Muundo wa Muungano: Tanganyika tunataka 'Serikali moja, nchi moja, taifa moja'!

Muundo wa Muungano: Tanganyika tunataka 'Serikali moja, nchi moja, taifa moja'!

WEWE BOYA HEBU THUBUTUNI KUTUAHIA ZNZ YETU MUONE KAMA MTATUPATA WASHENzi nyinyi

Wewe akili zako kama za Wazanzibar wenzako. Kwa kifupi nyinyi ni mapunguani. Akili zenu zipo kuomba omba misaada tu.
Eti Zanzibar itakuwa Dubai ndogo kwa kutegemea misaada ya Maskati, Omani na Falume za Kiharabu.
Mtaaolewa jinsia zote nawaambia na hivi mmesha rojeka kwa kula urojooo
Amueni Zanzibar siyo nchi, ni sehemu ya Tanzania tuishi kwa umoja ili tuwasaidie zaidi
 
Pole pole waHeshimiwa; Uzi huu niwa wote tafadhalini sana maneno machafu na matusi yasitawale humu!!
hapa pana mantiki na manufaa kwa pande zote Wapendwa tuwaheshimu wanaofuatilia humu." LUGHA YETU MOJA hii TAMU"
na wote tunaelewana. kwa vyovote vile hatutakuwa mbali kiGeographia.... !!
kila la heri kwa wote.
 
Wewe akili zako kama za Wazanzibar wenzako. Kwa kifupi nyinyi ni mapunguani. Akili zenu zipo kuomba omba misaada tu.
Eti Zanzibar itakuwa Dubai ndogo kwa kutegemea misaada ya Maskati, Omani na Falume za Kiharabu.
Mtaaolewa jinsia zote nawaambia na hivi mmesha rojeka kwa kula urojooo
Amueni Zanzibar siyo nchi, ni sehemu ya Tanzania tuishi kwa umoja ili tuwasaidie zaidi
Mchana mwema mkuu,Pole pole waHeshimiwa; Uzi huu niwa wote tafadhalini sana maneno machafu na matusi yasitawale humu!!
hapa pana mantiki na manufaa kwa pande zote Wapendwa tuwaheshimu wanaofuatilia humu." LUGHA YETU MOJA hii TAMU"
na wote tunaelewana. kwa vyovote vile hatutakuwa mbali kiGeographia.... !!
kila la heri kwa wote.
 
JameniEeee hapa Siasa inapikwa mie naona hakuna litakalo fanyika, siku zipo tutaona mbele!!
 
Ikiwezekana kila upande uangalie hamsini zake!! Sioni faida za kuwaendekeza Wazenji! Wakae huko, sisi huku, kwisha!!
 
Ndugu zangu

Nina mengi sana ndani ya moyo wangu kuhusu huu mchakato wa katiba (sitaiita mpya kwa sababu sio) na harakati zake ambazo zinaogofya na kutuporomoshea kwenye kuangamiza taifa letu.

Mimi tangu kuzaliwa mpaka leo hii na huu umri alionijalia Maulana nimejitambua, najitambua na naomba Mungu kwa nguvu zote niendelee kujitambua kwamba ni MTANZANIA.

Ni ukweli kwamba mawazo, makusudio na hatimaye utekelezwaji wa kuunganisha watu wa mataifa haya mawili yalichagizwa zaidi na Mwalimu na Mzee Karume. Ila mimi naamini kwa dhati ya moyo wangu kabisa kwamba ule ulikuwa uamuzi sahihi, kwa wakati ule hadi sasa na tuendako kwa muda mrefu sana ujao, licha ya sababu rasmi na zisizo rasmi zilizopekea muungano huu.Ni kweli pia kwamba haikutafutwa ridhaa ya watu wa mataifa haya mawili, ila kama nilivyosema awali, matunda ya viboko vya mama mzazi kunilazimisha niende shule nimeyaona, na sasa mimi na yeye tunafaidi asali ya matunda hayo.

Naomba niulize bila unafiki, jee ni wapi watu wanaotambulishwa kwamba ni wazanzibari walishaulizwa endapo wanataka muungano uvunjike ? Au ni kelele za madebe shinda tuu ? Na kwa upande wa watu wanaotambulishwa kwamba ni watanzania bara nao walishaulizwa wanataka muungano uvunjike ? Au ni mayowe ya wachumia tumbo tuu ?

Hili ni suala zito sana, linachoma sana moyoni. Naomba Mungu leo nisiwe shuhuda wala mshiriki wa kuua nchi yangu, taifa langu, taifa la TANZANIA.Na naomba Mungu historia inishuhudie hivyo.

Namalizia kwa kunukuu maneno ya biblia:

Mithali 5: 9 - 17;

9Usije ukawapa wengine heshima yako, Na wakorofi miaka yako;
10 Wageni wasije wakashiba nguvu zako; Kazi zako zikawa ndani ya nyumba ya mgeni;
11 Nawe ukaziombolea siku zako za mwisho, Nyama yako na mwili wako utakapoangamia;
12 Ukasema, Jinsi nilivyochukia maonyo, Na moyo wangu ukadharau kukemewa;
13 Wala sikuisikia sauti ya waalimu wangu, Wala sikuwategea sikio langu walionifundisha!
14 Nalikuwa karibu na kuingia katika maovu yote, Katikati ya mkutano na kusanyiko.
15 Unywe maji ya birika lako mwenyewe, Na maji yenye kububujika katika kisima chako.
16 Je! Chemchemi zako zitawanyike mbali, Na mito ya maji katika njia kuu?
17 Yawe yako mwenyewe peke yako, Wala si ya wageni pamoja nawe.

Respect !!!
 
Khaa!!! Mzee Mwanakijiji unanishangaza sana. Siku zote wananchi wa kawaida wamekuwa wakisemewa maoni yao na wanasiasa, na hili la serikali tatu lina manufaa kwa wanasiasa wenyewe. Tunamtuma Simba akatununulie mbogamboga badala ya nyama katika sherehe yetu ambayo naye atahusika, Do you think this will workout?? Tusubiri 2015 tutakapokuwa na wagombea uraisi 800,000, Ubunge 5,000,000. na udiwani 45,000,000. :heh:

Kweli kwa rasimu hii karatasi ya kupiga kura itakuwa booklet......
 
Wakenya wameanzisha upuuzi huu kwenye uchaguzi uliopita. Tunalo tatizo la kuiga mambo ya kijinga na kuacha yale yenye manufaa kwa jamii.
Unaweza ukanisahihisha,this is what I know about Kenya constitution;"women representatives are for every county(47) but r elected in all constituencies, i mean voted in all constituency, but represent the whole county just like governor or senator"County tunaweza kuifanananisha na Mkoa(region) hapa kwetu.
 
Sema hapana Serikali "Tatu", Sema ndiyo "Serikali moja". Nchi moja, Taifa Moja, Watu wamoja - nje ya hapo Hapana!!! Tumeshatengeneza ulaji na ukiritimba wa kutosha kwenye serikali mbili halafu tunataka kuongeza serikali ya tatu? Mizigo miwili midogo imetushinda (tunahangaika nayo) halafu magenius wetu wanataka kutupa mizigo mitatu mikubwa!? Kwanini tusiamue kutengeneza mzigo mmoja tu tukaubeba!?

Pamoja na jaribio dhaifu la Tume ya Warioba kupendekeza kuikataa majimbo, pendekezo lao la Katiba Mpya kimsingi linatengeneza majimbo yale yale (States) ambapo kutakuwa na majimbo mawili - Tanganyika na Zanzibar! Kwa sababu kama nchi mbili zimeungana na kuunda 'Shirikisho" basi zile zilizoungana haziwezi kuendelea kuwa nchi tena; zinahamisha hakimiya (sovereignty) yake kwenda kwenye federal government isipokuwa kama kilichoundwa (Shirikisho) siyo nchi!

Kwa kuanzisha mfumo wa Majimbo - Jimbo la Tanganyika litakuwa na nguvu kubwa sana kuliko jimbo la Zanzibar. Lakini kama wakiamua kufanya hali ya sawa katika kuendesha serikali ya Jamhuri ya Muungano Zanzibar itaonewa kwani ikitakiwa kuchangia nusu ya gharama za kuiendesha serikali ya Muungano italalamika mno na sidhani kama Wazanzibari watatakiwa kukubali mfumo huo.

Kwa sababu hiyo njia ya kuimarisha "Muungano" kama lengo ndio hilo basi ni kuingia Serikali Moja ya Kitaifa na Nchi Moja - siyo serikali tatu za kitaifa. Chini ya serikali hiyo moja ya kitaifa (federal government) kutakuwa na serikali za Majimbo (States) ambapo Zanzibar itabakia kama ilivyo (Visiwa vya Mafia, Bagamoyo, Pangani vinaweza kuongezwa huko... I know.. I know.. au ikagawanywa Unguja ikawa kivyake na Pemba kivyake!.) halafu Tanganyika igawanywe kwa States saba hivi ambazo zitaunda 'Regional Governments). Chini ya Regional Governments kutakuwa na "Local Governments" za Miji, Majiji, Vijiji na mifumo mingine ya kujitegemea.

Na maneno mengine mengi....

In short.. Tusikubali serikali tatu za nchi; bali serikali moja, nchi moja, taifa moja na watu wamoja.. Mapendekezo ya Tume ya Warioba kuwabebesha Watanzania mizigo hii ni ya kupingwa, kukataliwa na kupuuzwa.

Yale mameno ya Hayati Nyerere nayoana sasa.......subiri mtaona kama kuna zanzibar, wala CCM, kuna Unguja na Pemba na TANU na ASP vey sooon vyaaja
 
nadhan iandaliwe petition kuonyesha ni kwa jinsi gani watanzania wengi tunataka serikali moja na kama ni ngumu basi muungano uvunjike!!! sielewi hii idea ya serikali 3 hawa watu wa tume wametoa wapi???
 
Ukisema serikali moja lazima na zanzibar waafiki; kama hawaafiki we unaitoa wapi? hata kama ungewapenda vipi, sio afya. Zaidi tutajenga vikundi vya uasi kama boko haram.
Hili ndio tatizo kubwa la Tanganyika tuliorithi; tunapenda sana kushughulika na siasa za nje kuliko ziwagusazo wananchi wa ndani. Badala ya "tutaulinda muungano kwa gharama zozote", tutathimini manufaa na athari za muungano katika amani,usalama, uhuru, uchumi n.k

tragedy of the commons
 
Sintoshangaa nikisikia wananchi wanapendekeza zaidi kuwe na "marahisi" wawili mke na mume! na mawaziri wawiliwali wa kike na kiume, ni mwendo wa kuji-balance balance na kujipa nafasi, bila kufikiri mantiki yake ni nini.
Kwa ujumla mimi naona hio rasimu ni kichekesho kitupu hakuna chamaana kilichopendekezwa! Ni kama watu wametumbua posho kwa posho. Hivi hao wanasheria wame-practice wapi? Khaaa!

Tufikirie nje ya box! Everything has a begining! Nyie mnataka kuiga 2, sio kutoa vyenv viigwe? Kama utaratbu huu haupo kwngne kote bas, mi nawapa hongera kwa uvumbuz. Swala hili halina shda. Logic ni hii
Tunataka tuwe na uwiano wa kijinsia bungeni, hiyo ni njia safi.
Tunataka kupunguza idadi yd wabunge, tunaondoa viti maalum.
Wanawake watatetewa na nani? (mwanamme hawez kumtetea mwanamke kama anavyoweza kujitetea yeye) tutatumia utaratbu huo.
Hatimaye, tuna wabunge wachache bila kupoteza vitu kama watetez wa wanawake, na huku tumekuwa mfano ktk usawa wa kijinsia ktk uongoz.
Pia, wabunge wawil wanaeza gawana mjukumu ya kufuatilia na ufanisi ukaongezeka. Wakafikia wananch moja kwa moja na kwa umdn katka nyanja tofaut tofaut.
Tusipinge vitu kisa ni vipya, tutathibitisha kuwa kufikiri kwetu kuna ukomo!
 
Tunataka serikali moja tu

Serikali ya watu wa TANGANYIKA

Hao wengine hatutaki kuwasikia, waende kupika urojo huko kwao

Ni wakati umefika Ng'ombe akatae kunyonywa na kupe mlalamishi.

Hivi kwanza wana faida gani kwa bara hawa wazenji zaidi ya kelele na udini?sina la kuongea soma hapo halafu uliza sWalihttp://bishopikongo.blogspot.co.uk/2013/04/mtumishi-wa-mungu-kumekuwa-na-maswali.html?m=1
 
Kwa Mtazamo wangu naona Tume imekurupuka katika mambo mawili.
1 Ni suala la muungano na serikali zake, Kumekuwa na malalamiko mengi sana kuhusu Muungano hasa kwa upande wa pili (Zanzibar) kwa maoni yangu hapa nadhani lingekuwepo pendekezo la kupiga kura kuhusu muungano kama wanautaka au la na kama wanaunataka ni wa aina gani?

KUHUSU SERIKALI TATU.
Kama alivyosema ndugu Mwanakijiji kuhusu mzigo wa serikali tatu, napata shida kidogo kujua ni kwa namna gani serikali hizo mbili zitakuwa zinachangia katika serikali ya Shirikisho, kwa muono wangu naona kama kutakuwa kuna upande mmoja utakuwa unaelemewa (unanyonywa na upande mwingine) na hapa unaweza kuwa upande wowote ule either Tz bara au Tz Zanzibar, So kwa misingi hiyo tukisema tuwe na serikali moja ka anavyosema Ndugu Mwanakijiji ni jambo jema ambalo linapunguza matumiz makubwa katika shughuli za utawala na kupeleka gharama hizo katika matumimizi ya maendeleo, LAKINI tuwe wa kweli Je ni kweli Wazanzibari watakubali serikali yao "kufa" ili kufanikisha kuwa na serikali moja? Hasa ukizingatia kwamba kila kukicha wanapigania kupata mamlaka kamili? Tusubiri tuone.

2. KUHUSU BUNGE
kiuhalisia binafsi napinga kuwa na wabunge wawili kila jimbo (Mwanamke na Mwanaume) na hii ni kwasababu haya ni matumizi mabaya ya fedha za walipakodi, hii ni demokrasia ambayo hata kwa mabwana wakubwa ambao walituletea sisi mfumo wa demokrasia na haki sawa kwa wote haupo. Kwa mtazamo wangu Viti maalumu vifutwe na huu utaratibu wa wabunge wawili kila jimbo ufutwe na abaki mmoja kama ni mwanaume au mwanamke wote wapambane na atakayeupata ubunge ndo huyo tuachane na huu mfumo majimbo yenyewe yapo zaidi ya 200 so ukizidisha mara 2 ni wabunge zaidi ya 400 hii kwa kweli hapana hapa warioba anataka kuwatafutia watu ulaji.
Ni Mtizamo wangu kama Mtanzania.
 
Mkuu Mwanakijiji,
Na hili hili la wabunge wawiliwawili (jinsia tofauti) kwa jimbo unalionaje? Mbona kwa wenzetu waliotutangulia kwenye maswala ya demokrasia hatujawahi kusikia upuuzi huu? Kituko tulicholetewa na Warioba hakilingani na gharama tulizowalipa.
Wanawake ni mtaji wa ccm ili isife kwa kukosa maspika na mawaziri wa kuipigia kampeni inawekeza kwa wanawake kiujumla huu ni upuzi na ujinga uliomithilika tunataka kutawaliwa na watu wenye uwezo bila kujali jinsia na sio kuingiza pumba kwa visingizio vya jinsia tumeliwa kwenye uspika na kama watu hawajifunzi waendelee kukumbatia pumba za kina warioba za wabunge wawiliwawili
 
Mzee Mwanakijiji hii hoja ni zaidi ya upuuzi, huu ni usawa kweli au tunataka kuongeza mzigo kwenye serikali? Kuna maana gani ya kuwa na wawakilishi wa jinsia mbili tofauti katika jimbo moja? Kwenu bungeni wanaenda kuwakilisha jinsia au maoni na matatizo ya wananchi wao? Tunaabudu jinsia au tunataka maendeleo? Huu usawa nao wa kijinsia tusipouangalia vizuri, tunatengeneza bomu lingine la kudidimiza nchi!!! Nimekerwa na hili pendekezo! :heh:

Hili mara nyingi huwa inanisumbua.
Hivi kuna tatizo gani? Maana kwa kumbukumbu zangu Wanawake ndio wengi kuliko wanaume hivyo hoja ya kuwa wapewe Upendeleo haina mantiki maana wananafasi ya kujisimamia!
 
Back
Top Bottom