Muundo wa Muungano: Tanganyika tunataka 'Serikali moja, nchi moja, taifa moja'!

Muundo wa Muungano: Tanganyika tunataka 'Serikali moja, nchi moja, taifa moja'!

Hayohayo 400 ambayo ni madogomadogo yanawashinda... Yakiongezwa ukubwa watayaweza kweli??

Labda, ila ikipita itabidi watanzania wawe wanafanya uchaguz makini! Na wakiwa wawili wanaweza gawana mambo ya kufuatilia ili wawe efficient zaid
 
Kwa kuangalia kwa undani inaonekana dhahiri kuwa tumepotea njia na tulikotarajia kwenda hututafika kabisa. Kwa kupotea kwetu, wenzetu tulioanza nao safari kwa lengo la kufika kumoja wao waliamua mapema kutuacha na kubadili uelekeo ambao kwao wanaamini kuwa utawafikisha mahali salama na sahihi zaidi kuliko ilivyodhaniwa awali wakati tunaanza safari yetu pamoja.

Jambo la kujiuliza ni kuwa, kama tuliokubaliana awali kuwa kwenye safari moja walishaamua kutuacha na kufuata njia wanayoijua wao; mbona tunaendelea kujiaminisha kuwa wako pamoja na sisi ilhal sivyo ilivyo?. Kama tumeshagundua tumepotea na uhakika wa kufika tulikotarajia haupo, kwa nini basi tusirudi kule tulikoanzia safari yetu ili tukajipange upya. Yawezekana miongoni mwetu hawajui tulikoanzia hii safari lakini hilo lisitufanye tushindwe kurudi kwani bado miongoni mwetu wako wanaojua tulikoanzia.

Ni dhahiri kuwa miongoni mwa tulioanza nao safari hawataki wazo la kurudi tulikoanzia aidha kwa kuona aibu ama kwa woga wao tu. Lakini aibu ama woga wao usitufanye tuendelee kuhangaika na kumangamanga njiani huku tukiendelea kujidanganya kuwa iko siku tutafika tulikotarajia. Kama wao wanaona aibu ama woga kurudi kule tulikoanzia ni bora tukawaacha kwani naamini miongoni mwetu bado wamo baadhi wanakumbuka tulikoanzia na jinsi tulivyoianza safari yetu na wako tayari pia kujumuika nasi na hata kutuelekeza namna ya kurudi ili tukaianze upya safari yetu.

Kule tulikotoka kuna baadhi ya vitu kama hivi tuliviacha, tuvirudie ili tuangalie vyema kama vinaweza kutusaidia katika kupanga safari nyingine.

View attachment The Tanganyika (Constitution) Order in Council, 1961.pdf
View attachment Independence of Tanganyika.pdf
 
Swala hili halina shda. Logic
ni hii
Kama tunataka tuwe na uwiano wa kijinsia
bungeni, hiyo ni njia safi.
Tunataka kupunguza idadi yd wabunge,
tunaondoa viti maalum.
Wanawake watatetewa na nani?
(mwanamme hawez kumtetea mwanamke
kama anavyoweza kujitetea yeye)
tutatumia utaratbu huo.
Hatimaye, tuna wabunge wachache bila
kupoteza vitu kama watetez wa
wanawake, na huku tumekuwa mfano ktk
usawa wa kijinsia ktk uongoz.
Pia, wabunge wawil wanaeza gawana
majukumu ya kufuatilia na ufanisi
ukaongezeka. Wakafikia wananch moja
kwa moja katka nyanja
tofaut tofaut.
 
Tunataka serikali moja tu

Serikali ya watu wa TANGANYIKA

Hao wengine hatutaki kuwasikia, waende kupika urojo huko kwao

Ni wakati umefika Ng'ombe akatae kunyonywa na kupe mlalamishi.

Hivi kwanza wana faida gani kwa bara hawa wazenji zaidi ya kelele na udini?
kabisa mkuu, i hate these agnorance people, wanaweza uraramishi tu na majungu...... napenda hata kwenye sarafu wawaache wajitegemee then tuone mwisho wao.
 
Kinakuja sasa siyo Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, bali ni ama Shirikisho la Tanzania, au Jumuia ya Madola ya Tanzania.

Kama kweli tunataka kuwa na serikali mbili zenye nguvu sawa, ni afadhali tuvunje muungano na kubaki na ule wa afrika ya mashariki tu. Sidhani kama kweli kuna faida yoyote ya kuendelea na muungano wa ain hii. Urusi walishindwa wakavunja muungano huo, na matokeao yake nchi ndogo ndogo zilizokuwa kwenye muungano huo, wengine waliendelea sawasawa na wengine wakayumba sana hadi kufikia mapigano ya wenyewe kwa wenyewe. Nchi zote zenye federations zina wanachama wengi wenye nguvu karibu sawa, angalia mifano kama Canada, Australia, na Marekani. States zake ni nyingi na zina nguvu karibu sawa. Federal union ya nchi mbili tu ambamo moja ni kubwa sana na nyingine ni ndogo sana itakuwa ni ngumu sana kwa sababu ama nchi ile kubwa itabeba mzigo mkubwa wa kuendesha federal governement na hivyo kuwa na nguvu kubwa dhidi ya ile nchi ndogo, au nchi zote zigawane mzigo huo nusu kwa nusu na hivyo kuibebesha ile nchi ndogo mzigo mkubwa zaidi ya uwezo wake.

Muundo mzuri ungekuwa ni kuunda nchi moja yenye serikali moja ambamo raia wake wote wana haki sawa bila kujali wanatokea sehemu ipi ya muungano, na ili kuhakikisha kuwa element ya uzanzibar na ubara inatoweka, ingekuwa ni vyema visiwa vya zanzibar vikaunganishwa ama na mkoa wa Tanga na kuuita mkoa wa Zanzibar, hivyo mtu kusema katokea Zanzibar isiwe na maana ya moja kwa moja kuwa katokea visiwani.

Hata hivyo wakati wote ni vizuri kutolazimisha mambo ya kisiasa. Iwapo wananchi wanataka kusiwepo muungano, basi tuuvunje. Nikiwa nimetokea bara, sijawahi kuona faida yoyote ya muungano katika maisha yangu binafsi. Nimeona jamaa tuliosoma nao wakiwa wanapewa madaraka kirahisi sana huko zanzibar na baadaye kuingia kwenye serikali ya muungano kuliko wale bara. Mbunge mmoja anayewakilisha watu wasiofikia hata 1000 huko Zanzibar huwa ana sauti sawa na mbunge mmoja wa bara anayewkailisha watu zaidi ya laki tatu.
 
Kwa mtazamo wangu uwezekano wa Wazanzibar kuridhika without zanzibar being sovereignty state haupo, si ni juzi tu tumesikia Maalima anaomba sarafu yao, mambo ya nje yao?? so siungi mkono serikali tatu mbili wala moja naona tukubali tu kwamba Muungano umefika mwisho! kila mmoja ajikate kivyake.

Inashangaza sana timing ya Maalim Sefu kuorodhesha mambo wayatakayo siku chache kabla ya rasimu kutoka. Inawezekana Wazanzibari ndani ya tume walirikisha information ya mambo yaliyopendekezwa kwenye rasimu na kwa hivyo ni indication ya kile wakitakacho Wazanzibari, rasimu hii kwa Hakika itakataliwa na Wazanzibari kwani wao wanataka Serikali huru and issue ya Serikali moja ni next to impossible, HAITAWEZEKANA kamwe, la msingi kila mtu achukue chake and I wonder Kama kutakuwa na mgawanyo wa Mali za Serikali ya Muungano Muungano ukivunjika
 
Hivi kwanini CCM upande wa Tanganyika Wanawang;ang'ania sana huu Muungano.
Kwanini tusiuvunje na Kulilia Kuungano na Rwanda??????
 
[h=5]Sema hapana Serikali "Tatu", Sema ndiyo "Serikali moja". Nchi moja, Taifa Moja, Watu wamoja - nje ya hapo Hapana!!! Tumeshatengeneza ulaji na ukiritimba wa kutosha kwenye serikali mbili halafu tunataka kuongeza serikali ya tatu? Mizigo miwili midogo imetushinda (tunahangaika nayo) halafu magenius wetu wanataka kutupa mizigo mitatu mikubwa!? Kwanini tusiamue kutengeneza mzigo mmoja tu tukaubeba!?[/h]Pamoja na jaribio dhaifu la Tume ya Warioba kupendekeza kuikataa majimbo, pendekezo lao la Katiba Mpya kimsingi linatengeneza majimbo yale yale (States) ambapo kutakuwa na majimbo mawili - Tanganyika na Zanzibar! Kwa sababu kama nchi mbili zimeungana na kuunda 'Shirikisho" basi zile zilizoungana haziwezi kuendelea kuwa nchi tena; zinahamisha hakimiya (sovereignty) yake kwenda kwenye federal government isipokuwa kama kilichoundwa (Shirikisho) siyo nchi!

Kwa kuanzisha mfumo wa Majimbo - Jimbo la Tanganyika litakuwa na nguvu kubwa sana kuliko jimbo la Zanzibar. Lakini kama wakiamua kufanya hali ya sawa katika kuendesha serikali ya Jamhuri ya Muungano Zanzibar itaonewa kwani ikitakiwa kuchangia nusu ya gharama za kuiendesha serikali ya Muungano italalamika mno na sidhani kama Wazanzibari watatakiwa kukubali mfumo huo.

Kwa sababu hiyo njia ya kuimarisha "Muungano" kama lengo ndio hilo basi ni kuingia Serikali Moja ya Kitaifa na Nchi Moja - siyo serikali tatu za kitaifa. Chini ya serikali hiyo moja ya kitaifa (federal government) kutakuwa na serikali za Majimbo (States) ambapo Zanzibar itabakia kama ilivyo (Visiwa vya Mafia, Bagamoyo, Pangani vinaweza kuongezwa huko... I know.. I know.. au ikagawanywa Unguja ikawa kivyake na Pemba kivyake!.) halafu Tanganyika igawanywe kwa States saba hivi ambazo zitaunda 'Regional Governments). Chini ya Regional Governments kutakuwa na "Local Governments" za Miji, Majiji, Vijiji na mifumo mingine ya kujitegemea.

Na maneno mengine mengi....

In short.. Tusikubali serikali tatu za nchi; bali serikali moja, nchi moja, taifa moja na watu wamoja.. Mapendekezo ya Tume ya Warioba kuwabebesha Watanzania mizigo hii ni ya kupingwa, kukataliwa na kupuuzwa.

naunga mkono hoja.
"a wise man will be master of his mind, a fool will be its slave"
 
hahaha, mkuu nafikiri hujafikiria vyema, kumtupia lawama la ubaguzi wa kidini mzenji sikuelewi; na kuhusu serikali ya tanganyika yatupasa kwanza tuungane tuvunje huu muungano
 
Kwani hii katiba haijaamua kuvunjwa kwa muungano...muungano mwisho mwaka huu...wale wa kule wanatuongezea tu idadi ya kura za urais
 
Huwezi kuleta maswala mazito kama haya na kuwakabidhi kura ya turufu viongozi wachovu na goegoe kama tulionao. Hilo la EA linawashinda wataweza hili la Zanzibar. Zanzibar ni kisiwa cha viongozi wanashibisha matumbo yao kwa kutafuna pesa za walipa kodi wa hii nchi tena hawana aibu. Mikataba yote mibovu ni chimbuko la mzee rukhsa aliyetuletea hili jinamizi la Ki k w e r e. We need a revolution.
 
"Kila Jimbo la Uchaguzi litakuwa na Wabunge Wawili, 1 mwanamke na mwingine mwanaume". Kweli TZ tunavuta bangi. Kwani Ubunge ni ndoa?
Tena bangi zenyewe tunavutia chooni ukichanganya na harufu ya mav..... Ndio inaleta ukichaa ghafla,hivyo huyo mwanamke na mwanaume ndio wanatoka vyama viwili tofauti ama?mf mwanaume Chadema,mke magamba ama?warioba tunaomba ufafanuzi wa hili..
 
Naona ufufuo wa Tanganyika unanukia. Welcome back my country Tanganyika.
 
Una taahira iliyo wazi, ila ni vigumu kwa wewe mwenyewe ukiona.

Udini unakusumbua kiasi hata watu wakiwa wanajadili jambo lingine tu kuhusu kuku, basi lazima uanze kuanisha kwamba kuku mwenye ndevu ndefu atakuwa ni wa dini fulani.
Njela kasaka na G55 walidai serikari ya tanganyika lakini Pia walitaka serikari Tatu Ndio Maana Nyerere aliwapinga
 
Nyerere aliukataa muundo wa serikari tatu tena Miaka ile ya Analogia iweje kipindi cha hiki cha Digtal tusiyaenzi maoni ya Nyerere ?
 
[h=5]Sema hapana Serikali "Tatu", Sema ndiyo "Serikali moja". Nchi moja, Taifa Moja, Watu wamoja - nje ya hapo Hapana!!! Tumeshatengeneza ulaji na ukiritimba wa kutosha kwenye serikali mbili halafu tunataka kuongeza serikali ya tatu? Mizigo miwili midogo imetushinda (tunahangaika nayo) halafu magenius wetu wanataka kutupa mizigo mitatu mikubwa!? Kwanini tusiamue kutengeneza mzigo mmoja tu tukaubeba!?[/h]Pamoja na jaribio dhaifu la Tume ya Warioba kupendekeza kuikataa majimbo, pendekezo lao la Katiba Mpya kimsingi linatengeneza majimbo yale yale (States) ambapo kutakuwa na majimbo mawili - Tanganyika na Zanzibar! Kwa sababu kama nchi mbili zimeungana na kuunda 'Shirikisho" basi zile zilizoungana haziwezi kuendelea kuwa nchi tena; zinahamisha hakimiya (sovereignty) yake kwenda kwenye federal government isipokuwa kama kilichoundwa (Shirikisho) siyo nchi!

Kwa kuanzisha mfumo wa Majimbo - Jimbo la Tanganyika litakuwa na nguvu kubwa sana kuliko jimbo la Zanzibar. Lakini kama wakiamua kufanya hali ya sawa katika kuendesha serikali ya Jamhuri ya Muungano Zanzibar itaonewa kwani ikitakiwa kuchangia nusu ya gharama za kuiendesha serikali ya Muungano italalamika mno na sidhani kama Wazanzibari watatakiwa kukubali mfumo huo.

Kwa sababu hiyo njia ya kuimarisha "Muungano" kama lengo ndio hilo basi ni kuingia Serikali Moja ya Kitaifa na Nchi Moja - siyo serikali tatu za kitaifa. Chini ya serikali hiyo moja ya kitaifa (federal government) kutakuwa na serikali za Majimbo (States) ambapo Zanzibar itabakia kama ilivyo (Visiwa vya Mafia, Bagamoyo, Pangani vinaweza kuongezwa huko... I know.. I know.. au ikagawanywa Unguja ikawa kivyake na Pemba kivyake!.) halafu Tanganyika igawanywe kwa States saba hivi ambazo zitaunda 'Regional Governments). Chini ya Regional Governments kutakuwa na "Local Governments" za Miji, Majiji, Vijiji na mifumo mingine ya kujitegemea.

Na maneno mengine mengi....

In short.. Tusikubali serikali tatu za nchi; bali serikali moja, nchi moja, taifa moja na watu wamoja.. Mapendekezo ya Tume ya Warioba kuwabebesha Watanzania mizigo hii ni ya kupingwa, kukataliwa na kupuuzwa.

Akili yao ni pwani ya hariri km 10 toka pwani ya bahari ya hindi ni znz na ndo mpaka wanadai ulipo roughly ni mpaka lugalo hivi..

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Kwa nini viongozi wa CCM wanang'ang'ania muungano?

Jibu kwanza kwanini viongozi wa CUF wanang'ang'ania muungano uvunjike?

Unakumbuka siku zote walikua wanadai haki ya kujitegemea katika mambo ya kiuchumi hasa eti ''MAFUTA YAO'' yote hayo rasimu imeyatatua lakini hawaishi kulalamika. Mi naona tatizo ni Maalim, serikali 1, 2, au 3 zote zitalalamikiwa na huyu Mnafiki. Zinahitajika kampeni za makusudi za kuweka wazi huu unafiki ili wazanzibar wasiendelee kuburuzwa na huyu jamaa.
 
wanaong'ang'ania muungano ni watanzania sio viongozi wa ccm.. tume ya katiba ina wajumbe wa vyama vyote akiwemo baregu wa chadema na ile iliyosomwa na warioba ni taarifa ya tume ya katiba mpya..acha uzuzu

Warioba alisema watanzania wengi tu walitaka muungano uvunjike kabisa au muungano wa mkataba. Lakini kwa sababu sheria ya marekebisho ya katiba ilishawakataza kuhukua option yoyote inayelenga kuvunja muungano, maoni hayo hawakuyatilia maanani. Sasa kama unabisha tena kuwa sheria ya mabadiliko ya katiba haikutungwa na serikali ya CCM na kupitishwa na wabunge wake, basi utakuwa hufundishiki...
 
Back
Top Bottom