma?

Muulize kwanini hakumpinga Mbunge na Waziri wa zamani Njelu Kasaka ambae aliongoza orodha ya wabunge 55 mwanzoni mwa miaka ya 90, maarufu kama G55,kudai Serikali ya Tanganyika,hoja iliyopingwa vikali na Rais Mtaafu J.K Nyerere.Kweli sera ya Serikali moja au kuvunja Muungano ni hoja ya Kanisa.Hatushangai,maana Padri John Sivalone alishasema pia kua hata Azimio la Arusha lilikua chaguo la kanisa.
 
Kwa nini tumumunye maneno?
Iwepo serikali moja tu yenye mamlaka kamili,ikishindikana Muungano uvunjike au uwe wa hisani...Hatuwezi kutumia fedha nyingi, rasilimali nyingi na nguvu nyingi kulinda Muungano ambao haupo kwenye mioyo ya hao wanaoungana kwa kuanzisha vijinafasi vya kijanja janja tu....Huo mzigo si ni sisi walipa kodi tunaobebeshwa? Hizi mbili zimeshindikana ya tatu inatoka kwenye ndoa ipi?

Tunatumia akili nyingi na gharama kubwa kubuni vyeo ili kuharmonize situation. Kifalsafa jambo haliwezi kuwapo halafu tena lisiwepo kwa wakati huohuo.

Kama Serikali ya Tanzania itakuwepo, serikali ya Zbar na Tanganyika zifutwe, ibaki hiyo moja tu iwe na mamlaka kamili bara na visiwani.Kama haiwezekani Muungano uvunjike, Zanzibar wapewe nchi yao yenye mamlaka kamili na wajiendeshe wanavyojua na ikiwezekana tuwe na ubalozi wetu kule...
 
Zanzibar wamezoea vya kunyonga. Je vya kuchinja wataviweza?
Zanzibar wamesha zoea kudeka na kujambajamba ili wasitiri matumbo yao.
Kama serikali moja itashindikana tuwaachie kakisiwa chao ambacho akina ardhi ya kutosha yenye rutuba.
Tumewabeba sana wanashidwa kutulia kwenye mbereko. Mara watoe miguu, mara mikono, mara wasimamie tumbo.
Kwani CCM mnaajenda gani ya siri, tujuzeni basi tufahamu.
 
Mimi nasema ndio kwa serikali tatu,nimechoshwa na kelele za wanzanzibar kila siku kulalamika... hata hivyo sioni bado kama kulalamika kutaisha,watakuja na lingine tuuu... eee Mungu tusaidie.
 
tunataka serikali moja tu serikali ya watu wa tanganyika hao wengine hatutaki kuwasikia, waende kupika urojo huko kwao ni wakati umefika ng'ombe akatae kunyonywa na kupe mlalamishi. Hivi kwanza wana faida gani kwa bara hawa wazenji zaidi ya kelele na udini?
fresh tu ila naona wakubwa zako bado wanazidi kutung'ang'ania tu sisi mbona tushasema tuachiwe tupumuwe
 
Katika makala ya Mwanakijiji hakuna sehemu amezungumzia dini, wewe ndiyo umeingiza mambo ya dini kwenye mjadala, kati yako na MM ni nani mfia dini?

Kwani huwezi kuizungumzia Tanganyika bila ya kuitaja?au huwezi ukamzungumzia Dkt.Slaa bila ya kumtaja jina.Fikiri kidogo ewe mwana Tanganyika utaelewa.Msimamo wa "watu wa imani yake" mtoa mada unajulikana.Labda kama mtaendelea kumfumbia fumbo mjinga.
 
Kinadharia serikali moja ndiyo njia ya maana ya kujenga muungano imara. Lakini kiuhalisia ni jambo lisilowezekana. Kwa hiyo kudai serikali moja ni kutaka kuvunja muungano tu sawa na wale wanaotaka muungano wa mkataba.

Tumedai serikali tatu kwa miongo mitatu sasa na tunashukuru tume imeliona hili. Njia ya kupunguza gharama ni kumfanya Rais wa Muungano awe mkuu wa nchi bila kuwa mkuu wa serikali na achaguliwe na Bunge badala ya kuchaguliwa kwenye kura ya jumla. Hivi walivyopendekeza itakuwa ni maajabu kwa sababu kutakuwa na serikali tatu lakini zitakazokuwa na nguvu ya maana kiutendaji ni mbili tu za bara na visiwani. Mwisho wa yote Rais wa Muungano ambaye kimsingi hana nchi atapwaya vibaya sana, na wale wawili wanaweza kumzira na kuachana naye na hao mawaziri wake 15!

Kwa mfumo waliopendekeza walipaswa kuruhusu utawala wa majimbo kwa bara wakati Zanzibar wangeendelea na serikali yao. Sioni namna ambavyo Rais wa Muungano atafanya kazi huku kukiwa na Rais kamili wa Tanganyika.

Sisi tuliopata nafasi ya kuingia kwenye mabaraza ya katiba itabidi jambo hili tulidadavue vyema.

Sijui kwa nini bado tuna "flip flop" na suala la Muungano. Wote tunajua kuwa huu Muungano ni kikwazo kikubwa sana katika ku-design a good, an effective and a responsible governing system.

Kama siyo huu muungano wala tusingekuwa na system, au kujaribu hata kupendekeza system, ya utawala isiyoeleweka, even kufikia extent ya kupendekeza kuwa na ceremonial president.

Watanzania wapewe haki ya kujiamualia through a referendum. Waulizwe kama bado wanapenda kuendelea kuwepo kwa muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Kama hawapendi, basi na Muungano uvunjwe, kila mtu achukue times zake. Kama bado wanapenda Muungano uwepo, basi waulizwe wanapendelea Muungano wa aina gani.

Personally, kuendelea kupendekeza kuwepo Muungano wa serikali tatu, tena with a ceremonial president, ni kukwepa ku-address the core problems za Muungano wa sasa na kuendelea kuendeleza kiini macho cha Muungano.

Najaribu kufikiria idea ya kuwa na ceremonial president kwenye nchi ambayo viongozi wake waliochaguliwa kuwa accountable kwa wananchi, lakini wanafanya kazi zao in a ceremonial way. Sasa itakuwaje kama wakipewa full title ya kuwa ceremonial leaders?

Kwa nchi kama Tanzania, we need a responsible and accountable President, not a ceremonial president. Hatutaki kuwa na Rais ambaye kazi yake itakuwa ni kutembea na mikasi mfukoni kwa ajili kukata utepe kama anavyofanya Makamu wa Rais.

Kama vipi na tusiwe na rais wa aina hiyo kabisa. We aren't that rich to pay for someone simply for doing nothing.
 
Khaa!!! Mzee Mwanakijiji unanishangaza sana. Siku zote wananchi wa kawaida wamekuwa wakisemewa maoni yao na wanasiasa, na hili la serikali tatu lina manufaa kwa wanasiasa wenyewe. Tunamtuma Simba akatununulie mbogamboga badala ya nyama katika sherehe yetu ambayo naye atahusika, Do you think this will workout?? Tusubiri 2015 tutakapokuwa na wagombea uraisi 800,000, Ubunge 5,000,000. na udiwani 45,000,000. :heh:
 
Kwa kweli ni upuuzi; as a matter of fact ni kana kwamba hawajui hesabu za seti! Hivi Mbunge mwanamke atakuwa anawakilisha wanawake tu kwenye hilo jimbo na Mwanaume atawakilisha wanaume watupu?

Niliwahi kuapa kwamba hakuna kitu CCM wanaweza kukifanya kwa maslahi ya nchi bila maslahi yao kuwa mbele. Hao wanawake walioko bungeni sasa ni uozo kiasi wanaweza kuchekelea 1bn kununua makaburi ya viongozi huku wanawake wenzao wakijifungulia chini ya miti, leo tunataka usawa kwenye idadi as if tunafanya mchezo fulani.

Hii tume ni janga, tena janga kuu. Au ni njia ya ku-prolong mjadala kwa nia fulani
 
Muundo na uendeshwaji wa serikali tatu ni mzigo kwa watanzania walalahoi. Tukiwa kama Taifa linalo kabiliwa na changamoto nyingi za kimaendeleo leo hii itakuwa ni vichekesho kuamua kuongeza ukubwa wa serikali na kwamba itasaidiavipi upatikanaji wa maji safi na salama, huduma nzuri mahospitalini nk. na Je gharama hizi atazibeba nani?


Watanganyika pia tunazo kero nyingi tu za muungano nakama lengo lilikuwa ni ujirani mwema na kuwasitiri wenzetu wa Zanzibar na sasa koti limewabana mimi sioni sababu ya kuendelea na muungano huu ambao sasa unaingia dosari. Baba wataifa mwalimu Nyerere aliwahi kukataa mfumo huu ambao Wenzetu wanaupigia chapuo leo hii itakuwa ni uwendawazimu kwa mtanzania mlalahoi kama wewe na mimi kuja na kukukubali mfumo huu wa kinyonyaji.
 
SERIKALI YA TANGANYIKA NA YA ZANZIBAR
101.(1) Kutakuwa na Serikali ya Tanganyika na ya Zanzibar ambazo zitakuwa na mamlaka katika Tanganyika na Zanzibar juu ya mambo yote yasiyo ya Shirikisho kwa mujibu wa Katiba hii;
(2) Serikali ya Tanganyika na ya Zanzibar zitaundwa na kutatekeleza madaraka yake kwa mujibu wa Katiba hii na Katiba ya Tanganyika na Zanzibar;
(3) Kiongozi Mkuu wa wa Serikali ya Tanganyika na pia Kiongozi Mkuu wa Serikali ya Zanzibar ataitwa Gavana wa Tanganyika na Gavana wa Zanzibar;
(4) Kutakuwa na kiapo rasmi cha Gavana wa Tanganyika na cha Gavana wa Zanzibar kitakachosimamiwa na Jaji Mkuu wa Tanganyika na Jaji Mkuu wa Zanzibar ambapo viongozi wote wawili wataapa kuitii, kuilinda na kuitetea Katiba hii, kiapo cha utii mbele ya Rais wa Jamuhuri ya Shirikisho la Tanzania, na kiapo kingine chochote kwa mujibu wa Katiba ya Tanganyika na Katiba ya Zanzibar.

102. (1) Magavana wa Tanganyika na Zanzibar watachaguliwa kwa mujibu wa Katiba ya Tanganyika na Katiba ya Zanzibar;

Umepata wapi hii mbona Rasimu inasema 101.-(1) Kutakuwa na Sekretarieti ya Baraza la Mawaziriambayo itakuwa na jukumu la kuhudumia Baraza la Mawaziri, Kamati
Maalum ya Makatibu Wakuu na kutekeleza majukumu mengine kama
itakavyopangiwa na Baraza la Mawaziri.
(2) Bunge linaweza kutunga sheria kuhusu utaratibu na
utekelezaji wa shughuli za Serikali.
 
"Kila Jimbo la Uchaguzi litakuwa na Wabunge Wawili, 1 mwanamke na mwingine mwanaume". Kweli TZ tunavuta bangi. Kwani Ubunge ni ndoa?

kama suala ni equal representation sijui opportunity ni bora wasema kila jimbo litakuwa na wagombea 2 (to choose from), mwanamke na mwanaume then tunawapigia kura kupata mbunge
 
Muulize kwanini hakumpinga Mbunge na Waziri wa zamani Njelu Kasaka ambae aliongoza orodha ya wabunge 55 mwanzoni mwa miaka ya 90, maarufu kama G55,kudai Serikali ya Tanganyika,hoja iliyopingwa vikali na Rais Mtaafu J.K Nyerere.Kweli sera ya Serikali moja au kuvunja Muungano ni hoja ya Kanisa.Hatushangai,maana Padri John Sivalone alishasema pia kua hata Azimio la Arusha lilikua chaguo la kanisa.

Una taahira iliyo wazi, ila ni vigumu kwa wewe mwenyewe ukiona.

Udini unakusumbua kiasi hata watu wakiwa wanajadili jambo lingine tu kuhusu kuku, basi lazima uanze kuanisha kwamba kuku mwenye ndevu ndefu atakuwa ni wa dini fulani.
 
Having three government is properity toward archeving democracy and this could be through having independent governing state such as Zanzibar and adopting culture,political,and social change accordingly to their expectation and social change,the same in Tanganyika under the umbrella of fedaral state Tanzania.
 
Zanzibar wamezoea vya kunyonga. Je vya kuchinja wataviweza? Zanzibar wamesha zoea kudeka na kujambajamba ili wasitiri matumbo yao. Kama serikali moja itashindikana tuwaachie kakisiwa chao ambacho akina ardhi ya kutosha yenye rutuba. Tumewabeba sana wanashidwa kutulia kwenye mbereko. Mara watoe miguu, mara mikono, mara wasimamie tumbo. Kwani CCM mnaajenda gani ya siri, tujuzeni basi tufahamu.
WEWE BOYA HEBU THUBUTUNI KUTUAHIA ZNZ YETU MUONE KAMA MTATUPATA WASHENzi nyinyi
 
Mkuu mzee mwanakijiji,
Me naona bora kila mmoja we huru tu kwani tunaogopa nini?!
Ila jina la tanzania libakie vilevile kwa maana hakuna haja tena kurudi utanganyika nikimaanisha mtanganyika ni sawa na mtanzania ila mzanzibari sio mtanzania!
 
serikali tatu ama muungano uvunjwe!
nyinyi chadema vipi mbona hamuuitakii mema zanzibar, uislam wake na watu wake?
mkiambiwa ni chama cha kikristo mnakuja juu.
hivi mbona mnaendea kuwakashifu wenzenu kwa majina machafu?
hivi mnapowaita ccm magamba, ama cuf waliberal hamuoni kuwa hamuwatendei haki,
kwa hiyo kwa sababu NKAMIA aliwafananisha na mbwa, Kuanzia sasa na nyinyi muitwe MBWA.
kumaanisha chadema! itapendeza kweli?
acheni dharau!
 
Back
Top Bottom