SMU
JF-Expert Member
- Feb 14, 2008
- 9,613
- 7,889
Tulikosea tangu mwanzo wakati ToR zinatolewa. Tume ya Warioba kimsingi ilikuwa inafungwa na yafuatayo:
Misingi 9(2)
Tume itaongozwa na misingi mikuu ya kitaifa na maadili ya jamii ya kuhifadhi na kudumisha mambo yafuatayo:-
i. kuwepo kwa Jamhuri ya Muungano;
ii. uwepo wa Serikali, Bunge na Mahakama;
iii. mfumo wa kiutawala wa kijamhuri;
iv. uwepo wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar;
v. umoja wa kitaifa, amani na utulivu;
vi. uchaguzi wa kidemokrasia wa mara kwa mara katika vipindi maalum kwa kuzingatia haki ya watu wote wenye sifa ya kupiga kura;
vii. ukuzaji na uhifadhi wa haki za binadamu;
viii. utu, usawa mbele ya Sheria na mwenendo wa sheria;
ix. uwepo wa Jamhuri ya Muungano isiyofungamana na dini yoyote na inayoheshimu uhuru wa kuabudu; na
x. kutoa fursa kwa wananchi kutoa maoni yao kwa uhuru kwa lengo la kuendeleza na kuboresha masuala hayo 9(3).